Kuna tatizo mahali, dola hakuna sekta binafsi zinakufa

Kuna tatizo mahali, dola hakuna sekta binafsi zinakufa

Kwa sasa hivi pesa ya kigeni hususani dola haipatikani hata kwenye mabenki ambayo sekta zetu binafsi zinafanya nazo biashara. Mambo yanakwama inapofika kuagiza mahitaji kutoka nje ambavyo ni sehemu ya utekelezaji wa kazi yoyote au mradi. Hata dola 1000 kupata ni tatizo.

Je, kitu gani kinaendelea? Mimi na umri wangu mkubwa tumepitia changamoto nyingi za kiuchumi toka enzi za Mwalimu lakini jambo kama hili halikuwahi kutokea. Sasa tunaelekea wapi? Mbona hata hakutolewi tamko kuelezea hili jambo? Je, waziri wa fedha haoni kwamba hili ni tatizo?

Miaka michache ya nyuma na hususan wakati wa Hayati Magufuli tulikuwa tunapewa taarifa kuwa nchi yetu ina akiba ya kutosha na wakawa wanataja hata kipindi ambacho kama itokee dhiki ya namna gani, kwa akiba iliyopo tungeweza kumudu kuagiza nje kwa miezi kadhaa. Sasa hii akiba imeenda wapi?

Jamani tuzidi kujitafakari, kuna tatizo mahali.
Sio kweli
 
Tupunguze uagizaji wa vitu visivyo vya ulazima..

Kwa tuagize furniture nje?
Kwa nini tuagize toothpick china?
Kwa nini tuagize mapambo ya plastic nje?
Kwa nini tuagize mchele toka nje?
Kwa nini tuagize vitu tunavyoweza kufanya uzalishaji hapa ndani?
Kwa nini tufanye matumizi makubwa kuliko uwezo wetu?
Tupunguze ukubwa wa Serikali yetu-Tupunguze Wizara,Tu fanye merging ya idara,Kurugenzi.
Tupunguze safari zisizo za lazima
Nimekuelewa
 
Kwenye benki hupati zaidi ya dolar 200 ,sasa imagine dollar 200 ndiyo limit .
Yaani dollar 200.
Na huipati Kwa chini ya 2900 hadi 3000
Kutoka kwa rate ya 2200-3000 ndani ya miezi michache tu .
Hii si indicator ya economic failure ?
Sio kweli
 
Nguvu kubwa zinatumika kukusanya kodi kufikia Malengo ya makusanyo mwisho wa mwaka wa fedha yamkini maandalizi ya uchaguzi mkuu..nadhani matumizi yanapaswa kudhibitiwa haswaa..Wizi pia matumizi mabaya.

Wafanyabiashara Wapo hoi..hatua Za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kunusuru madhara zaidi Kwa uchumi na taifa..
 
Back
Top Bottom