Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Kuna tatizo mahali kwenye nafasi ya uongozi nchi hii. Je, kafara la Lindi linahusika?

Walichagua Tabora wachawi wake wakajitetea zindiko hilo litahusisha majini mengi na huko Tabora hakuna maji mengi.Tanga wakagoma wakasema mazindiko mengi makubwa yalifanyikia kwao ikabakia Lindi wapo karibu na bahari na madhara yake ni mkoa kuwa masikini kuliko na wananchi zindiko lilipofanyika kuwa na akili au uelewa mdogo.

Walizindika Kwa kutumia shimo kubwa linalozunguka na majini mengi mnooo na waliweka aina na species zote za mazao,mimea,wanyama, binadamu ,madini ,samaki bila kusahau yaani kila kitu.Hata mzee wao mchawi mkuu aliyeshiriki zindiko kuu la nchi la kwanza la Bagamoyo mzee Mfaume Golo Tumbo alifariki

Zindiko la kwanza la Bagamoyo waliohusika ni hawa
1.Forojo Ganze 'Master' huyu alikuwa le top hakuna mwingine ndiyo aliingia shimo la kuzimu kuongea na wakuu na baadae alikufa akiwa na namba 115 kiganjani.
2.Mfaume Golo Tumbo (wa Lindi)
3.Sheikh Yahya Hussein (alikuwa na miaka 29 muda huo mchawi huyu)
4.Shaibu Kalole Mtiga
5. Primus Mubanga Julius'alikuwa mtaalam mkuu wa kuelewa lugha za majini'
Chama cha kichawi kilimpelekesha JK Nyerere mno na mawaziri wakuu walipigwa pini kuwa Marais au umeona Waziri mkuu Alishinda urais?!
Hapo sasa ndiyo napata picha kwanini Edward Moringe Sokoine yalimkuta yaliyompata.
 
Watanzania hatutakaa tuendelee kama kila wakati tutakuwa tunawaza makafara. Nini faida ya kusoma kama watu wenye ufahamu kama wewe mnaendelea kuwazia mambo ya kijima?
Hakuna taifa lolote duniani lililosimama imara bila nguvu za mkuu wa anga! Kuanzia matambiko mpaka makafara na vyama vya kishetani.

Hivi vyote vimejenga madhabahu zao kwenye kila ardhi ya kila taifa. Wananchi wake wana dini na imani zao lakini mataifa yamesimikwa kwenye hizi madhabahu viapo na makafara.

Tanzania ni taifa kama mataifa mengine duniani, nayo ina makafara na madhabahu zake za kuifanya nchi itawalike iheshimike na iwe na 'stability' kwenye kila nyanja kuanzia kiuchumi, kijamii, kimaono mpaka kiulinzi nk

Kuna makafara ya kuilinda Tanzania yanatajwatajwa sana. Kafara la Bagamoyo na kafara la Lindi! Kafara la Bagamoyo linaelezewa kwa ufasaha na wahusika wake wanajulikana. Shida ipo kwenye usiri mkubwa unaotawala kwenye kafara la Lindi

Hili limebaki kuwa fumbo na tetesi isiyothibitishwa popote. Wanaolijua ni wachache na hulisimulia kwa tahadhari kubwa sana! Lina nini ndani yake hili?

Kafara la Bagamoyo ni la moto na kiongozi wake ni Mzee mchawi marehemu Forojo Ganze na hiki ndicho alikisema kabla ya kukata roho

"Baba, sisi tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau"

Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl. Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU". Ina maana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa?

Hli kafara la Bagamoyo tunaweza kuliita kafara la mambo ya nje na lile la Lindi tunaweza kuliita la mambo ya ndani. Sasa hapa ndio penye shida ni kafara la mambo ya ndani na limebaki ndani na kuwa siri kubwa

Mwalimu Nyerere Mchonga meno kwa hakika anayajua vema makafara yote mawili na miiko yake na pengine ndio maana katika tawala zote tangu uhuru ni utawala wake pekee ndio ukifanikiwa kwa kiwango cha juu kwenye
Kuweka misingi sahihi ya uongozi, uwajibikaji na uzalendo
Kuweka misingi sahihi kijamii, kisiasa na kiulinzi
Kuweka misingi sahihi ya kimtazamo na kimaono
Mipango endelevu na dira sahihi tangu tulipoanzia, tulipofikia na tunakoenda

Baada ya hapo waliofuatia wote kila mtu alikuja na MAGAZIJUTO YAKE na sarakasi zake
Baada ya hapo kila aliyeingia alianza vizuri lakini hakuchelewa kuharibu. Kama si kipindi cha kwanza basi cha pili cha uongozi wake

Baada ya hapo waliofuatia wote waliingia kwa upole na unyenyekevu lakini mara wakageuka wajivuni, wababe, na baadhi yao dharau kujikweza na kujimwambafai kwingi...bila kusahau vitisho na ugiligili mwingine mwingi

