katika hali ya maisha magumu kama haya, wakishusha rungu tutakuwa kama malawi. tulifanya makosa makubwa sana kwenye uchaguzi uliopita, na hii inatugarimu live, hata kama watu wanajifariji lakini iko wazi, watu tuliowaweka madarakani tuliingia mkenge na tutajuta hadi 2020. tuangalie kama 2020 tutafanya makosa tena kama haya. ni sawa na kumpa intern kazi ya mteja wako wa miaka mingi. itaharibika tu. watu hawana uzoefu na uongozi hasa wa kimataifa, hawana uzoefu na uchumi, hawana uwezo wowote ni sawa tu na wametoka bush juzu, tukawakabidhi madaraka. nchi imesambaratika, hata pesa za kuendesha ofisi za serikali hamna, waulizeni wafanyakazi wa uma wanafanyaje kazi maofisini huko, wanaogopa tu kulalamika lakini hali ni mbaya kupita maelezo. tulitegemea hali itakuwa mbaya kwa mafisadi na wafanyabiashara wakwepa kodi, lakini hali ni mbaya zaidi ofisi za serikali, magari hayafanyi kazi hamna mafuta, hamna hela, afu mtu anakuja kusema anajenga uchumi? wanaeleza hata maana ya uchumi au walikuwa wanausikia tu. watu walipata madaraka kwa bahati nasibu ya kujaribisha na wanakotupeleka hakueleweki. Mungu aingilie kati hawa watu hawatufai maishani.