Kuna tetesi Dunia inafikia ukomo, Masiha anarudi?

Mkuu ila naamini unyakuo itakuwa kimya wala haitajulikana ila sasa baada ya kukaa huko mbinguni na kisha kurudi ndio watamwona au mimi nimetafsir vibaya.

1 Wathesalonike 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹³ Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
¹⁴ Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
¹⁵ Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
¹⁶ Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
¹⁷ Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
 
Mkuu ila naamini unyakuo itakuwa kimya wala haitajulikana ila sasa baada ya kukaa huko mbinguni na kisha kurudi ndio watamwona au mimi nimetafsir vibaya.

1 Wakorintho 15 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵¹ Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
⁵² kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
⁵³ Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
 
Hujakosea mkuu.

Pope Francis Urges Jews to "Kill Jesus Again"if He Returns to Earth.

Pope Francis left onlookers stunned at an Italian prison when he made a statement that sent shock waves through the Catholic Church.
Warumi Kama warumi.
 
Kweli,mwamba Jesuit nilimwona juzi mawinguni ndio anakuja huku duniani
 
Y2K nilishangaa wazungu walisema ni mwisho wa Dunia halafu cha ajabu walikuwa wanapigana vikumbo wakinunua mamia ya toilet paper na maji sijui walikuwa wanaenda nayo wapi
Hizo ndio akili za wazungu msizozijua
Y2k kirefu chake nini
 
1 Wathesalonike 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯

¹⁷ Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Hawa waliosema "sisi tulio hai" bado wapo hai?
 
Kwani Netanyahu anabiga wayahudi we zake? 😀
 
Mkuu umesahau,milima pia itakimbia kujisitiri na hasira zake,dunia itakunjwa kama karatasi
 
Soma Biblia vizuri kaka dhiki itawakuta wema na wabaya wote hapa duniani ndiyo maana Yesu akasema kama hizo siku zisipofupishwa hakuna mtu ambaye ataokoka
 
Wanamsemea?
Aliwaambia hakuna ajuaye siku wala saa

1 Wathesalonike 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.
² Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
³ Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
⁴ Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
⁵ Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
⁶ Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…