Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #261
Unajaribu kujibu kwa kuchanganya mambo mengi kwa wakati mmoja mwisho unaishia kukosa jibu sahihiKwa maana yenye kujitosheleza kuhusu uongo, uongo ni kinyume cha ukweli,na ukweli ni kauli au kitendo kuafikiana na hali halisi.
Kipimo cha uongo na ukweli uzani wake ni HALI HALISI,yaani vyote hurejea huko,kwenye hali halisi kuna elimu na maarifa. Leo hii utabaki kuwa muongo unapo dai ya kuwa hakuna taifa lililo simama nje ya njia hizo ulizo zitaja huku uhalisia ukiwa dhidi yako.
Mimi tangu na balehe najifunza mambo ya ushirikina na uchawi na namna ya kuyaeupuka na najifunza elimu ya kumpwekesha Mola wangu,na hizi elimu naendelea kuzisoma mpaka pale nitakapo rejea kwa Mola wangu.
Asilimia za uongo na ukweli nazijua kwa kurejea uhalisia ambao uko.
Hakuna kipimo cha uongo wala hakuna kipimo cha ukweli kwakuwa hizi ni dhana na si yabisi
Ukiwa muongo ni muongo tuu...na ukiwa mkweli ni mkweli tu..lakini si mambo yote utakuwa muongo na si mambo yote utakuwa mkweli .. Kila jambo moja linajitegemea uongo ama ukweli Wake! Hivyo usije ukajichanganya hapa
Kuhusu ukweli na uhalisia hapa ndio umepotea kabisa
Ukweli hubadilika lakini uhalisia hubaki vilevile.. Ukweli kwangu unaweza kuwa uongo kwako kama unavyoni brand kwenye hii mada..lakini je ndio uhalisia? Jibu ni moja tuu HAPANA