Kuna tofauti kubwa kati ya mganga wa kienyeji na mchawi ila jamii imepotoshwa

Kuna tofauti kubwa kati ya mganga wa kienyeji na mchawi ila jamii imepotoshwa

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
8,105
Reaction score
20,307
Kuna tofauti kubwa kati ya mganga wa kienyeji na mchawi ila jamii imepotoshwa na sasa haina uwezo wa kuwatofautisha tena na sasa inaishia kuwaweka kaput moja!!

1. Mganga wa kienyeji ni daktari wa asili ambae ametumika kuitibu na kuikinga jamii dhidi ya mabalaa mbalimbali kwa maelfu ya miaka kabla ya ugunduzi na ujio wa hizi hospitali za kisasa. Kumbuka hizi hospitali za kisasa hazina hata miaka 300 tangu kuanza kumhudumia mwanadamu kwa usahihi kabisa.

2. Uchawi na wachawi wapo pia kwa maelfu ya miaka tangu kuumbwa kwa mwanadamu. Mchawi kazi yake ni kuharibu ndio maana vitabu vya dini zote vimeandika mchawi ni mtu wa kuchomwa maana hana faida yoyote kwa jamii. Utakachojifunza kwa mchawi ni roho mbaya na ukatili wa hali ya juu sana.

3. Kuna aina mbili za uganga wa kienyeji, wa kwanza ni ule wa kuoteshwa(kipaji cha kuzaliwa nacho) na wa pili ni ule kujifunza.
- Ukitaka kujifunza uganga wa kienyeji Kuna ada kama zilivyo ada zingine tu, mfano unaweza kuambiwa ada yako ulete Ng'ombe watano, au mbuzi au hela, ni juu ya maelewano yenu.

4. Uchawi ada yake ni moja tu ya damu! Yani ukitaka kujifunza uchawi utaambiwa mtoe mzazi wako au mtoto wako pendwa.
- Ukitaka kujifunza uchawi hutaambiwa lete hela au lete Ng'ombe.

5. Mganga wa kienyeji ni kama daktari wa lei au mwanajeshi ambao kazi yao ni kulinda jamii kutoka kwenye shida mbalimbali.

6. Mchawi ni kama jambazi au muasi kwenye jamii ambao kazi yao ni kuhakikisha kila anayeinuka kwa maendeleo anarudishwa chini.

7. Mganga wa kienyeji wa ukweli hawezi kukaa Meza moja na mchawi ni kama ambavyo jambazi au muasi hawezi kukaa Meza moja na mwanajeshi.

8. Uganga wa kienyeji ni fani iliyoingiliwa kama fani nyingine siku hizi Kuna waganga wa kienyeji feki wengi kama ilivyo trafiki feki, daktari feki, wachungaji feki etc

9. Kwa masikitiko makubwa jamii ya leo haijui kutofautisha kati ya mganga na mchawi. Jamii inajua wote ni wachawi tu.
 
Unaweza kuta mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji anaumwa balaa,anatibiwa kisha anaambiwa njia zimezibwa kurudi home, so inatakiwa aendelee kukaa kwa mganga,siku zimeenda jamaa anaanza kuaminiwa na mganga, kama kuagizwa dawa,kuwatibu wagonjwa, kadri siku zinavyokwenda anaaminiwa zaidi na kuoneshwa dawa zaidi na zaidi,halipishwi hela kuwa amejua uganga ila kazi zake za usaidizi zimemfanya ajue uganga, badae anapewa eneo anajenga anaishi kwake anakuwa mganga.
 
Kilichosababisha wakaekwa kundi moja ni baada ya waganga kuingiwa na tamaa, wivu hadi kuwa matapeli. Ila kwa dunia ya sasa waganga ni waaminifu ni wachache sana. Mganga wa cku hizi hata kama hawez jambo atakwambia hiyo kwake n kaz ndogo hawana referials kama zaman naskia mganga alikuwa akishndwa anakutuma kwenda kwinge lakn wa cku hizi watakunyonya mali yako cku ukifilisika ndo wanakwambia mambo ya mizimu imekataa kukusaidi. Utapeli huo na tamaa.
 
Unaweza kuta mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji anaumwa balaa,anatibiwa kisha anaambiwa njia zimezibwa kurudi home, so inatakiwa aendelee kukaa kwa mganga,siku zimeenda jamaa anaanza kuaminiwa na mganga, kama kuagizwa dawa,kuwatibu wagonjwa, kadri siku zinavyokwenda anaaminiwa zaidi na kuoneshwa dawa zaidi na zaidi,halipishwi hela kuwa amejua uganga ila kazi zake za usaidizi zimemfanya ajue uganga, badae anapewa eneo anajenga anaishi kwake anakuwa mganga.
Duh
 
Usisahau kuna waganga nao wanatapeliwa..unakuta kamsaidia mtu matoke yake yule mtu akishafanikiwa kutatua tatizo lake....anamwambia mganga kwamba ni uwezo wa Mungu siyo wewe
 
Usisahau kuna waganga nao wanatapeliwa..unakuta kamsaidia mtu matoke yake yule mtu akishafanikiwa kutatua tatizo lake....anamwambia mganga kwamba ni uwezo wa Mungu siyo wewe
Kweli kabisa, hata wachungaji wanatapeliwa
 
Usisahau kuna waganga nao wanatapeliwa..unakuta kamsaidia mtu matoke yake yule mtu akishafanikiwa kutatua tatizo lake....anamwambia mganga kwamba ni uwezo wa Mungu siyo wewe
Hahaha
 
Back
Top Bottom