Tetesi: Kuna tetesi kwamba Marekani inapanga kutangaza vikwazo kwa Serikali ya Tanzania

Tetesi: Kuna tetesi kwamba Marekani inapanga kutangaza vikwazo kwa Serikali ya Tanzania

Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...
Tuna amini sna hadithi za pangu pa kavu Tia mchuzi....rumours?
 
fanya utafiti. hela za kuendesha ofisi huko sekta ya umma hamna, na mwaka 2020 vyama vya upinzani vijijenge tu vitakuwa na kazi ndogo sana kwasababu hakuna uchumi unaojengwa hapa na wajenga uchumi wanafanya kazi katika mazingira magumu sana sana. uliza mfanyakazi wa umma yeyote atakuambia.tunawaona wanavyohangaika na tunaongea nao kila siku, wanatia huruma na wanapata shida sana.
Kwani hawalipwi mishahara yao? Wanalalamika ofisi haziendi kwani ni za kwao? Huo uzalendo wa kutaka kazi za serikaki ziende vizuri wameupata lini na kwasababu zipi?
Sio hawa tuliokuwa hatuwakuti ofisini saa nne asubuhi? Sio hawa waliokuwa wanashughulikia mambo yetu mwaka mzima bila majibu?
Waambie kama mwenye ofisi anakulipa unachostahili ila kazi zake anazichelewesha mwenyewe muache aue ofisi yake kwani wa kuulizwa ni yeye sio wewe.
Saa nyingine muwaambie hao mnaowaita watumishi waache kiherehere na umbea, wewe ni daktar mfano dawa hakuna na umeshamwambia mwenye nchi yake hataki kuleta dawa, nenda kazini mwisho wa mwezi kachukue chako acha umbea, ukiulizwa waambie wamuulize aliyewaahidi na sio wewe.
Wanaolalamika ni wezi tu, mtu anabomoa nyumba yake kwa hiari yake wewe uliyekodishwa kufabya jazi ya kubomoa unalia nini wakati unalipwa hela ya kubomolea?
Kama magar ya ofis hayatembei kwani daladala nazo hazitembei na wao wanalazimishwa kutembea kwa miguu? Magar gani hayo hayatembei? Yale wanayoyatumia kwenye harusi zao na mambo yao? Wewe ni secretary ulikuwa unakuja kwa daladala unawashwa nini ukiona mashangingi yamepakiwa uwani? Kama ulipewa gari kama mkataba wako unavyosema na wamekupokonya bila kukupa usafiri nenda kashtaki kuvunjiwa mkataba wa kazi wakulipe.
Waambie hao watumishi waache unafiki kama wanatendewa mabaya wanashindwa vipi kuungana kuishtaki hii serikali choka mbaya wanawaambia nyinyi wa vijiweni wakati hamuwezi kuwasaidia chochote.
 
Hao Marekani waambie wajishushie rungu wenyewe na kujiwekea vikwazo wenyewe kwa ujinga walioufanya kwenye uchaguzi wao.
Kama taifa kubwa namna ile Rais anaamuliwa na watu 370 huoni nao wanahitaji kujiwekea vikwazo? Waambie chaguo la wengi kwa maana ya wananchi na sio magavana ni yule bibi yao na sio huyo babu yao.
Hata hivyo USA hata ukimchoma raia wao moto hadharani ila ukalinda maslahi yake hawatakulaumu na watakuongezea fungu zaid.
USA sio kama chadema au cuf wakinuna wamenuna, wao maslahi yao mbele mengine mtamalizana wenyewe, na hawataweka kikwazo chochote kila zaid ya kujikomba kwetu tu. Wakisusa China na Putin wanakula kirahisi tu yeye abakie na demokrasia yake.
 
mimi ni mtanzania halis. kwa makandokando yaliyotokea zanzibar mwaka jana naunga mkono wazo la marekani. tujibebe wenyewe.
 
