Wakuu naomba kufahamishwa tofauti kamili ya hayati na marehemu na je kwa case hii ya Rais wetu aliyetutoka hivi karibuni John Pombe Joseph Magufuli,Je tutamuita marehemu au Hayati au yote kwa pamoja na kwanini.
Asanteni
Rest easy Mr President, mwenyezi Mungu akulaze mahali unapostahili,Amina.
Pia nilikuwa natatizwa Sana... Sijapitia post zote hapo juu but nilizopitia sijaona tofauti sahihi... Japo Kuna mmoja alisema hayyat ni uhai akabishiwa but alikuwa sahihi... Page ya 1 au 2.
Iko hivi....
Hayati limetokana na neno la kiarabu likimaanisha uhai au vital kwa kingereza...
Kulikuwa na mafuta ya Naitwa hayyat... mambo ya kuharibiana biashara wakasema ni kwa ajili ya kupata maiti...
Basi ikawa imezoeleka hivo kuwa Hayati ni maiti/marehemu....
Badae Sana BAKITA wakajua kufafanua but ikawa ngumu kutoka ktk jamii...
Ndo wakafikia muafaka kuwa neno Hayati litumike tu pale unapoelezea matendo aliyokuwa anatenda marehemu akiwa Hai..
Mfano Hayati Magufuli alipendelea Sana watu wafanye kazi. 👍
But Ukisema Hayati Magufuli atazikwa kesho hii sio sahihi but Sema marehemu Magufuli atazikwa kesho.
Hayati babu yangu alikuwa analia Sana mchicha hii ni sahihi...
Hayati babu yangu aliacha shamba kubwa... Hii sio sahihi kwa kuwa hujaelezea alichokuwa anapenda kufanya marehemu.
Sema tu ni kutojua kwetu tu nadhan Hayati ni spesho kwa ajili ya watu maarufu... Hapana.
Kumbuka kuwa huwa tunawaombea marehemu na sio Hayati.
NB
Salamu Za Rambirambi ni Salamu Za pongezi....ipekue hii uone tunavotumia tofauti...