Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Huyo haamini katika KRISTO. Ni sawa na wewe umzungumzie ng'ombe wa wahindi kuwa anafaa kwa kitoweo. Watakuona kama unavyomuona huyu ilihali wewe hutokuwa na wasiwasi wowote maana huamini kama huyo ng'ombe ni MUNGU.
Mkuu siwezi kukuta Uzi wanaoabudu Ng'ombe nikauvamia na kuanza kuandika mambo ya ajabu kama aloandika.

Anapungukiwa Nini kutokuandika ama kueleza maoni yake hata ikiwa Yako tofauti Kwa ustaarabu?

Anajua kuwa hao kina Netanyahu atakaporudi mara ya pili watafunguliwa macho na watamwamini?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hizo taarifa zimekuwepo karne zote.

2 Petro 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁷ Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
⁸ Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
⁹ Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
¹⁰ Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
¹¹ Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
¹² mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
 
Alisema hakuna ajuaye siku Wala saa,

Hapo hapo akasema majira ya kuja kwake Mathayo 24.

Ndipo ujue, siku wala saa havijulikani, ila jiulize vipi kuhusu mwezi au mwaka pia havijulikani?

Ujio na uanzaji KAZI wa 666 duniani ni Ishara ya kunyakuliwa Kanisa, Kisha baada ya miaka elfu, mwisho wa Dunia kuchomwa unawadia.

Usiombe ukaachwa duniani Unyakuo utapofanyika,

Usiombe kuishi duniani mtawala akiwa shetani na Malaika waliofungwa watapoachiwa.

Time is now, the choice is yours.
Taja huo mwezi na mwaka
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Nina uhakika hata mwaka 300 AD wapo ambao walisema mwisho wa dunia unakaribia kumbe kilichokuwa ni mwisho wa dunia yao wenyewe!
 
Pia tujue hili,

Unyakuo utaanza kwanza Kisha maisha ya taabu na dhiki kuu yataanza rasmi duniani WATAKATIFU wakiwa mapumzikoni.

Baada ya miaka elfu , Yesu atakuja kuwachukua na kufufuka waliowake washindao mateso ya dhiki kuu.

Baada ya hapo ndipo ataihukumu Dunia na Ulimwengu kutupwa Ziwa la moto jehanum baada ya kuhukumu.
Uongo
 
Mkuu siwezi kukuta Uzi wanaoabudu Ng'ombe nikauvamia na kuanza kuandika mambo ya ajabu kama aloandika.
Ni heshima kuheshimu imani za wengine
Anapungukiwa Nini kutokuandika ama kueleza maoni yake hata ikiwa Yako tofauti Kwa ustaarabu?
Hatopungukiwa, ni ameamua tu kutokuheshimu maana haamini kama YESU anaweza mfanya chochote. Anaamini waamini ndo watamjibu si YESU maana inawezekana haamini kama hata yupo achilia mbali kurudi..
Anajua kuwa hao kina Netanyahu atakaporudi mara ya pili watafunguliwa macho na watamwamini?
Hajui wala haamini.
 
Kuna ka UKWELI fulani kuhusu jambo hili.......kuna watu kadhaa nikiwemo mimi nina ahadi ya kumuona masihi Yesu,,,,,yaani nina uhakika sitakufa bali nitamshuhudia akirudi duniani...na mie ni mmoja wa wachache hapa Duniani mwenye uhakika wa kwenda naye MBINGUNI,,hiiii ni special ahadi wala si masihara.......na yanayoendelea wala hayanishtui manake nimeonyeshwa BEFORE....ila kwa siku na saa..I DONT KNOW
Mkuu unahisi kabsaa 2027 hatutoboi hii dunia.
Mana lazima.pia uangalie na age yako.
 
Hivi Mungu mwenye huruma ni wa kumtupa mwanadamu kwenye ziwa la moto kweli?nahisi baadhi ya watu mnatafsiri biblia vibaya.

Mungu ni wa rehema, ndio maana akamleta Mwanawe Yesu Kristo afe msalabani kwa ajili yetu. Ndio maana ameachilia neema ya wokovu kupitia Yesu Kristo ili kila amwaminiye ahesabiwe haki. Apate uzima wa milele. Usipopokea wokovu ulio katika Kristo Yesu, kuangamia na shetani katika ziwa la moto kuko palepale!
 
Kuna taarifa za kushangaza huko USA inasemekana mwisho wa Dunia (doomsday) ni karibu mno na kizazi hiki kitashuhudia Yesu anarudi stay tuned kwa ushahidi.
Kama atarudi akiwa mzungu tutamkataa wasituone sisi ni wajinga. Kwanini Yesu awe mzungu (rangi nyeupe) alafu shetani ndo awe mtu mweusi (rangi nyeusi)
 
Aisee zama za kuingia ghetto zilishanipita. Naingia kwenye nyumba au hotel...sio lodge.
wahaya kawaida yenu kujinasibu..😃
haya tuambie ukienda hotelini unakunywaga nini..?
 
2 Petro 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁷ Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
⁸ Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.
⁹ Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
¹⁰ Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
¹¹ Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
¹² mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Mkuu ila naamini unyakuo itakuwa kimya wala haitajulikana ila sasa baada ya kukaa huko mbinguni na kisha kurudi ndio watamwona au mimi nimetafsir vibaya.
 
Back
Top Bottom