Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

mimi sijachukua chochote kutoka kwenye biblia lakini naamini bila shaka imeelezwa kuwa duniani ni sehemu ya mtihani na majaribio wala si sehemu ya kudumu, uhalisia ndio huo tumeumbwa ili tujaribiwe ni nani mwenye vitendo vizuri zaidi na hata hao uliowataja walipewa mitihani ibrahim alikosa mtoto kwa miaka mingapi!? unadhani ni starehe au jaribio?!....kwa kukazia huyo shetani yuko overrated hana umalaika wowote ni jini kama majini wengine sema yeye ana uwezo kwa makusudio maalum ila kwa mtu mchamungu ni mwepesi kama nzi tu..
 
Sikuhizi weye mgonjwa unaandika vitu havieleweki au umewehuka?
 
Wacha waloz waje
 
Hivi huyo mkuu wa anga ni nani? Hapa kuna jirani yangu kila akisali anasema ANAMTEKA MKUU WA ANGA. Yaani leo anamteka, kesho anamteka tena wala hatusikii lini huyo mkuu wa anga amekimbia mateka

hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mkuu umeniacha hoi
 
nijibu haya maswali

1. nani alie tuumba?

2.dhumuni la alie tuumba ni nini?

3.je dhumuni la alie tuumba sisi ni tuteseke na hizi shida za duniani na maangaiko yake ambayo unaita ni mitihani/majaribio??

tuanzie hapo ukijibu nadhani tutafikia muafaka mimi na wewe.
 
SOMA VIZURI HIYO SEHEMU ULIYOANDIKA " Umulike hata nje ya Mipaka yetu" maana yake ndni ya mipaka yetu limezingatiwa.
Unajidanganya tu. Mtakuja kusema pia Azimio la Arusha lilikuwa kafara, Azimio la Musoma na Iringa yote makafara.
Vilaza kweli wako wengi. Japo wana Tanu /ccm walieleza dhamira ya Mwenge na ilerleweka kizazi cha leo kinahusicha na matambiko.
Duu hatare
 
sawa kwa ufupi, alietuumba sisi na vitu vyote ni mwenyezi mungu na madhumuni ya kutuumba si kumnufaisha au kumpa faida yeyote bali ametuumba ili tu tumuabudu yeye peke yake....sasa eneo la kuishi ni duniani kama jina lilivyo ni eneo duni na lisilo thamani starehe zake hazidumu na neema zake vilevile bali mambo hapo huenda kwa noba leo furaha na shangwe kesho matatizo na huzuni hayo ndio maisha ya duniani na si kwa kuwadhulumu au kuwaonea hao viumbe wake bali kwa kuwapa mtihani na kuwajaribu ni nani atafanya vitendo vizuri zaidi na ni nani atakuwa mwenye subra na uvumilivu..

kisha baada ya kurudi kwake ambapo ndipo tulipotoka hapo awali tutakwenda kulipwa uzuri kwa uzuri zaidi na ubaya kwa ubaya zaidi...na twendapo juu ya maneno haya utambue hapa duniani sio kwetu hatukuandikiwa kuishi hapa milele, laiti ukiona maisha yalivyo mafupi na yasivyodumu utazingatia ninachokisema..

shukran..
 
Mkuu, hapa kuna Tunu za Taifa. Ni vema histotia ya Taifa ibaki kama ilivyo, na lisipunguzwe neno katika sentesi kwa nia ya kuleta mkanganyo.

Kabla ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Baba wa Taifa Hayati Mwl.J K.N. pamoja na mambo mengine, alifanya mambo mawili ya msingi., (1)aliwasilisha UN ramani ya Tanganyika. Ilipokelewa na hakuna aliyeihoji. Hata baadaye, chokochoko ya ziwa Nyasa ni la Malawi., mlima Kilimanjaro na North Mara (Tarime&Rorya) ni sehemu ya Kenya., mpaka wa Burundi na Tanganyika upo Kahama, hivyo Kigoma na baadhi ya maeneo ya Tabora na Katavi ni sehemu ya Burundi zilikosa mashiko.
(2) alihutubia kikao cha UN na kueleza, nanukuu "SISI TUNATAKA KUWASHA MWENGE, NA KUUWEKA JUU YA MLIMA KILIMANJARO. UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU, ULETE TUMAINI, PALE AMBAKO HAKUNA MATUMAINI, UPENDO MAHALI AMBAKO PANA CHUKI, NA HESHIMA AMBAKO PAMEJAA DHARAU. Na huu ulikuwa msingi mkuu wa Sera ya nje ya Tanganyika.
Baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Baba wa Taifa aliamini na aliwaeleza wananchi kuwa Tanganyika haiwezi kuwa huru, kama nchi nyingine zitakuwa chini ya ukoloni na utawala wa mabavu. Na ndio ukawa mwanzo wa kuunga mkono jitihada za ukombozi kusini mwa Afrika, Sahara Magharibi, Biafra na hata Palestina.

Ufafanuzi zaidi utaupata endapo utatafuta, nini maana ya:-
~Ramani
~Bendera
~Ngao/Nembo ya Taifa @ bi & bw
~Twiga
~Mwenge wa Uhuru
Ikiongezeka na Lugha ya Kiswahili, Umoja na Amani

Ni maoni yangu,
 
kuhusu dhumuni la kutuumba hupo sahihi lakini pengine umepuyanga .

Maana aujasema bado chanzo cha binadamu kufukuzwa bustanini!!

ulichoeleza hapo ni kwamba MUNGU alikusudia kutuleta kwwnye ulmwengu wa mateso moja kwa moja.mkuu nakwambia bado unaitaji kujifunza nakuukubali ukweli sio kupinga tu.
 
Nimeishia kusoma hapo ulipoandika hili badala ya ili..
Nikasema huyu nae ni mmojawapo wa wajinga wa humu jf.
Get some time to school yourself the way you write a single sentence.
 
Nimeishia kusoma hapo ulipoandika hili badala ya ili..
Nikasema huyu nae ni mmojawapo wa wajinga wa humu jf.
Get some time to school yourself the way you write a single sentence.
sio shida ni makosa madogo tu ya kiuandishi yanayo tokana na kasi ya mwandishi.
 
Kaka itabidi ufanye utafiti tufahamu hili la Lindi ilikuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…