Kuna tofauti gani kati ya Hayati na Marehemu?

Kipindi cha maombolezo kabla ya mazishi ni marehemu kwa kuwa tunamuombea MWENYEZI MUNGU amrehemu.
Baada ya mazishi anakuwa hayati, tukikumbuka mambo ya enzi zake.
... ila sio kila marehemu ana hadhi ya kuwa hayati baada ya mazishi; ungefafanua kwa kina ili kutoacha maswali yasiyo na ulazima.
 
Kipindi cha maombolezo kabla ya mazishi ni marehemu kwa kuwa tunamuombea MWENYEZI MUNGU amrehemu.
Baada ya mazishi anakuwa hayati, tukikumbuka mambo ya enzi zake.
Hayati inatumika kumaanisha mtu anayetajwa kishafariki na marehemu ni hivyo hivyo isipokuwa Marehemu inatumika kama unataka huyo aliyefariki apate rehema za Mungu ama awe hajazikwa au awe kishazikwa kwa kipindi chochote.

Mfano kwa mtu muovu kama Firauni huwezi kumuita Marehemu ila unaweza kumuita Hayati kumaanisha tayari ni mtu aliyekufa.
 
Kipindi cha maombolezo kabla ya mazishi ni marehemu kwa kuwa tunamuombea MWENYEZI MUNGU amrehemu.
Baada ya mazishi anakuwa hayati, tukikumbuka mambo ya enzi zake.
Hayati inatumika kwa marehemu ila sio wote, bali ni yule mwenye nafasi fulani katika jamii au labda niseme inatumika kwa yule mtu ambae katika maisha yake ameacha alama, mfano Hayati Bob Marley nk..
Ila akifa mtu wa kawaida anakuwa tu marehemu siku zote....
 
Hii sikujua, merci!
 
Sio sawa, Hayati inatumika kwa mtu yeyote aliyekufa na Marehemu inatumika kwa mtu aliyekufa na unataka mtu huyo apate rehema za Mungu huko alipo ndipo utaanza kwa kumuita Marehemu fulani.
 
Mi niliandika maelezo kwa mujibu wa kugha ya kiswahili na sio imani ya kidini.
 
Diamond pia Afundishwe hili Maana pale Taifa kang'ang'ana Oh Hayati Raisi Alinipigia Simu kwenye Sakata Nilipomkataa baba Yangu
 
Mi niliandika maelezo kwa mujibu wa kugha ya kiswahili na sio imani ya kidini.

Marehemu ni yule mtu anatakiwa apate rehema, sasa rehema hizo zinatoka wapi???---- sio zinatoka kwa Mungu??!!, neno rehema linao msingi wa kidini.
 
NIlisema kuwa nimeandika kwa mujibu wa kiswahili na sio kidini kifupi ni kwamba wanaomuita Magufuli Hayati wako sahihi.
Watu wote wanaweza kuitwa marehemu ila sio wote wana hadhi ya kuitwa HAYATI.
 
Wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa hayati lakini sio wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa marehemu.

Mfano, Ukimuua jambazi fulani aliyetaka kukudhuru huyo huwezi na itakuwa ni jambo la kushangaza umwite Marehemu fulani lakini haitashangaza ukimwita hayati fulani.

Marehemu ni jina linaloanza kutajwa kabla ya jina la mtu aliyekufa kama dua ya rehema kwake na rehema hizo ni kutoka kwa Mungu.

Hayati ni jina linalotangulia jina la mtu aliyekufa.na lipo kama utambulisho tu kwamba mtu huyo kishafariki, Marehemu ni jina linaloangulia jina la mtu aliyekufa linalotambulisha kwamba mtu huyo kafariki na anaombewa rehema kutoka kwa Mungu, Kwa kiarabu neno hilo ni Marhum yaani mtu mwenye rehema au mtu anayehitaji rehema.

Kwanini unashindwa kuelewa ndugu???.

Mtu yeyote aliyekufa anaitwa hayati lakini sio kila mtu aliyekufa anaweza kuitwa marehemu.
 
Kipindi cha maombolezo kabla ya mazishi ni marehemu kwa kuwa tunamuombea MWENYEZI MUNGU amrehemu.

Baada ya mazishi anakuwa hayati, tukikumbuka mambo ya enzi zake.
Yap....ni contextual. Enzi (Hayati), Dua/Maombi(Marehemu). Kwa hivyo naweza kuomba misa kanisani kwa ajili ya MAREHEMU Julius Kambarage Nyerere au Nikaandaa muhadhara au mkanasha kuhusu maisha ya kisiasa ya HAYATI Julius Kambarage Nyerere
 
Wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa hayati lakini sio wote waliokufa wanayohadhi ya kuitwa marehemu.

Mfano, Ukimuua jambazi fulani aliyetaka kukudhuru huyo huwezi na itakuwa ni jambo la kushangaza umwite Marehemu fulani lakini haitashangaza ukimwita hayati fulani.

Marehemu ni jina linaloanza kutajwa kabla ya jina la mtu aliyekufa kama dua ya rehema kwake na rehema hizo ni kutoka kwa Mungu.

Hayati ni jina linalotangulia jina la mtu aliyekufa.na lipo kama utambulisho tu kwamba mtu huyo kishafariki, Marehemu ni jina linaloangulia jina la mtu aliyekufa linalotambulisha kwamba mtu huyo kafariki na anaombewa rehema kutoka kwa Mungu, Kwa kiarabu neno hilo ni Marhum yaani mtu mwenye rehema au mtu anayehitaji rehema.

Kwanini unashindwa kuelewa ndugu???.

Mtu yeyote aliyekufa anaitwa hayati lakini sio kila mtu aliyekufa anaweza kuitwa marehemu.
FYI hakuna jambazi anaeitwa Hayati kwa mujibu wa Bakita only kwa mujibu wa hiyo imani yako ya dini uliyosema ndio unaweza kufanya hivyo

Kawaida wezi, vibaka, na watu wote wanaomaliza muwa wao wa kuishi hapa duniani, kuanzia mitaani na hata kwenye vyombo vya habari huwa wanaitwa marehemu (wakimaanisha mtu aliekufa/kufariki) na wanatumia neno hilo pasipo kujali imani ya mhusika sababu ndio kiswahili fasaha

Wakifa majemedari utaona lugha inabadilika kuanzia kwenye media na kila mahali na mtu huyo anaitwa HAYATI!!

Wewe binafsi unaweza kuita utakavyo sababu ya imani yako hamna atakaekuzuia ila kwenye jamii hususa ni vyombo vya habari usitegemee hilo.
 
Back
Top Bottom