Baada ya hapo wengine wote watakanguliza maslahi binafsi, ya ndugu zao, jamaa zao na watu wote waliokuwa na maslahi nao

Mambo yanazidi kuharibika na pengine hawaoni wametiwa upofu.. Huu ugiligili sasa ni mpaka kwa viongozi wanaowateua kuwasaidia majukumu ya kiutendaji. Sasa hivi kiongozi akipewa kipaza sauti aongee mbele ya makamera asipotoa boko basi atatoa kituko cha karne ama kuongea yasiyowezekana

Matamko ni mengi mno
Maelekezo ni mengi mno
Makatazo ni mengi mno
Maonyo ni mengi mno
Yani haya ni mengi mno mpaka yanapishana barabarani na kupigana vibega

Kuna tatizo kubwa la kiuongozi na hili lina mizizi mirefu tangu ang'atuke mwalimu. Je, kwa mtazamo wa kiroho ni lile kafara la Lindi?

Wakati utaongea. Hebu tuupe muda!
 
Watanzania hatutakaa tuendelee kama kila wakati tutakuwa tunawaza makafara. Nini faida ya kusoma kama watu wenye ufahamu kama wewe mnaendelea kuwazia mambo ya kijima?
Ulimwengu wa roho ndio engine ya dunia.. Na huu ndio umebeba hatima na mustakabali wetu wote.. Ni ulimwengu beyond normal thinking ya kibinadamu
 
Dih
Walichagua Tabora wachawi wake wakajitetea zindiko hilo litahusisha majini mengi na huko Tabora hakuna maji mengi.Tanga wakagoma wakasema mazindiko mengi makubwa yalifanyikia kwao ikabakia Lindi wapo karibu na bahari na madhara yake ni mkoa kuwa masikini kuliko na wananchi zindiko lilipofanyika kuwa na akili au uelewa mdogo.

Walizindika Kwa kutumia shimo kubwa linalozunguka na majini mengi mnooo na waliweka aina na species zote za mazao,mimea,wanyama, binadamu ,madini ,samaki bila kusahau yaani kila kitu.Hata mzee wao mchawi mkuu aliyeshiriki zindiko kuu la nchi la kwanza la Bagamoyo mzee Mfaume Golo Tumbo alifariki

Zindiko la kwanza la Bagamoyo waliohusika ni hawa
1.Forojo Ganze 'Master' huyu alikuwa le top hakuna mwingine ndiyo aliingia shimo la kuzimu kuongea na wakuu na baadae alikufa akiwa na namba 115 kiganjani.
2.Mfaume Golo Tumbo (wa Lindi)
3.Sheikh Yahya Hussein (alikuwa na miaka 29 muda huo mchawi huyu)
4.Shaibu Kalole Mtiga
5. Primus Mubanga Julius'alikuwa mtaalam mkuu wa kuelewa lugha za majini'
Chama cha kichawi kilimpelekesha JK Nyerere mno na mawaziri wakuu walipigwa pini kuwa Marais au umeona Waziri mkuu Alishinda urais?!
Duh!!
 
Kwenu ndipo masikini kuliko pote nchini na ndipo penye watu wenye low IQ kuliko wote nchini japo kuna utajiri wa raslimali tele,chanzo ni kafara la kuitambikia nchi 1992.
Kuna jingine la 1992 Tena!!!????
 
Linajulikana kama nilivyojaribu kulielezea tena Hadi eneo la hicho kijiji ila as hatujashiriki hatujui undani sana.

Hilo eneo linatakiwa linunuliwe lote ili Hao wachawi wasiende kuongezea nguvu za kuinyonga nchi zaidi .Ni kipande kidogo kimeshanunuliwa inahitajika linunuliwe lote then pajengwe kitu kizuri kuua uchawi huo .Tatizo watu hawatoi pesa za kununua wengi washirikina na wanaishi Kwa ushetani.Ni high time tuokoe nchi yetu hata kujua hizi Siri ni mwanzo wa safari ndefu kwani zimefichwa mno hizi habari na wahusika wanakufa Kila siku.
Ni kijiji gani hicho?
 
Lengo lilikuwa nchi itawalike kirahisi, uongo wa shetani eti nchi ingestawi
ila kwa upande fulani, wamezuia machafuko, yaani hali ingekuwa shwari bila hayo matambiko hii Tz ilivyojawa na wanaojifanya much knowers kingenuka kila siku. ila watu wamepozwa mno sometimes najiulizaga hivi viongozi wa kijeshi hawajawahi kuwaza kuishika nchi hata siku 1, kweliiiiiii!
 
