Kuna tatizo la kiufundi mahali kwenye kizazi hiki tukubali au tukatae au ni njia mpya ya siasa?

Huenda vya kurithi vimezidi, Mwl JKN alisifiwa sana kiasi kwamba ilikuwa ukitofautiana nae unaonekana adui na hapo ndio ilikuwa punde tu baada ya kutuongoza kupata uhuru, Mwinyi yeye alidharaulika zaidi ukizingatia mtangulizi wake alikuwa mwl hivyo ikawa kana kwamba Mwinyi ni Raisi Mjinga Mjinga hivi aisie na maana kuna wakati hadi mwalimu mwenyewe akimnanga, alipokuja Mkapa nae hakukubali kukosolewa huenda umesahau, aaah alipokuja mkwere yeye ndio Kiki zikazidi Rais Handsome na kijana, hao wengine waliofuata umewataja.

Suala la Honorary PhD lilikuwepo pia, kina Mzindakaya wakiitwa kabisa Dr pasina hata kufika chuo kikuu, lakini mimi nakubaliana na wewe na wakati tulionao hata hao wenye PhD za darasani ni watupu hasaa, zamani Degree tu ikitema madini unaielewa Leo mtu mwenye PhD ni kama form four failure
 
KIzazi chawa...
Kizazi lamba miguu...
Kizazi kiliponzwa na vitisho vya mwendazake magu na wabunge wake wajinga,wamchongo na waoga sifiasifia ili upate cheo.
Niupepo mchafu but utapita tukipata prezdaa msomi, mwenye akili na anayejiamini.
Hauwezi kupita hadi Adabu ishikwe, kikanuni - kizazi imara/elevu huzaa kizazi dhaifu na kinyume chake kizazi dhaifu huzaa kizazi imara, ile first generation ya Tanganyika ilikuwa na watu hasaa ukimsikiliza mtu wa middle school (aliyeishia hapo) anazungumza unamuelewa Leo hii unasikiza PhD unasikitika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…