Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Hapa bila shaka unamaanisha ushirikina. Kama una maanisha Ushirikina kauli hii si ya kweli bali ina uongo mwingi. Yapo mataifa mengi yamesimama pasi na chembe ya hayo uliyoyasema,bali mengi yalianguka kutokana na hayo uliyo yasema. Mataifa yote ambayo yalikuwa chini ya mitume haua yalisimama pasi na chembe ya kafara wala matambiko bali wala kwa vyama vya mashetani,rejea ufalme wa nabii Suleyman,rejea taifa la Saudia kwa zama zetu hizi,sasa unaposema hivi sijui uliwaza nini ?
Kama hujui kitu tulia uulize upate ufahamu wa kukufumbua akili uyafahamu yaliyo ya kiroho
 
Hatukatai ila usibishie masuala ya kiroho kwani ndiyo yanacontrol masuala ya mwilini .

Madhara ya hayo MATAMBIKO ndiyo maana Kuna shida kwenye vitu vifuatavyo Kwa Tanzania.
1. Nchi kuwa na rasilimali nyingi kama Tanzanite,Mlima Kilimanjaro, maziwa makubwa kama Victoria Tanganyika ,bahari ,makaa ya mawe,mbuga za wanyama,ardhi kubwa yenye rutuba,madini ,misitu na mbao na vingine vingi mno lakini hakuna sera Wala mipango madhubuti haijaonekana na Taifa Lina miaka 60 sasa [emoji24][emoji24][emoji24]

2. Wananchi kutokuwazia maendeleo au kutokuwa na Utamaduni wa kuyaleta maendeleo ila kubakia wanawaza vitu vidogo vya ajabu kama udaku, ukipata nafasi kufanya ufisadi na ubadhirifu na kuwavuta ndugu na washkaji kwenye nafasi.

3. Mfumo wa elimu kubakia ule ule wa kikoloni wa kutengeneza White collar jobs badala ya kutoa elimu na maarifa ya Sayansi, ufundi na vitendo , biashara na ujasiriamali.Hivyo vijana wanaanza awali Hadi Form 6 hawana ujuzi wowote. Elimu Kwa wananchi wa kawaida ni duni na wale wachache walionacho watoto wao hawasomi kwenye shule hizi zisizo na ubora. Hii inaongeza pengo la walionacho na wasionacho na watawala kuendelea kuwatawala watawaliwa milele.

4. Sera za nchi kwenye maendeleo kuwa mbovu mfano kwenye uwekezaji Tanzania hali ya kufanya biashara ni Mbaya . Kuanzia kuwavuta wawekezaji,kushughulikiwa vizuri na Kwa haraka Kuna bureaucracy za ajabu huko TIC,TRA na vyombo vingine vyote. Kupata mitaji ni shida,kupata ardhi ni shida,kupata umeme ni shida,miundo mbinu na mawasiliano ni shida,masoko ni shida.Sera zinabadilika muda wowote hata ukikadiria kuwa utalipa kiasi Fulani Kwa miaka 10 atakuja kuibuka mtu au watu watabadilisha sera ,taratibu na sheria hawatabiriki.

5. Mazingira ya kupata Ajira Kwa sekta binafsi na serikali ni mabaya sana.Wahitimu wamejaa mitaani Hadi wanazeeka hawajui wafanye nini.Sera ni mbaya na zilizopo utekelezaji sio mzuri.

6. Nchi kujaa rushwa na ufisadi kwenye maeneo yote iwe mahakamani na Polisi,ofisi za umma ,mamlaka zote. Kama humjui mtu huwezi kutoboa hili sio Tanzania tu bali nchi nyingi za kiafrika.Shida hii inasababisha tupate majengo,barabara,huduma na bidhaa zilizo na ubora wa hali ya chini au hafifu kabisa.Tofauti na nchi zilizoendelea ambapo hata rushwa ikihusika viwango Bora huzingatiwa.

7. Kuminywa Kwa uhuru wa kuzungumza na kuwasiliana na uhuru wa vyombo vya habari.Yaani mambo ya kukosoana hakuna ukikosoa wewe mbaya unatakiwa usifie tu.Wasifiaji wanapewa tuzo na watu kuogopa kuongea wengine wanakuja JF kuandika nyuma ya keyboard [emoji3491].Hii inaleta impunity state.

8.Kilimo pamoja na kuitwa UTI wa mgongo wa nchi hakuna jitihada za makusudi kisera,kibajeti ili kikukue Imebakia siasa tu . Wananchi wengi wapo vijijini na ni wakulima na wafugaji ila wanalima kijima tu jembe la mkono na mvua za misimu tu.Kuwezeshwa hakupo ni siasa tupu ndiyo maana unaona bajeti za matumizi ya kawaida na chai ofisini ni kubwa kuliko kuwezesha miradi ya maendeleo.

Kiufupi ni hivyo sio tunaongelea uchawi kwenye dunia ya kisasa ila tunawekea mkazo kuwa haya masuala yana mzizi wake kabla ya uhuru na baada ya Uhuru.
Uliyoyataja hayana uhusiano wowote na matambiko.

Ninyi mnaajenda yenu binafsi.

Endeleeni!

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Nyie waongo watupu. Lindi sio mkoa masikini kuliko yote TZ. Yaani hata darasa la 7 anapata hilo swali. Wewe inaonekana ndio wale wale unafaulu kwa madesa.

sababu za mikoa mingi ya pwani kuwa masikini ndio utakuwa hujui kabisa
Wamesahau mikoa ya shinyanga,singida.
 
Nchi za kijamaa kwa ujumla wake naona zina shida. Mtu akiishakuwa kiongozi anaona wengine woote hamnazo. viongozi wote ni wakatili. Imagine mtu anawaambia mhamie Burundi

Imagine mtu hataki kusikiliza wananchi wake
mfumo huu wakijamaa ukiukosea mwazo ndo basi tena
 
Mkuu huyu binti anapatikana kwa njia zipi ?

Na je huwa anatolewa kafara au hubaki hai ?
Sifahamu mkuu. Huu uzi umenifanya nifanye jitihada za kumpata alietupa taarifa hizi. Nilikutana nae Morogoro ila ni mkazi wa shinyanga kama kumbukumbuku zangu ziko sawa. Nikimpata ntawajuza, by then alikuwa anaandaa kitabu kilichokiwa kinaelezea matambiko mengi ya karibu ukanda mzima wa Afrika Mashariki yakiwemo ya Buganda empire huko Uganda.
 
Back
Top Bottom