Aisee
Umenikumbusha mbali sana, kweli tumezeeka
Haile Sellasie road ndio nyumbani kabisa ilikuwa miaka hiyo kabla hujafika Mhalibwa grocery, hebu fikiria ndio lilikuwa duka pekee, ukiacha Supermarket ya Morogoro stores.
Enzi za kina Rob D, na Nigga one (RIP) ndani ya mtaa
Wakati huo basi ni moja tu la UDA, mitaa kimyaaaa
Kibibii ya Tryphone Maji peke yake ndio alikuja kupewa leseni ya daladala
Mitaa mingine unajikuta ni wewe peke yako barabara nzima
Nilikuja kwenda na familia miaka kadhaa niwaonyeshe madogo wangu nilipokulia, duuh..hadi aibu kama uswahilini tu mabaa na bodaboda, wamasai wametapakaa mtaa mzima, tulipokuwa tunaishi sasa mbele kuna Pub, nilishindwa hata niwaonyeshe nini watoto wenyewe hawajazaliwa bongo ni ilikuwa kituko tu
Masaki kumechafukwa na kuvurugwa haswa, sio tena residential area ya kishua