Tetesi: Kuna tetesi kwamba Marekani inapanga kutangaza vikwazo kwa Serikali ya Tanzania

Tetesi: Kuna tetesi kwamba Marekani inapanga kutangaza vikwazo kwa Serikali ya Tanzania

Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...
Mbona wewe unafurahia wengine wanapoonewa,mfano Lema ,na wengine wengi.
 
na underson ndambo.

Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.

Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC, pamoja na kuzishawishi nchi zengine. Serikali ya Tanzania ipo hatarini kukumbwa na janga la njaa, ikiendelea kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki itendeke kabla ya Febr 2017.

Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguz mkuu wa Zanzibar uliofanyika 25th Oct 2015.
Unaiabudu Marekani ?!
 
Uzushi tu huu, Yaan vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa vishindwe kupata hizi tetesi wewe ambaye upo Tanzania ndo uipate?

Hakuna kitu kama hicho, na Obama hawezi kufanya kitu kama hicho, kama TUME ya uchaguzi ingelikuwa imemtangaza rasmi Maalim Seif kama Rais afu CCM ikashinikiza matokeo yafutwe hapo kweli vikwazo vingewekwa, lakini kwa namna ilivyotokea ni ngumu sana hatua kama hizo kuchukuliwa, labda useme kuwa, MAREKANI ilazimishe mazungumzo kati ya CUF na Serikali yafanyike lakini si vikwazo.
Mtoa mada Ni mnafiki wazi kabisa !
 
Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...
Mungu atuepushe vikwazo visitikoe, maana Dk Sheni hatadhurika na vikwazo hivyo shida ipo kwangu mimi nawewe.
 
Mkuu UN kuna vitengo sita ambavyo ni
1 General Assembly. President.
2 Security Council. Members.
3 Economic and Social Council.
4 Secretariat. Secretary-General. Deputy-Secretary General. Under-Secretary-General.
5 International Court of Justice. statute.
6 Trusteeship Council.

Na wenye kuweka vikwazo ni mkutano wa General Assembly ambao ni wanachama wote si Security Council. Members. ambao ni wababe wa dunia
Hizo ni story tu uhalisia unaujua, vita vya irak baraza la usalama ambalo ndilo lenye nguvu lilikataa kuivamia irak Marekani ikaamua yenyewe, Bush akasema, "if you are not with us you are with them" nani alikohoa.
 
Hizo tetesi umezitoa wapi? Huna lolote utakuwa mzushi tu wewe
 
Mkuu acha kutokwa na povu kwa kulilia misaada ya wazungu, tufanye kazi kwa bidii watz wote tuachane na dhana ya bila misaada nchi haiendelei. Nchi yetu tuna rasilimali karibu aina zote kwa hiyo habar za misaada tuziweke kando tupige kazi
Soma tena uelewe stress zako usizitolee kwangu.
 
Tuombe Mungu hili lisitokee maana huu ugumu wa Maisha tulionao unatutosha hatutaki madhara zaidi.
Acha woga ww, tuliambiwa zaid ya mara 1 na watu tofautitofauti wa ndan na nje ya nchi, sasa kama hatukusikia acha watufunze maisha kwa njia mbadala.
 
Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...
Kwa nn asiwe???? Ishii watu wakimchagua atakua tu wasipomchagua hatakua, wewe ni kamtume eti web, hahaha una akili finyu na huamini katika demokrasia hivyo wewe ni adui wa maendeleo ya kisiasa na kiuchumi,
 
Mkuu, Suala La" Vikwazo vya Kiuchumi" ni ngumu sana kutokea, na huwa haviwekwi hivi hivi tu, labda kunyimwa misaada, lakini si vikwazo ndugu yangu, vikwazo ni issue nyingine kabisa.

Vikwazo vya kiuchumi vinawekwa ikiwa nchi imekiuka/ imeweka "SERA" ambazo zinakiuka Misingi Fulani, inaweza kuweka vikwazo vya kibiashara, Uwekezaji au shughuli zingine za kibiashara.

Vikwazo vinawekwa kama nchi inatengeneza Silaha za Maangamizi, eg. IRAN, North Korea ect., AU, Kama nchi Imekiuka Haki za Binadamu, Ukubwa wa vikwazo unategemeana na Ukubwa wa ukiukaji.

Na Vikwazo vya kiuchumi ni hatua kubwa sana, ndio maana Urusi ilipochukua Eneo la Cremea nchini UKRAINE Marekani na EU iliweka vikwazo vya kusafiri kwa maafisa wa Urusi na kushikiliwa kwa mali zao, hivyo vikwazo vya kiuchumi ni hatua kubwa sana.

Kwa swala la Zanzibar, ni ngumu kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa sababu hakuna basis yoyote kujustfy uwekaji vikwazo, MAALIM alijitangaza mwenyewe kuwa ameshinda, TUME haikumtangaza, ingelikuwa TUME imemtamka kama GAMBIA ilivyotokea labda ndo ingewekewa vikwazo lakini napo ni ngumu kwa sababu haki za binadamu hazijavunjwa huko Zanzibar.

Sasa Figisu za Uchaguzi wa UGANDA zilivyotokea hadi MUSEVEN mpaka sasa anamnyanyasa KIIZA BESIGYE kwa nini marekani haijaweka vikwazo? ni ngumu sana.

Marekani inaweka vikwazo kama, Serikali inaua watu wake, inaweza kuweka vikwazo vya silaha, au kutosafiri, kwanza kabla haijaweka huwa inaku-arlet kwanza, mfano Burundi, Marekani imekuwa ikitishia kuiwekea vikwazo lakini hadi sasa bado.

Sudan Kusini ndo imewekewa vikwazo vya silaha kwa kushutumiwa kuua Raia wake mwenyewe.
 
Tuombe Mungu hili lisitokee maana huu ugumu wa Maisha tulionao unatutosha hatutaki madhara zaidi.
Unamuomba mungu haki itendeke waheshimu maoni na chaguo la wananchi na sio kuwa vinganganizi
 
Tuombe Mungu hili lisitokee maana huu ugumu wa Maisha tulionao unatutosha hatutaki madhara zaidi.
Mimi Naomba Sana Marekani waweke vikwazo.
Maana uonevu wa kikatili umezidi kwenye hili taifa, acha vikwazo vije, Kama kuumia ma ccm mengi ndo yataumia maana yapo mengi na ndo majinga zaidi.
Kama kufa acha tufe tu Kwa shida, nchi imefikia pabaya Sana hii, na si Zanzibar tu, hata Tanzania bara hali ni mbaya Sana, kuna mtu anajifanya mungu na hataki kukosolewa hata kidogo na ameminya demokrasia na Uhuru wa habari.
kwanza naona Marekani wanachelewa tu, taifa limekosa dira, imekuwa kila Siku ni kufukuza watu hovyo Kwa Sababu za hovyo.
Kikwete umetuachia legacy mbaya Sana.
 
Hii sio tetesi. Huu ni mpango umeshafanywa toka zamani. Tanzania ilitoa matamko ya kejeli kipindi kile imebaniwa pesa za MCC. Sasa leo ndyo yanatuponza.
 
Mpaka 2020 karibu wafuasi wote wa chagadema watakuwa wanaongea peke yao barabarani
 
Back
Top Bottom