Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Mtazamo wangu ni Huu. Kukosa Kibali na Neema Ya Kristo Yesu Katika Karama na Kipawa. Maana Walio na Vyeo Hawakustahili Na Sisi Tusiojulikana Na Tunaostahili Hatuna Kibali Kwa Walimwengu.
Kuna point kubwa sana umeiongea mkuu...
 
Linajulikana kama nilivyojaribu kulielezea tena Hadi eneo la hicho kijiji ila as hatujashiriki hatujui undani sana.

Hilo eneo linatakiwa linunuliwe lote ili Hao wachawi wasiende kuongezea nguvu za kuinyonga nchi zaidi .Ni kipande kidogo kimeshanunuliwa inahitajika linunuliwe lote then pajengwe kitu kizuri kuua uchawi huo .Tatizo watu hawatoi pesa za kununua wengi washirikina na wanaishi Kwa ushetani.Ni high time tuokoe nchi yetu hata kujua hizi Siri ni mwanzo wa safari ndefu kwani zimefichwa mno hizi habari na wahusika wanakufa Kila siku.
Duuh!! Uko vizuri, nimekupenda ghafura!!
 
Tukaliondoe kafara la Lindi kwanza ...tutachukua nchi asubuhi na mapema[emoji1550][emoji1550][emoji1550][emoji1550]
Mkuu, kulikuwa na kafara moja Morogoro,palikuwa hapaishi ajali!!Mungu alinionyesha nikaombe mchana, kuzunguka kimvuli Cha huo mti, nilifanya hivyo. na ajali zimekoma hadi leo!! Ninatakakusema, hatujachelewa!! Mungu anatafuta watu wa kufanyanae kazi!! tuingie kwenye maombi, Mungu atatuonyesha namna ya kufanya!!
 
Uzi huu umenifanya nigundue huyu mshana jr ana account 7. Nitafungua uzi kuziweka hadharani
Ungekanusha achokisema, ningekuona unakili!! lakini kwajinsi unavyodili na mshana, nakuona Kama vile wewe ni mnufaika wa hayo makafara!!
 
nijibu haya maswali

1. nani alie tuumba?

2.dhumuni la alie tuumba ni nini?

3.je dhumuni la alie tuumba sisi ni tuteseke na hizi shida za duniani na maangaiko yake ambayo unaita ni mitihani/majaribio??

tuanzie hapo ukijibu nadhani tutafikia muafaka mimi na wewe.
Mkuu wafia dini watasema umepotoka kwa maswali haya
 
Mkuu, kulikuwa na kafara moja Morogoro,palikuwa hapaishi ajali!!Mungu alinionyesha nikaombe mchana, kuzunguka kimvuli Cha huo mti, nilifanya hivyo. na ajali zimekoma hadi leo!! Ninatakakusema, hatujachelewa!! Mungu anatafuta watu wa kufanyanae kazi!! tuingie kwenye maombi, Mungu atatuonyesha namna ya kufanya!!
Aaamen...! Aaamen ...! Aamen..![emoji1545][emoji1545]
 
kuhusu dhumuni la kutuumba hupo sahihi lakini pengine umepuyanga .

Maana aujasema bado chanzo cha binadamu kufukuzwa bustanini!!

ulichoeleza hapo ni kwamba MUNGU alikusudia kutuleta kwwnye ulmwengu wa mateso moja kwa moja.mkuu nakwambia bado unaitaji kujifunza nakuukubali ukweli sio kupinga tu.
mkuu utakuwa umekusudia ubishi au hilo kafara la lindi limekuathiri, hapo juu kwenye maswali yako umeuliza kuhusu mambo ya bustani?!..
 
Nchi aliikuta ina unafuu ameiacha hohe hahe, mambo ya katiba yake ya Imperial President (Rais mwenye hadhi ya kifalme kama Malkia wa Uingereza au kwingine) anacontroll Kila kitu na hakusimamia ibadilike,kuua upinzani kikabakia chama kimoja ,vita ya Kagera kumsupport Obote, kuwapigia kampeni akina Ben wakaja kumlet down

Wananchi tunabakia na akili za kushikiwa ukinyanyua mdomo mabwe pande inakukuhusu eti wasiojulikama.Matambiko haya yanatumaliza
So sad aisee
 
JIWE ALIUAWA NA ALIJUA ATAUAWA NDO MAANA ALIAWMA KUNASIKU MTANIKUMBUKA AU MANENO KAMA NAFANYA KAZI HII NGUMU ILI MTAWALA AJAE ATAWQLE Vizuri.
Jiwe alioewa mashart ya kuchawi akakataa..ndo maana aliamua kusali kila siku na kukimbilia chato katika kupambana.
Hivyo akina kinenes na ikwetwa kwa kushirikiana na watu wa nje wakaamua kumuua..huku wakiwahusisha watu waliikuwa karibu yake..
Typing errors nyingi Sana lkn ujumbe wako mzuri ungejaribu kuandika vizuri na kwa kirefu zaidi mkuu
 
Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.

Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.

Tanzania ni taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk

Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi

Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?

Kafara la Bagamoyo ni la moto na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho

"Baba, sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"

Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?

Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani. Sasa hapa ndio penye shida ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa

Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda

Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake

Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi

Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao

Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana

Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega

Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?

Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
...Mkuu, Ninaomba kusahihisha tj kidogo hii santensi. Inasema:


'Imulike HATA nje ya Mipaka yetu...'. .

Hiyo Hata tayari inaleta utofauti na jinsi ulivyoinukuu wewe Mkuu...
 
...Mkuu, Ninaomba kusahihisha tj kidogo hii santensi. Inasema:


'Imulike HATA nje ya Mipaka yetu...'. .

Hiyo Hata tayari inaleta utofauti na jinsi ulivyoinukuu wewe Mkuu...
[emoji1752][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
...Mkuu, Ninaomba kusahihisha tj kidogo hii santensi. Inasema:


'Imulike HATA nje ya Mipaka yetu...'. .

Hiyo Hata tayari inaleta utofauti na jinsi ulivyoinukuu wewe Mkuu...
[emoji1752][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Najifunza hapa
JamiiForums1278646264.jpg
 
Back
Top Bottom