Nyie waongo watupu. Lindi sio mkoa masikini kuliko yote TZ. Yaani hata darasa la 7 anapata hilo swali. Wewe inaonekana ndio wale wale unafaulu kwa madesa.

sababu za mikoa mingi ya pwani kuwa masikini ndio utakuwa hujui kabisa
Kwa manenoo ni mkoa tajiri kuliko mkoa wowote nchi hii ila kwa muonekano Ni MASKINI KULIKO!!!
 
Azazel wakati anatupwa duniani kwa kiburi chake kabla hajatua duniani alitamka haya; NAKWENDA KUKALIA AMALI ZOTE ZA DUNIA MADINI YOTE MALI ZOTE NA FAHARI ZOTE ZA DUNIA . haya mamali mi huwa nayaangalia tu lakini ili uzipate kirahisi onana na aliyezikalia kwa ujira wa damu ya nduguyo ili utajirike kupindukia na uwastaajabishe binadamu wenzio,
Damu ya nduguyo[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hili jambo lipo spiritual na linaathiri kuanzia ardhi,mimea,wanyama, resources aina zote Hadi viongozi.

Angàlia nchi zingine wanakotokea hadi nchi zao zinapofika Rwanda,South Korea,Angola, Singapore,Japan Kwa uchache na sio kwamba wao wanamcha Mungu wa Kweli

Jambo likifanyika rohoni linamaliza kabisa huku ulimwengu mwili.

Tanzania mkombozi wa Afrika eti ni ovyo , masikini,uongozi usio na dira. Eti Nyerere aliingiza nchi vita vya Kagera na ujamaa ambao China ,Urusi ,Ujerumani Mashariki na wengine wamebadilika vizuri.

Eti akaja Mwinyi akauza Loliondo na madudu mengine.KATABALO yakamkuta.......Akaja Mkapa akaleta Network Solutions ya SA ,akauza NBC kiajabu na program yake ya kuiondoa serikali kwenye biashara,akaiba mno mfano Radar,Meremeta na ishu za akina. Daudi Balali.Akanunua hotel South Afrika ANBEN mgodi wa makaa ya mawe.Sethy Chachage akaandika MAKUWADI WA SOKO HURIA ..........

Akaja JK naye akaiba mno Tegeta ESCROW account,Kagoda Agriculture,Twin Towers za BOT,RICHMOND na zingine ambazo nikipata muda nitakumbushia.Pia mihadarati ikashamiri mno.Kutokuwajibika ,Rais kuwa VAsco Da Gama anasafiri duniani kuliko kukaa nchini tena na delegates zinazofilisi nchi kwa gharama kupitia kodi za wavuja jasho. Kina KUBENEA,DR. ULIMBOKA na Mhariri wa TANZANIA DAIMA .........

Tukumbuke Rais ni Sponsor anapokea briefings zote hakuna kitu kibaya kinafanyika hajapewa intelli sema yeye akaamua tu kuwa anajinufaisha na ukoo wake na washkaji na tabaka la watawala kwenye chama chake.Ukielewa haya utajua jinsi laana zenyewe zilivyo

Akaja jiwe yeye akaua sekta binafsi,akazuia Ajira majamaa wamerundikana mitaani kwani wakiomba kuajiri haruhusu na akruhusu ni wawili watatu tu Hadi wanajilamu kusoma na kuzuia kupanda madaraja makazini na mishahara,tenda zote zikabakia kwenye makampuni ya serikali,akaua Precision Air,Fast Jet kutengeneza monopoly ya Air Tanzania wakati ushindani huboresha biashara.Akateua watu hao daah,akajikompramandi Kwa PK Mtu mrefu .Akazuia mikutano na Harakati za vyama vya siasa , wananchi hawajui hata nchi inaenda vipi na wapo kwenye umasikini na kukaa gizani kifikra Hadi kwenye nyumba zao.Mahoteli yakafa,makampuni ya utalii na ulinzi binafsi yakajifia


Akaweka ndugu jamaa na marafiki Hadi mabibi ,cabal yake ikafurahia mno kuliko Taifa.Akaanza kucrack down vyombo vya habari,AZISE,hapa kulitungwa sheria za ajabu kwa dharura za vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii kama JF,vyama vya siasa.
Akina CAG wakaondolewa,sheria za NSSF na mashirika mengine zikabadlishwa na kutengeneza monopoly,bodi ya mikopo ikaweka madaraja mengi,

Akajaza mitambo na Ajira za vyombo vya Dola kujilinda sio PCCCB,Kitengo ,na kwingine.Akaenda kwenye chama akabadili katiba.Akawabana watoa mawazo na maoni mbadala,ikawa ni usifiaji tu hatukui Kwa kusifiwa tu yaani his ego was so BIIG.Akaanza kuwanunua wapinzani na kuwapa nafasi za juu serikalini

Wakaanza kubeep kuw atawale milele akawa kama anakataa kumbe.Ukaja uchaguzi mkuu wakaurig mno wakaweka bunge lisilo na mawazo mbadala 'Wapinzani wametucherewesha sana ' Walizima Hadi mitandao.Eti Kuna wabunge19 viti maalum ambao wengine walishinda wakaombwa waachie tu watapitishwa mlango wa nyuma.

