Namfuye wa Mianzini
Senior Member
- Sep 4, 2023
- 170
- 179
Huenda vya kurithi vimezidi, Mwl JKN alisifiwa sana kiasi kwamba ilikuwa ukitofautiana nae unaonekana adui na hapo ndio ilikuwa punde tu baada ya kutuongoza kupata uhuru, Mwinyi yeye alidharaulika zaidi ukizingatia mtangulizi wake alikuwa mwl hivyo ikawa kana kwamba Mwinyi ni Raisi Mjinga Mjinga hivi aisie na maana kuna wakati hadi mwalimu mwenyewe akimnanga, alipokuja Mkapa nae hakukubali kukosolewa huenda umesahau, aaah alipokuja mkwere yeye ndio Kiki zikazidi Rais Handsome na kijana, hao wengine waliofuata umewataja.Nikiwa ninapata utambuzi wa akili Nimebahatika Kushuhudia Uongozi wa mwisho wa Mwalimu Nyerere, Uongozi wa Mwinyi, Uongozi wa Mkapa wote, Uongozi wa kikwete.
Katika Uongozi wote huo sikuwahi kuona vijana na Viongozi wakisifiwa Kama wanavyosifia kwenye uongozi wa Magufuli na Rais Samia.
Kukiwa na Sukari imeletwa na serikali bhasi utasikia "Tunamshukuru Samia" ikinyesha Mvua Tunamshukuru Magufuli kwa mvua"..
Kuna yule jamaa Mwaka fulani ilitokea kupatwa kwa Jua kama siumbuki mwala 2017 bado akasema anamshukuru Magufuli kwa kuleta kupatwa kwa Jua.
Hii kitu iko serious na inapunguza uwajibikaji kwa Viongozi.
viongozi wengi wanaowajibika hawatafuti kusifiwa sana bali wanatafuta kuacha Legacy.
Au mimi ndo Nimezeeka na sijui modern political zinaendaje?
Sikuwahi kuona Mkapa akisifiwa na ndo alifanya makubwa sana pengine kuliko hata Marais wote..
Nyerere alikuwa na honorary PhD ila hakuwahi kukubali kuitwa Dr Nyerere, Mwinyi alikuwa na PhD ila hakutka kuitwa Dr Mwinyi, Mkapa alikuwa na PhD naye pia hakutaka.
Tatizo liko wapi..
Vipi mbona Ruto ana PhD na sijawahi kusikia akiitwa Dr Ruto..
Hivi ni mimi ndo sielewi au uzee ndo unanichanganya?
Suala la Honorary PhD lilikuwepo pia, kina Mzindakaya wakiitwa kabisa Dr pasina hata kufika chuo kikuu, lakini mimi nakubaliana na wewe na wakati tulionao hata hao wenye PhD za darasani ni watupu hasaa, zamani Degree tu ikitema madini unaielewa Leo mtu mwenye PhD ni kama form four failure