Tetesi: Kuna tetesi kwamba Marekani inapanga kutangaza vikwazo kwa Serikali ya Tanzania



Wewe umeandika kizalendo maana umetokea ccm na wana ccm ndio wazalendo pekee nchi na ndio waliumbwa na Mungu kutawala nchi. Hongera sana wewe unayefurahia kuvunjwa kwa haki na sheria za nchi
 
Marekani mmeifanya kuwa Mungu,wenu unakaa unaabudu mtu fanya kazi acha fikra mfu,kwani kama wao waliendelea sisi tutashindwa nini.
Misaada yenyewe ni ukoloni mtupu halafu mnaleta ngonjera hapa.
Leo ndio mmeanza kubeza misaada ya wahisani wakati mmeshazingua katika terms zao hasa masuala ya kidemokrasia
 
KIBURI, JEURI NA ULIMBUKENI HAVIJAWAHI KULETA NEEMA WALA KUWA SEHEMU YA UTATUZI WA MATATIZO YALIYOPO.
 
Ni kweli kabisa. Watu waliofirisika kifikra wanadhani nchi hii itajengwa na Marekani. Kama Marekani wangekuwa na dhamira ya kweli kuiletea maendeleo nchi yetu, Tanzania isingekuwa hapa ilipo.
Kutegemea misaada ni sawa na MME ALIYEOA MKE, LAKINI HELA YA KUMTUNZIA MKE WAKE ANATEGEMEA MSAADA KUTOKA KWA MWANAUME MWENZIE.
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe kama Marekani ilivyojengwa na wamarekani wenyewe.
 
Unafikiri Marekani wapo kwa ajili ya kutetea demokrasia ya Tanzania? Kama kuna yeyote nu mwenye wazo hilo anahitaji maombi!
 
Kwani kila anayeandika ni CUF au CDM??
 
Ata ww inaonekana ni gamba
 
Unajuaje kama siyo sera ya Trump.
Mkuu haiwezi kuwa sera ya Trump maana HAJAAPISHWA rasmi. Na mara nyingi yule Waziri atakayechukua wizara ya nje STATE Department ndiye ataketoa SERA na MABALOZI wapya wa Trump.
Kuna wachache wanaweza kubakizwa ama kuondolewa kabisa.

Kwa sasa KISHERIA Obama ndiye rais wa Marekani.
Hata amiri jeshi mkuu ni Obama hata kama zimebakia siku mbili
Bado Trump anaitwa ni rais mtarajiwa.
Hivyo kwa kigupi hana sauti wala sera ya mambo ya nje ambayo yaweza kutekelezwa.
labda KUTWEET pekee!
 
Kama hadi rambirambi tunazitegemea kujengea miundombinu unategemea lini Tanzania itajitegemea.
 
Acha wawekee hivyo vikwazo nchi ngap wamewekewa vikwazo lakin maisha yanaendelea
 
We mpuuzi sana kama CCM wenzio....sasa obama na Feb 2017 anahusika nini? Mwisho wake Jan 20....baada ya hapo ni isiempenda kaja
 
Marekani ni zaidi ya UN. Kama hujui muulize sadam Hussein Kama anaweza kukwambia
 
Mkuu elewa wakati wa kampeni kila mgombea huwa ananadi sera zake, chama huwa na ilani yake, kwahiyo hata kabla ya kuapishwa wananchi wanajua anakwenda kufanyanini.

Pia kumbuka Secretary of states ni appointee wa rais.

Juzi Obama kasema atalifunga gereza la gwantanamo jana Trump kasema yeye hana haja ya kulifunga, unaona sera zinavyopishana hata kabla ya Trump kuapishwa.

Hata Magufuli tulijua sera yake ya viwanda hata kabla ya kuapishwa.
 
Kama tuliweza kuishi baada ya vita vya kagera hii ya sasa haitishi, wakitaka waweke vikwazo bado hatutawasujudu.
 
Acha wawekee hivyo vikwazo nchi ngap wamewekewa vikwazo lakin maisha yanaendelea
Inategemea ni nchi gani inawekewa, North Korea na Zimbabwe zote zina vikwazo ingawa maisha wanaendelea lakini angalia tofauti ya maisha kati ya wananchi wake, vipi Tanzania ikiwekewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…