Hao Marekani waambie wajishushie rungu wenyewe na kujiwekea vikwazo wenyewe kwa ujinga walioufanya kwenye uchaguzi wao.
Kama taifa kubwa namna ile Rais anaamuliwa na watu 370 huoni nao wanahitaji kujiwekea vikwazo? Waambie chaguo la wengi kwa maana ya wananchi na sio magavana ni yule bibi yao na sio huyo babu yao.
Hata hivyo USA hata ukimchoma raia wao moto hadharani ila ukalinda maslahi yake hawatakulaumu na watakuongezea fungu zaid.
USA sio kama chadema au cuf wakinuna wamenuna, wao maslahi yao mbele mengine mtamalizana wenyewe, na hawataweka kikwazo chochote kila zaid ya kujikomba kwetu tu. Wakisusa China na Putin wanakula kirahisi tu yeye abakie na demokrasia yake.
duh bange za wapi hizi. je katiba ya marekani inasemaje kuhusu uchaguzi?
 
Duh! Aisee yaani maisha yalivyo makali sasa hivi ndiyo watuongezee na vikwazo vya kiuchumi si tutakufa sasa?
 
Hata hapa kwetu tunatengeneza Silaha za maangamizi kama hiyo yaweza kuwa sababu ya vikwazo.
Hivi kumnyima msaada wa chakula mtu ambaye amekumbwa na ukame na hana chakula hizo sio silaha za maangamizi?
 
Uzushi tu huu, Yaan vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa vishindwe kupata hizi tetesi wewe ambaye upo Tanzania ndo uipate?

Hakuna kitu kama hicho, na Obama hawezi kufanya kitu kama hicho, kama TUME ya uchaguzi ingelikuwa imemtangaza rasmi Maalim Seif kama Rais afu CCM ikashinikiza matokeo yafutwe hapo kweli vikwazo vingewekwa, lakini kwa namna ilivyotokea ni ngumu sana hatua kama hizo kuchukuliwa, labda useme kuwa, MAREKANI ilazimishe mazungumzo kati ya CUF na Serikali yafanyike lakini si vikwazo.
Una uhakika gani kama mleta uzi sio sehemu ya "chombo kikubwa cha kimataifa"?
 
Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...
labda utoe sabab za kwnn awez kuw Raisi wa Zanzibar.. kwn kuna watu wameandikiw kuongoza wao tu ktk nchi hii... iQ yako ndogo ndio inayosababsha umaskin ktk nchii hii maana watu dizain yako mko weng sn...
 
na underson ndambo.

Taifa la Marekani linatarajia kushusha rungu la aina yake kwa serikali ya Tanzania kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kutokana na sakata la uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Habari zinadokeza kuwa taifa hilo kubwa duniani litaweka vikwazo vya kiuchumi kwa Tanzania hali itakayopelekea Tanzania kuandika historia nyingine mbaya mbele ya uso wa dunia.

Serikali ya Marekani tayari imezuia misaada mbalimbali kwa Tanzania na pia ndiyo iliyoshinikiza Tanzania kunyimwa fedha za MCC, pamoja na kuzishawishi nchi zengine. Serikali ya Tanzania ipo hatarini kukumbwa na janga la njaa, ikiendelea kupuuza juhudi za kimataifa kuitaka kuumaliza kwa haraka mgogoro wa Zanzibar unaofukuta kwa kuacha haki itendeke kabla ya Febr 2017.

Habari zinadokeza kuwa balozi wa Marekani nchini atatoa msimamo unaoelezwa kuwa 'mkali' ili kuishinikiza serikali ya Tanzania kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye uchaguz mkuu wa Zanzibar uliofanyika 25th Oct 2015.
Ndoto za mchana mbaya sana.
 
Haya ndiyo makosa yaliyifanyika ba upinzani bara, miaka mitano ikitumika kunchafua Kikwete. rais anayemaliza muda wa kutawala badala ya kukuna vichwa kumuandaa mgombea imara atakayepambana na mgombea yeyote atakayeletwa na ccm.

Kupambana na kumchafua Shein visiwani ni kupambana na Kivuli wenzenu wanajipanga jutafuta mgombea wa 2020 ninyi mbatafuta Shein kuadhibiwa mtajasituka uchaguzi umefika
 
Umeandika kinazi...utakuwa ni CUF au CHADEMA...unafurahia Tanzania kuwekewa vikwazo...dah...Watanzania wengine bwana kazi ipo...haya endeleeni kuandika hivyo...tutaona mwisho wake utakuwaje...Lakini lililo wazi ni kuwa Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar na haitatokea kuwa hivyo...

Wewe unafurahia 'wenyewe kwa wenyewe' kuwekeana vikwazo vya kidemokrasia?
 
Back
Top Bottom