Lengo lililojificha ilikuwa kutawala maisha ila bahati mbaya mambo yakaenda sio.Yaani nchi inapitia dhoruba zisizoisha

Sasa wananchi waliosoma na kuandaliwa tangu uhuru leo ni kama mayatima,humjui mtu hupati stahiki yako,Wala Ajira ni mwendo wa connection,ukifungua biashara TRA na wengineo wanakumaliza mapema ni tozo na sheria za ajabu.

Wawekezaji wanajuta,wapya hawathubutu kusogeza pua,hofu imejaa

Walioumia ni Azory Gwanda,Roma Mkatoliki,Abdul Nondo,Ben Rabiu Saa nane, Tundu Lisu,Freeman Mbowe,Peter Msigwa,Godbless Lema,.......

Nchi Haina dira kuu, malengo ,sera mbovu zinabadilika akiingia mtawala mpya yaani sio sera zinaongoza ni utashi w mtu.Rushwa zimetawala,hakuna haki,ubabe yaani laana za mazindiko kutokea rohoni kuja kuku physical realm

HII NCHI INATAKIWA IPONE KWANI MBELE NI GIZA ZAIDI HAYA MATAMBIKO DUUH
Hapa ndipo nimekuelewa zaidi.
 
Mkuu, hapa kuna Tunu za Taifa. Ni vema histotia ya Taifa ibaki kama ilivyo, na lisipunguzwe neno katika sentesi kwa nia ya kuleta mkanganyo.

Kabla ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Baba wa Taifa Hayati Mwl.J K.N. pamoja na mambo mengine, alifanya mambo mawili ya msingi., (1)aliwasilisha UN ramani ya Tanganyika. Ilipokelewa na hakuna aliyeihoji. Hata baadaye, chokochoko ya ziwa Nyasa ni la Malawi., mlima Kilimanjaro na North Mara (Tarime&Rorya) ni sehemu ya Kenya., mpaka wa Burundi na Tanganyika upo Kahama, hivyo Kigoma na baadhi ya maeneo ya Tabora na Katavi ni sehemu ya Burundi zilikosa mashiko.
(2) alihutubia kikao cha UN na kueleza, nanukuu "SISI TUNATAKA KUWASHA MWENGE, NA KUUWEKA JUU YA MLIMA KILIMANJARO. UMULIKE HATA NJE YA MIPAKA YETU, ULETE TUMAINI, PALE AMBAKO HAKUNA MATUMAINI, UPENDO MAHALI AMBAKO PANA CHUKI, NA HESHIMA AMBAKO PAMEJAA DHARAU. Na huu ulikuwa msingi mkuu wa Sera ya nje ya Tanganyika.
Baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Baba wa Taifa aliamini na aliwaeleza wananchi kuwa Tanganyika haiwezi kuwa huru, kama nchi nyingine zitakuwa chini ya ukoloni na utawala wa mabavu. Na ndio ukawa mwanzo wa kuunga mkono jitihada za ukombozi kusini mwa Afrika, Sahara Magharibi, Biafra na hata Palestina.

Ufafanuzi zaidi utaupata endapo utatafuta, nini maana ya:-
~Ramani
~Bendera
~Ngao/Nembo ya Taifa @ bi & bw
~Twiga
~Mwenge wa Uhuru
Ikiongezeka na Lugha ya Kiswahili, Umoja na Amani

Ni maoni yangu,
Aiseee haya watu mnayapatia wapi?
Mbona mna madini makubwa Sana?
 
Kuna vitu nakamilisha niliandike kwa kina... Kuna vitu umenipatia vimenisaidia sana[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Nyerere aliwaficha watz Siri nyingi Sana kupitia media control,thus aliwafanya watz maiti Ili awatawale.
Baada ya upepo wa mabadiliko ya fikra kulinda heshima aliona bora aachie.
Sasa viongozi wa ccm wanaongoza kizazi cha sasa kwa fikra za miaka ya 70,thus awatofaulu.
 
Nyerere aliwaficha watz Siri nyingi Sana kupitia media control,thus aliwafanya watz maiti Ili awatawale.
Baada ya upepo wa mabadiliko ya fikra kulinda heshima aliona bora aachie.
Sasa viongozi wa ccm wanaongoza kizazi cha sasa kwa fikra za miaka ya 70,thus awatofaulu.
The Sun [emoji295] is going down[emoji116] to Chiolu and soon it will be sunset ...!!!!
 
Back
Top Bottom