Wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa hayati lakini sio wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa marehemu.
Mfano, Ukimuua jambazi fulani aliyetaka kukudhuru huyo huwezi na itakuwa ni jambo la kushangaza umwite Marehemu fulani lakini haitashangaza ukimwita hayati fulani.
Marehemu ni jina linaloanza kutajwa kabla ya jina la mtu aliyekufa kama dua ya rehema kwake na rehema hizo ni kutoka kwa Mungu.
Hayati ni jina linalotangulia jina la mtu aliyekufa.na lipo kama utambulisho tu kwamba mtu huyo kishafariki, Marehemu ni jina linaloangulia jina la mtu aliyekufa linalotambulisha kwamba mtu huyo kafariki na anaombewa rehema kutoka kwa Mungu, Kwa kiarabu neno hilo ni Marhum yaani mtu mwenye rehema au mtu anayehitaji rehema.
Kwanini unashindwa kuelewa ndugu???.
Mtu yeyote aliyekufa anaitwa hayati lakini sio kila mtu aliyekufa anaweza kuitwa marehemu.