Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Uneanza kuharibu
 
Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?

Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
Ukweli mchungu ni kwamba, Kafara la Lindi halina uhusiano wowote na tatizo la kiuongozi kwenye taifa hili isipokuwa kuna kila dalili ni hilo kafara ndilo limefanya Watanzania wengi kuwa mazombi!!!

Afrika hii hakuna pahala palipowahi kuwa na viongozi bora lakini kwavile huko kwingine wananchi wao sio mazombi kama Watanzania, ndo maana unakuta wanafanya mabadiliko... iwe kwa shari au kwa heri!!

Yaani pamoja na yote yanayoendelea, bado unakuta hadi kwenye vyuo vikuu nako kuna ufuasi mkubwa tu wa CCM!! Kama sio uzombi tuite nini?!

Mfumo wa vyama vingi umeanza rasmi 1992! Kwa maana nyingine, waliozaliwa 1990 hawajui lolote kuhusu chama kushika hatamu!

And in fact, hata aliyezaliwa 1987, hawajui lolote kuhusu chama kushika hatamu, au mfumo wa chama kimoja!!

Lakini ni hao hao waliozaliwa from 1987 ndio wanaounda population kubwa zaidi Tanzania!!!

Hivi hata mtu aliyezaliwa 1986 atakuwa anafahamu nini kuhusu mfumo wa chama kimoja?!

Lakini pamoja na yote hayo, hebu kaa chini na tafakari!! Umekutana na vijana wangapi walio below 35 ambao wanaishabikia CCM?!

Umekutana na vijana wangapi walio below 35 wanaojitoa ufahamu na kushabikia flyovers zinazojengwa kwa kuona ndo tayari tunaelekea kuwa Dubai?!

Hayo yote hayatokani na uongozi bali yanatokana na uzombi wetu!!

Of course, ni uongozi ndio unatoa elimu ya ovyo na hatimae kuwafanya Watanzania kuwa mazombi, lakini akina Bibi Titi Mohamed sidhani kama waliwahi kuingia darasani lakini waliona Mkoloni hatufai!!!

Bara na pwani kote wakaupinga ukoloni, ingawaje majority hawakujua hata kuandika majina yao!!

I wish ningekuwa na ujasiri wa kuelezea historia ya baba yangu ambae viunga fulani vya Temeke alikuwa anaitwa jina la Mpambanaji Mmoja barani Afrika to the point, wakati nikiwa mdogo nikiulizwa jina langu, nilikuwa nai-include jina la huyo mpambanaji wa Afrika kwa sababu hilo jina lilikuwa maarufu sana kwa mzee hadi nikadhani ni jina lake halisi!!

Hakuitwa hilo jina kwa bahati mbaya!!

Nakuja kupata akili, Bi Mkubwa wangu ananiambia "baba ako mjanja mjanja tu yule, hata shule hakwenda"!! Wallah sikuamini, especially niliposikia hata kusoma na kuandika alifundishwa na mother!!!

Lakini pamoja na kutokwenda shule kwake, bado hakuwa zombi na ndo maana alipachikwa jina la huyi Mpigani Uhuru mmoja!! Hakuwa zombi kwa sababu Kafara la Lindi lilikuwa bado!!

And guess what... ingawaje alikulia TANU na CCM lakini yeye alikuwa ni miongoni mwa wana-CCM wa mwanzo kabisa kusambaza kadi za NCCR-Mageuzi, nadhani hata kabla vyama vya upinzani havijaruhusiwa rasmi!!

Hao ndo wale watu ambao walikua (growing) kabla ya Kafara la Lindi, kwahiyo kafara hilo lilishindwa kuwafanya kuwa Mazombi!!
 
Nakuja kupata akili, Bi Mkubwa wangu ananiambia "baba ako mjanja mjanja tu yule, hata shule hakwenda", wallah sikuamini, especially niliposikia hata kusoma na kuandika alifundishwa na mother!!![emoji23] [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
And guess what... ingawaje alikulia TANU na CCM lakini yeye alikuwa ni miongoni mwa wana-CCM wa mwanzo kabisa kusambaza kadi za NCCR-Mageuzi, nadhani hata kabla vyama vya upinzani havijaruhusiwa rasmi!!
Had guts...[emoji1534][emoji1534][emoji1534][emoji1534]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…