Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Kuna tofauti kubwa kati ya Masaki niliyoishi mimi na Masaki ya leo

Masak naona imeanza kuwa uswazi, na mdogo mdogo inaanza kuwa ya kawaida saana, yani saana...

Bar na restaurants nyingi, na security ya premier residential inaondoka kwa kuwa na maghorofa yenye watu wengi sana, lakini zaid nyumba za ghorofa kumi kuendelea zinaongezeka sana.. soon itaanza fanana na Kariakoo.

Security kwa premier residential services ni priority... sasa hapa bungalow hapa ghorofa lenye apartments 40.

Hapo sijazungumzia frame na viduka uchwara.... hadi mama ntilie
Kweli mfano mm naishi Hapa mwaya street ckuiz had mama ntilie kibao kama sio masaki yan
 
Dah! Mnaongelea mambo mazito mno. Kama isingekua kufika chuo ingenichukua muda sana kufika Dar. Naishukuru elimu kunifikisha Dar bila kuwasahau HESLB. Mwisho wangu ilikuwa Chalinze wakati naenda shule Iringa. Nilikuwa nikiona kile kibao kinaelekeza Dar napatwa na mzuka balaa. Siku nimekuja Dar kwa mara ya kwanza nikamtafuta rafiki yangu na kumsihi anipeleke nione Coco Beach. Bahati mbaya kwenye siku zangu za mwanzo kabisa Dar nilipata mkasa ulionipa aibu kubwa sana... pale Mabibo hostel ukivuka barabara kwa mbele kidogo kama unaenda Buguruni kulikuwa na Bar ambayo pia ilikuwa na gesti... enzi hizo Akudo impact ndo inavuma hatari. Sasa mimi nikawa namtaka mhudumu flani ila akawa ananila hela kunipa hanipi katika kumlazimisha lazimisha kukawa kuna kubishana nae.. mara akatokea jamaa sijui ndo meneja akanichimba mkwara na kuniambia nipotee eneo lile nisionekane kwasababu naleta kero huku hata bia sinywi.
 
Masaki ya leo sio ile tulivu ya kishua tena, limebaki jina tu.

Kuna ushamba katikati umetokea ata upanga wakati sisi tunakuwa yalikuwa maeneo ya wafanyakazi wa serikali wenye kipato cha kawaida hasa walimu. Eti siku hizi prime areas.

Yaani watu badala ya kutanua jiji wamevunja na kujenga maeneo hayo hayo machache na kuharibu mandhari ya maeneo; masaki kuna maeneo nilipita nikawa najiuliza hivi ndio hapa kweli ata kilima nyege sikukitambua niliposhuka kwa kushangaa.
Hapo kwenye kilimanyege kwenye huduma
 
Hapo kwenye kilimanyege kwenye huduma
Kilima jina kwa sababu cha ghafla halafu kifupi ukipita ndani ya gari kuna ka msimumuko fulani. Sijui siku hizi kama wanatoa huduma hapo.

Hayo maeneo palikuwa na uwazi siku hizi kumejaa ma bar ukipita usiku kama unaijua masaki ya zamani na ujaenda muda mrefu panakuchanganya. Ilipo elements opposite alikuwa anakaa shushushu mmoja kanali Mnyani kulikuwa na space kubwa tu hadi ufikie gate lake.

Kulikuwa kimya sana maeneo hayo hasa kwenye hiyo cross-junction hapo ya kilima nyege halafu land niliyokuwa naijua ni nyumba ya captain Mutafungwa zile chongoma hazipo tena. Ukishuka chini kwenye walikokuwa wanakaa hakina Wasia Mushi unatembea barabarani magari kupita nadra, ukipanda juu wanapokaa kina James Lugembe ile mitaa ukipita kama humjui mtu ata bila ya kuitiwa mwizi unaweza jistukia.
 
Kilima jina kwa sababu cha ghafla halafu kifupi ukipita ndani ya gari kuna ka msimumuko fulani.

Hayo maeneo palikuwa na uwazi siku hizi kumejaa ma bar ukipita usiku kama unaijua masaki ya zamani na ujaenda muda mrefu panakuchanganya.

Kulikuwa kimya sana maeneo hayo hasa kwenye hiyo cross-junction hapo ya kilima nyege. Ukishuka chini walikokuwa wanakaa hakina Wasia Mushi unatembea barabarani magari kupita nadra, ukipanda juu wanapokaa kina James Lugembe ile mitaa ukipita kama humjui mtu ata bila ya kuitiwa mwizi unaweza jistukia.
Kabisa kiongozi!leo kimebaki tu kile kilima 😂 na pale ndo mpaka kati ya Masaki na Obey!Wakijenga upya ile barabara nafikiri kitakufa!
 
Kabisa kiongozi!leo kimebaki tu kile kilima 😂 na pale ndo mpaka kati ya Masaki na Obey!Wakijenga upya ile barabara nafikiri kitakufa!
Imearibika sana hakuna open space kabisa na land marks za zamani hazipo tena. Mie nilipotea ilikuwa usiku ata niliposhuka hapo kilima nyege sikujua wala IST sikuitambua maana mbele pale kulikuwa na kimila fulani unapanda kwenda kwa Dr Mbawala nafika sikioni nakutana na high rises nikajiuliza hapa nipo masaki kweli; hiyo ilikuwa baada ya kama 18 years natokea kijijini.

Wamepaaribu sana kumebaki jina tu.
 
