Hapa Kuna mtu ameamini mtu Hadi denial inamtesa ,hakuna kitu hapo.Hivyo akina kinenes na ikwetwa kwa kushirikiana na watu wa nje wakaamua kumuua..huku wakiwahusisha watu waliikuwa karibu yake..[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Thus awataki katiba mpya na uraia pacha hivi vinafungua code.Inasikitisha sana uchawi na matamko ni laana mbaya sana, na ninafikiri wazee wote wa matambiko karibia waishe bila kutoa codes za kuondoa Hilo tatizo
🤣🤣🤣 Mkuu mwambie huyo jirani yako aache kujisumbuaHivi huyo mkuu wa anga ni nani? Hapa kuna jirani yangu kila akisali anasema ANAMTEKA MKUU WA ANGA. Yaani leo anamteka, kesho anamteka tena wala hatusikii lini huyo mkuu wa anga amekimbia mateka
Unayajua mafundisho Yao yalivyokengeuka ni Yale madhehebu yanayokataa vitu na ili ujue sio wazuri ni SoMo la siku ingine .Kama ni Jehovah's Witness kubali tu hii ni ngumu kumeza.Mashahidi wa YEHOVA umewaonea
Unajichanganya hatujamzungumzia Lowasa tumeongelea mawaziri wakuu hivyo wachukue kiujumla usimuweke huyo Lowasa mbele.ULITAKA LOWASSA AWE RAIS KUPITIA CHADEMA? . AU.. SI MPAKA APITISHWE NA KAMATI KUU PAMOJA NA MKUTANO MKUU WA TAIFA CCM. KAMA HAJAPITISHWA JINA LAKE ATAWEZAJE KUGOMBEA
Nchi imepoteza mwelekeo.Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.
Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.
Tanzania nj taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk
Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana.. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana.. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi
Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?
Kafara la Bagamoyo ni la moto..na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"
Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?
Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani...sasa hapa ndio penye shida...ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa
Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda
Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake
Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi
Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao
Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana
Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega
Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?
Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
Ili iweje logic kwako ni ndogo sana hebu Anza kusoma upya uelewe tofauti.NIMEFUATILIA HUU UZI NIMEONA UNA MAPUNGUFU MENGI MNOO
HUYU dive na mshana jr ni mtu mmoja au wanafanya kazi zao pamoja. yaani ni mtu na mtu wake
Mwalimu Christopher Mwakasege (Arusha) na Omari Mnyeshani (Tanga) wanaweza kutusadia 0719 356206 na 0755 025821Hebu tuanze kuchangishana tupate hela sasa tukalinunue halafu tujenge hema kuu ya Mungu mkuu Muumba wetu tukusanye watu wa kiroho wanaosema na mungu wetu tukakemee hayo mashetani Taifa lipone!!!
Nakumbushia ukipata utulivu fungua codes hizi mkuuDive kwanza asante kwa madini yako..[emoji1545]nimeongeza kitu kwenye maarifa yangu ya kiroho..nimeshaingia kazini sina utulivu ngoja nikitulia nitafanya hivyo hakika kama itakuwa hajapatikana wa kutoa assist
Inabidi upate SoMo kuhusu maagano na athari zake mkuuViongozi wa dini wanaomba sana ina maana matambiko yana nguvu kuliko maombi ya viongozi wa dini?
Lakini mi mambo ya dini siyajui vizuri kabisa lakini wao wana sema Kwa Mungu hakuna linaloshindikana so kwa mantic hiyo maagano ya binadamu yana nguvu kuliko za Mungu?Inabidi upate SoMo kuhusu maagano na athari zake mkuu
Sasa unaaminije laana za kishetani bila kujua uwepo wa dini? Hakuna malumbano ya kidini nazan ww ndo mpofu wa kifikraa.Unachoongea upo kwenye upofu nisingependa mada iingie kwenye malumbano ya kidini.Nafunga mjadala kati yangu na wewe.
Waambie mkuu yaan kuna mizee humu imekalia uchawii uchawii mada zao za kichawi kutwa kucha..nchi inahitaj maendeleo ya kielimu mijitu inawaza uchawii..HAKUNA JIPYA. HILI LIMESHAANDIKWA SANA. TENA NA TENA.
