Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Inabidi waifanyie implementation,watu huko huko Dar wana ekari zaidi ya 10 wameziacha tu....Mbona Sumaye walimnyang'anya ekari zake 33 huko Bunju A? Balali naye ana ekari kibao kafuga mapori ,Kwa kifupi viongozi wengi wamehodhi ardhi na kufuga mapori tu inabidi wanyang'anywe.
Sisi wenyewe tunazo 10 ila zina fensi
 
Hapo sijazungumzia frame na viduka uchwara.... hadi mama ntilie
kule mwisho kabisa makonde vilikuwepo vyote hivyo mda tu kule tulikua tunajipigia wali nyama buku na gongo unapata mpaka papuchi hadi jero unapata.
upande wa pili sasa ndio ushuani usivuke uende chole,sellasie road hadi kuna border badae ukitembea tu slipway hii hapa tatizo nyie mlikua watoto wa geti ukitoka mjini,shule ukirudi ndani unacheza p3 na kunywa maziwa.
wagumu tulikua jirani tu tunapiga mishe na kona zetu tunazijua.masaki hiyohiyo
 
Baada ya kutoka Masaki tulihamia Oysterbay baada ya hapo nikaanza kujitegemea mwenyewe from msasani mafleti krb na ubalozi wa Marekani to Mbezi Makonde then Mikocheni B kwa sasa naishi Kinyerezi na ni kwa sababu ya kazi mimi si mpenzi wa kuendesha distance ndefu kwa kifupi nafanya kazi Julius Nyerere International Airport.Na siteseki, I live my to the fullest.
Fresh kaka. That's the spirit! Kuteseka ni kawaida ndugu yangu, wanaume tumeumbwa mateso
 
Bila kutaja miaka ya kipindi unachokiita "enzi hizo" au "wakati huo" huu uzi ni BATILI.
 
Sema Mbweni sasa hivi ni habari nyingine na mji unakuwa kuelekea Bagamoyo, natamani Dar na Pwani ingeunganishwa uwe mkoa mmoja tu uitwe Dar ili watu wasogeesogee huko, na waondokane na ile dhana ya kutaka kuonekana hawaishi Dar wanaishi nje ya miji
 
Masaki ilikua mbali na sehemu zenye harakati nyingi kama kariakoo na posta.

Ila kadri muda unavyozidi kusogea watu wanasogelea maeneo wanayoishi watu kwenda kufanya biashara.
Hata maeneo mengi pembezoni mwa mji ilikua ni makazi tu, lakini sasa bar na ofisi mbalimbali zinafunguliwa.

Wale tusiopenda kelele tunazidi kusogea tu, acha tuendelee tu miaka 50 ijayo tutafika mikumi
 
Sema Mbweni sasa hivi ni habari nyingine na mji unakuwa kuelekea Bagamoyo, natamani Dar na Pwani ingeunganishwa uwe mkoa mmoja tu uitwe Dar ili watu wasogeesogee huko, na waondokane na ile dhana ya kutaka kuonekana hawaishi Dar wanaishi nje ya miji
Mbweni ya washua kbs ni noma.
 
We utakuwa unampata smbdy kamaka na wakina kiligini

Ova
Hapana kaka, labda kwa majina mengine to name a few, watu maarufu nilikuwa nawafahamu I mean mabro ni kina Mpoki Mwambenja pamoja na Adili (Nigga One) na Robert Mwingira (D-Rob) all the way from Morogoro Stores , Ahmed mtoto wa gavana wa benki kuu mstaafu mzee Rashid ambaye alikuwa opposite na bro Mpoki hawa jamaa walikuwa wakipiga ma- House Party they have influenced me to be diehard fan wa rap music until today I bang Hip Hop music to the fullest.RIP Bro Mpoki,Adili na Rob.🤍🤍🤍🕊️
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;

Enzi hizo wakati naishi mimi:
Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors.

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.
Kumbe tulikuwa pamoja pande hizo mimi nilikuwa na ishi hapo morogorostore mtaa wa mzinga way[emoji1787] shule nilisoma oyster bay primary school
 
Iko hivi miji inatanuka masaki ya zamani au sinza ya zamani au kinondoni ya zamani sio ya sasa hiviipo hivi watu wanahamia na watu wanaondoka kwaiyo miaka 20 ijayo masaki itakuwa ya kawaida kama sinza ya zamani kwaiyo mji mwingine utaibuka kuwa wakishua maana siku hizi wengi wanaamia kigamboni uko kuna mijengo ya maana au bagamoyo siku hizi mjini kuna makelele sana
Siyo chini ya serikali ya ccm ya team msoga ....wahuni wa msoga wao kaziyao ni kuvunja na kuharibu tu
 
Back
Top Bottom