Kwanza kabisa naomba mnisamehe kama Uzi wangu unaofanania na kudhihaki ila hii si shabaha yangu!Shabaha yangu kubwa ni kutoa taswira ya namna mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya maeneo husika yalivyotofautiana sana na mpango wa awali wa matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kabla;

Enzi hizo wakati naishi mimi:
Masaki ilikuwa ni Residential Area pekee huwezi kuta ofisi yoyote iwe ya serikali au taasisi binafsi ikifanya shughuli zake maeneo hayo.

Miaka hiyo Masaki huwezi kuta jengo lenye urefu wa ghorofa zaidi ya ghorofa tatu kwa uchache na upekee wake utakutana na mazingira ya namna hiyo kwny maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya flats yakiwemo maeneo kama ya TIB,THB na kule Harbors.

Masaki ya wakati huo wahudumu walikuwa hawarudi makwao zaidi ya kuishi kwenye nyumba za servants zilizokuwa nyuma ya nyumba kubwa za maboss wao

Wakati huo Masaki huwezi kuta watu wakiwa wamezagaa zagaa hovyo asilimia kubwa kwenye mtaa husika watu tulikuwa tukifahamiana kwa sura hata kama tulikuwa hatusalimiani.

Kwa kifupi mimi nimeishi na kukua kwenye mtaa wa Haile Selassie.
VItuo vya boda boda, bodaboda wamekuwa wengi,wakati Kila nyumba Ina ndinga zaidi ya Moja
 
Ama kweli maisha yana badilika sana ,ulichosema ni kweli kabisa .kipindi cha nyuma miaka ya 2000 huko,kuna ki mji kilikuwepo shinyanga na walio kianzisha wengi ni watumishi wa shirika moja hivi.
Wale wazee walifirisi shirika hilo ,na wote walikuwa wamejenga sehemu moja ,nyumba zote zilikuwa na kuta na mageti ,nyasi zilimea kwa kumwagiliwa maji ya kutosha(garden)

Miaka imeenda wazee wakaanza kuugua na kufa mmoja mmoja,inasemekana ukimwi uliwapiga KO ya hatari ,kipindi kile hakua cha ARV wala nn,walikuwa wana share totozi ,si unajua mambo ya pesa.

Nyumba zilibaki na watoto tu ,nyasi zilikauka kila mji.hali ili badirika sana ,baba na mama hawapo ,unazani famia itakuwaje?
Si mji ule tena ambao ilikuwa ukipita unasikia sauti nene za music taratibu na harafu ya vinono vikikaangwa.

Nyumba ziliuzwa na wajomba na mashangazi baada ya wazazi kuondoka gafla na kukosekana mwelekeo wa malezi.
walio baki ni wachache sana ambao hata leo hii uzao wao upo pale
Hiyo sehemu imejengwa miaka ya 90's na wafanyakazi wa SHIRECU,2000's ilikuwa tayari ilishadoda.Nilipelekwa kuangalia nyumba ya kupanga unakuta jumba kuubwa hadi linatisha.Nadhani kwa sasa patakuwa hoi zaidi.
 
Upo sahihi,mwezi uliopita kuna nyumba mitaa ya Mkadini Oysterbay karibu na Qatar Charity tulienda kugonga geti akatoka beki tatu na kutuambia bosi hakai hapo siku hizi muda sana...
Dah kumbe ndo nyinyi mligonga geti nikawafungulia? Madalali matapeli.
 
Zambia,lusaka kuna sehemu ya kishuwa ilijengwa inaitwa kingsland
Aise mahala hapo si mchezo
Bongo sijui tunashindwa nn
Unajua hakuna eneo baya sema tTizo ni namna ya watu wanavyojenga
Huyu kajenga vile huyu kajenga kile
Huyu kaziba njia basi vurugu tupu

Ova
Kuna mama mmoja msomi kwenye hiyo sector ya urban planning nilikutana nae short course Dodoma kwenye maswala monitoring and evaluation nilimuuliza nini chanzo cha huu utopolo wa ujenzi holela alinijibu in short ni "kuacha kila mtu ajenge"vitu hivi vinapaswa kuachia makampuni makubwa ya Real Estates then sisi tunakuwa wanunuzi tu kutokana na nguvu ya mfuko wako.
 
Wakati huo lami haileselasie inashia shule ya IST mbele kote vumbi tu

Ova
Sijui IST ya leo ila IST ya kipindi kile pembeni kulikuwa na kontena watoto wa kishua wakitoka shule wakati wengine wakisubiria kuchukuliwa wanakula pombe na mafegi kwa kwenda mbele dah wakati huo mi nasoma Obey primary school!! Watoto wa kike wazuri kinoma!Mara moja moja watoto wa mtaa tulikuwa tukiruhusiwa magetini na walinzi tuingie kwenye ile basketball court yao kupiga kikapu.
 
Longtime,kuna mtoto mmoja wa kizungu alikuwaga obay alikuwa anaitwa John bichwa kama mtu alikaa obay na masaki hyu atakuwa anamfahamu...
Wazee wake walikuwa maeneo mengi wanayamiliki huko

Ova
Kbs John alikuwa ni mtu sana pamoja na Banzi wa pale Mbuyuni Primary School!.
 
Upo sahihi,mwezi uliopita kuna nyumba mitaa ya Mkadini Oysterbay karibu na Qatar Charity tulienda kugonga geti akatoka beki tatu na kutuambia bosi hakai hapo siku hizi muda sana...
Mkadini kipindi hiko ulikuwa ni mtaa wa majaji na wanasheria manguli mfano mzuri ni mzee wetu Lubuva,Mihayo pamoja na Jaji Bahati na wengine wengi tu.
 
Back
Top Bottom