Ngoja nikupe Darsa kidogo la lugha na maana.
"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike HATA nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini"
Mtu anapoaema umulike HATA maana yake ni nyongeza. Umulike ndani na hata nje ya mipaka yetu. Sasa wewe mwenyewe hapo juu ulicopy na kupaste maneno yaliyosemwa kama yalivyo. Ila chini umekuka ondoa neno HATA. umetukosea sisi wasomi.
Kabla hujaandika uwe unajua kuna watu mbalimbali humu ndani. Na uelewa umetofautiana.
Nikisema HATA mbwa anauma maana yake kuna mnyama mwingine yupo anauma. Tunataka kuwasha taa HATA za nje ziwashwe. Maana yake za ndani ni kawaida na kuna nyongeza ya taa za nje pia kuwashwa.
Habari za Makafara na ninii sijui ni uongo ule ule wa miaka yote. Tanzania inahitaji kuelimika ili iwe na mtizamo mpya zaidi.
Uongo mtupuMkuu wa anga ni aina za majini au fallen angels wanaozuia maombi yetu yasimfikie Mungu. Ni jini mkubwa na wenzie (wakuu wa anga). Kumbuka Lusifa ana wenzie 6 Malaika waasi na wao na wengine ni theluthi (moja ya tatu) ya Malaika na walipoasi walishushwa chini ni matrilioni ya viumbe vya kiroho vinavyotutesa.
Nitataja Hao 6 na baadae ila tukumbuke ulimwengu wa roho una madaraja 7 nayo ni physical realm (ulimwengu wa nyama) huu wa kibinadamu ,pili ni spiritual huko ndiko mizimu ,wachawi ,misukule,majini wa kati ,vibwengo n.k. yaani tofauti na WA nyama ,tatu ni Luciferian hawa ni majini wakubwa ambao wanaitawala dunia na watu wakubwa duniani wakipata ukuu wa spiritual realm wanaenda huku ili wawe wakuu kidunia kama vile tajiri wa dunia, kucontrol teknolojia na Sayansi za dunia,magonjwa na tiba kidunia,nne ni Fallen Angels realm yaani Lucifer na kaka zake 5 na dada Yao mmoja hawa ndiyo wameleta dini za uongo zote kuanzia uhindu, budha,tao,Shinto,Mashahidi wa Yehova na zingine pia wasioamini Mungunitaongelea siku ingine na maovu yote .Tano ni Angels realm, SITA ni Prophets and seers realm yaani manabii na waonaji Mungu huwaonyesha hawa vingi vinavyotokea .Daraja la 7 la Mungu ni la juu huko Mungu ana wenye uhai wanne na Wazee 24 yaani 12 wa zamani enzi za agano la kale na 12 wale wanafunzi wa Yesu ila Yuda Iskarioti hayumo.
Nikupe kufungu Cha Biblia ili uamini kuhusu mkuu wa anga ?Uongo mtupu
Nachukia sana mwenge. Natamani aje atokee mwamba anaemuamini Mungu kikweli kweli atengue hilo tambiko. People have been praying over and over lakini wapii. Kuna tambiko lingine lilifanyika Zanzibar, ni baya zaidi kuliko haya yanayofahamika sana. Mungu atusaidie tu la sivyo hatutatoka hapa.Hapana aliharibu alipolidharau kafara la kukimbiza moto...Ule moshi wa Ruangwa ndio ilikuwa alama ya onyo na karipio
Hatukatai ila usibishie masuala ya kiroho kwani ndiyo yanacontrol masuala ya mwilini .Waambie mkuu yaan kuna mizee humu imekalia uchawii uchawii mada zao za kichawi kutwa kucha..nchi inahitaj maendeleo ya kielimu mijitu inawaza uchawii..
Wapuuzi sana hawaa
Hebu funguka zaidi kuhusu tambiko la nchi la Zanzibar mkuuNachukia sana mwenge. Natamani aje atokee mwamba anaemuamini Mungu kikweli kweli atengue hilo tambiko. People have been praying over and over lakini wapii. Kuna tambiko lingine lilifanyika Zanzibar, ni baya zaidi kuliko haya yanayofahamika sana. Mungu atusaidie tu la sivyo hatutatoka hapa.