Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

Wakuu naomba kufahamishwa tofauti kamili ya hayati na marehemu na je kwa case hii ya Rais wetu aliyetutoka hivi karibuni John Pombe Joseph Magufuli,Je tutamuita marehemu au Hayati au yote kwa pamoja na kwanini.

Asanteni

Rest easy Mr President, mwenyezi Mungu akulaze mahali unapostahili,Amina.
 
Mimi nijuavyo maneno yote mawili marehemu na hayati hutumika kwa kutangulizwa kabla ya kutaja jina la mtu aliyekwisha kufariki.

Lakini tofauti yake ni kwamba neno marehemu linatumika bila kujali kama aliyefariki amefariki leo muda mfupi uliopita, wiki iliyopita, miaka kumi, miaka hamsini au zaidi iliyopita wakati hayati linatumika pale mtu anaezungumziwa habari zake alikuwa ni mtu maarufu katika jamii tena anakuwa alifariki muda mrefu kidogo uliopita pengine miaka kadhaa nyuma mfano hayati Mwalimu Nyerere, hayati Shaaban Robert na wengineo. Pengine ndiyo maana mleta mada umekuwa ukisikia akina "hayati" wachache tofauti na marehemu kwa sababu wengi tunakufa bila umaarufu wowote au kuacha legacy yoyote nyuma yetu.

Sijawahi kusikia mtu aliyefariki mfano leo asubuhi au jana akatanguliziwa jina la hayati.
Nashukuru kwa ufafanuzi mzuri sana.
Baba au mama yangu ambaye kwangu kanitendea mengi na makubwa nimwite marehemu au hayati?
 
Maneno mengi ya kiswahili yametokana na lugha ya kiarabu
Na haya maneno mawili ambayo ni Marehemu (Marhoum) ni aliyekufa
Na Hayati kama linavyotamkwa maana halisi kiarabu ni My life
Hutumika sana kwa wapendanao
Unamwambia mpenzi wako wewe ndio maisha yangu

Ila wahenga wakalichukua tofauti
Kwangu naona marehemu ni marehemu tu au mfu
 
Wakuu naomba kufahamishwa tofauti kamili ya hayati na marehemu na je kwa case hii ya Rais wetu aliyetutoka hivi karibuni John Pombe Joseph Magufuli,Je tutamuita marehemu au Hayati au yote kwa pamoja na kwanini.

Asanteni

Rest easy Mr President, mwenyezi Mungu akulaze mahali unapostahili,Amina.
Pia nilikuwa natatizwa Sana... Sijapitia post zote hapo juu but nilizopitia sijaona tofauti sahihi... Japo Kuna mmoja alisema hayyat ni uhai akabishiwa but alikuwa sahihi... Page ya 1 au 2.
Iko hivi....
Hayati limetokana na neno la kiarabu likimaanisha uhai au vital kwa kingereza...
Kulikuwa na mafuta ya Naitwa hayyat... mambo ya kuharibiana biashara wakasema ni kwa ajili ya kupata maiti...
Basi ikawa imezoeleka hivo kuwa Hayati ni maiti/marehemu....

Badae Sana BAKITA wakajua kufafanua but ikawa ngumu kutoka ktk jamii...
Ndo wakafikia muafaka kuwa neno Hayati litumike tu pale unapoelezea matendo aliyokuwa anatenda marehemu akiwa Hai..
Mfano Hayati Magufuli alipendelea Sana watu wafanye kazi. 👍
But Ukisema Hayati Magufuli atazikwa kesho hii sio sahihi but Sema marehemu Magufuli atazikwa kesho.
Hayati babu yangu alikuwa analia Sana mchicha hii ni sahihi...
Hayati babu yangu aliacha shamba kubwa... Hii sio sahihi kwa kuwa hujaelezea alichokuwa anapenda kufanya marehemu.

Sema tu ni kutojua kwetu tu nadhan Hayati ni spesho kwa ajili ya watu maarufu... Hapana.
Kumbuka kuwa huwa tunawaombea marehemu na sio Hayati.

NB
Salamu Za Rambirambi ni Salamu Za pongezi....ipekue hii uone tunavotumia tofauti...
 
Mfano Hayati Magufuli alipendelea Sana watu wafanye kazi. [emoji106]
But Ukisema Hayati Magufuli atazikwa kesho hii sio sahihi but Sema marehemu Magufuli atazikwa kesho.
Hayati babu yangu alikuwa analia Sana mchicha hii ni sahihi...
Hayati babu yangu aliacha shamba kubwa... Hii sio sahihi kwa kuwa hujaelezea alichokuwa anapenda kufanya marehemu.

Sema tu ni kutojua kwetu tu nadhan Hayati ni spesho kwa ajili ya watu maarufu... Hapana.
Kumbuka kuwa huwa tunawaombea marehemu na sio Hayati.

NB
Salamu Za Rambirambi ni Salamu Za pongezi....ipekue hii uone tunavotumia tofauti...
Asante kwa ufafanuzi mzuri
 
Kipindi cha maombolezo kabla ya mazishi ni marehemu kwa kuwa tunamuombea MWENYEZI MUNGU amrehemu.
Baada ya mazishi anakuwa hayati, tukikumbuka mambo ya enzi zake.

Hiyo tafsiri umeipata wapi???

Screenshot_20210321-070204.png
Screenshot_20210321-070138.png
 
Back
Top Bottom