Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Jesus and Muhammad
1000018468.jpg
 
Acha kujidanganya mkuu, Yesu hawez kurudi.

Tena Kwa wayahudi tulionao sahivi, watampiga Yesu makombora mpk achakae.

Bora kina Pilato walimhurumia wakamgonga misumari nchi 6 mikonini na miguuni Ila wakauacha mwili wake angalau unatambulika ukiutizama

Ila Kina Netanyau hawacheki na kima, wataulipua,kuuchakaza na kuufukia na vifusi vya Gaza.
Wewe Mbona unaandika vitu kuashiria kuwa una laana?

Unawezaje kumzungumzia MUNGU namna ulivyofanya?
 
Alisema hakuna ajuaye siku Wala saa,

Hapo hapo akasema majira ya kuja kwake Mathayo 24.

Ndipo ujue, siku wala saa havijulikani, ila jiulize vipi kuhusu mwezi au mwaka pia havijulikani?

Ujio na uanzaji KAZI wa 666 duniani ni Ishara ya kunyakuliwa Kanisa, Kisha baada ya miaka elfu, mwisho wa Dunia kuchomwa unawadia.

Usiombe ukaachwa duniani Unyakuo utapofanyika,

Usiombe kuishi duniani mtawala akiwa shetani na Malaika waliofungwa watapoachiwa.

Time is now, the choice is yours.
Wakiachwa itabidi wajitetee kwa kukubali kuuwawa ili kumfia kristo, nawaza hayo mateso yake ni hatari.
 
Netanyahu ni thousand times ya pilato. Jamaa hajui misumari, ni makombora mwamwi
 
Kuna yule yesu fake anayeandaliwa huyo inawezekana kabisa na huyo ndiye anaandaliwa.

Ila yule mwenyewe kabisa aah bado kuna ishara hazijakaa sawa.

Hapo ulipo wewe bado mnapendana na ndugu zako hadi mwisho wa mwaka unaenda kwenu na zawadi, ika dalili za kurudi kwa Jesus upendo utapoa hutokwenda kwenu.

Haya yanayoendelea ni dalili theruthi ya makubwa sana yajayo ambayo hutojua ukimbilie wapi.
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Kuna ka UKWELI fulani kuhusu jambo hili.......kuna watu kadhaa nikiwemo mimi nina ahadi ya kumuona masihi Yesu,,,,,yaani nina uhakika sitakufa bali nitamshuhudia akirudi duniani...na mie ni mmoja wa wachache hapa Duniani mwenye uhakika wa kwenda naye MBINGUNI,,hiiii ni special ahadi wala si masihara.......na yanayoendelea wala hayanishtui manake nimeonyeshwa BEFORE....ila kwa siku na saa..I DONT KNOW
 
Wewe Mbona unaandika vitu kuashiria kuwa una laana?

Unawezaje kumzungumzia MUNGU namna ulivyofanya?
Huyo haamini katika KRISTO. Ni sawa na wewe umzungumzie ng'ombe wa wahindi kuwa anafaa kwa kitoweo. Watakuona kama unavyomuona huyu ilihali wewe hutokuwa na wasiwasi wowote maana huamini kama huyo ng'ombe ni MUNGU.
 
Kivipi wakati alisema kizazi hiki hakitapita ?
Kizazi hiki ni kipi? Kila kizazi ni kizazi hiki tangu maandishi hayo yameandikwa. Vitukuu vyako vitasoma kizazi hiki, vilembwe vyako vitasoma kizazi hiki kama ambavyo mababu wa mababu zako walisoma kizazi hiki.
 
Pengine wewe bado mtoto mdogo wa 2000, ila sie wazee wako tulishaahidiwa na manabii wa kizazi kipya kuwa mwisho wa dunia ulikuwa mwaka 1978, wakachemka tena na kusema mwaka 1982 mara 1999......cha kushangaza mpaka leo bado tunapeta tu na kugawana dhambi according to dini za kuletewa.
Mwaka 82 kuna jamaa aliuza kila kitu...akawa analewa ...akisema PONDA MALI KUFA KWAJA>>>>>>>>>> akawa lofa na kufa hakufa na mwisho wa dunia hakuna.....🙂🙂🙂🙂
 
Mkuu tatizo sio tetesi tatizo
Tunalinganisha kile kilichoandikwa na kinachotokea yaani ni kile kilichotabiriwa yaani matukio ndio kinatokea leo.
Uki connect dots something utang'amua.
Wote waliokuqa wanasema dunia inaisha tangu enzi walikuwa wanalinganisha na maandiko na bado haikuisha. Achana na tetesi hizo chapa kazi
 
Wakiachwa itabidi wajitetee kwa kukubali kuuwawa ili kumfia kristo, nawaza hayo mateso yake ni hatari.
Yakitokea hayo, Mungu ameahidi ktk neno kuwa, atazifupisha siku hizo za mateso ya watu wake .
 
Wanamsemea?
Aliwaambia hakuna ajuaye siku wala saa

hatutojua siku wala saa, ila majira na nyakati tutazijua. Neno la Mungu liliweka wazi kwa habari ya majira ya majilio.

1 Wathesalonike 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
² Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
³ Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
⁴ Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
⁵ Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
⁶ Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.


YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
Back
Top Bottom