Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

IMG20230506155032.jpg
 
Ama kweli maisha yana badilika sana ,ulichosema ni kweli kabisa .kipindi cha nyuma miaka ya 2000 huko,kuna ki mji kilikuwepo shinyanga na walio kianzisha wengi ni watumishi wa shirika moja hivi.
Wale wazee walifirisi shirika hilo ,na wote walikuwa wamejenga sehemu moja ,nyumba zote zilikuwa na kuta na mageti ,nyasi zilimea kwa kumwagiliwa maji ya kutosha(garden)

Miaka imeenda wazee wakaanza kuugua na kufa mmoja mmoja,inasemekana ukimwi uliwapiga KO ya hatari ,kipindi kile hakua cha ARV wala nn,walikuwa wana share totozi ,si unajua mambo ya pesa.

Nyumba zilibaki na watoto tu ,nyasi zilikauka kila mji.hali ili badirika sana ,baba na mama hawapo ,unazani famia itakuwaje?
Si mji ule tena ambao ilikuwa ukipita unasikia sauti nene za music taratibu na harafu ya vinono vikikaangwa.

Nyumba ziliuzwa na wajomba na mashangazi baada ya wazazi kuondoka gafla na kukosekana mwelekeo wa malezi.
walio baki ni wachache sana ambao hata leo hii uzao wao upo pale
Bila shaka utakuwa unazungumzia mwasele
 
Nimetia timu hapa kuona labda nitawapata street mates wangu maana hiyo ni mitaa yangu .

Kitambo sana Masaki sio sasa kuna mpaka boda boda , mara hostel za wanafunzi wa Muhimbili mh sio patamu tena .

Kwasasa ni uswazi na tunaowapangisha ni maisha ya kawaida ndiyo maana kodi ikikaribia kuisha tunakuja walau wapangaji watastuka wakumbuke kulipa maana kwenye simu janja nyingi.
Gily wa tandale manzese tuna comment wapi😂
 
Masak naona imeanza kuwa uswazi, na mdogo mdogo inaanza kuwa ya kawaida saana, yani saana...

Bar na restaurants nyingi, na security ya premier residential inaondoka kwa kuwa na maghorofa yenye watu wengi sana, lakini zaid nyumba za ghorofa kumi kuendelea zinaongezeka sana.. soon itaanza fanana na Kariakoo.

Security kwa premier residential services ni priority... sasa hapa bungalow hapa ghorofa lenye apartments 40.

Hapo sijazungumzia frame na viduka uchwara.... hadi mama ntilie
Wajanja wamehamia mbweni nyie bakini huko huko.
 
Back
Top Bottom