Mimi naelewa sayansi sana upande wa electronic na software engineering.
Hiyo simu unayotumia unajua ni vipande vya madini asili ndio unapata kutumia mpaka vimekufikisha hapo.
Hakuna uchawi, ni sayansi. Hapo kuna foundry na wafers wala sio uganga. Kuna kampuni kama TSMC, ASML na Corning zimefanya kazi sio magenge ya wachawi.
Kwenye sayansi ungekuwa unaishi ulaya wenzetu teknolojia nyingi wanakopy kutoka kwa wanyama na asili za zamani na uchawi.
Kuiga wanyama, ndege na asili ndio sayansi yenyewe na sio uchawi. Sayansi inaelezea ni namna gani samaki anavuta hewa, ni namna gani nyuki anatoa sauti akipaa ni sababu bawa lake linajipiga mara 200 kwa sekunde moja na kitu gani kinatoa sauti ni mgandamizo wa hewa. Uchawi haujui lolote kuhusu hilo.
Ungekuwa unafatilia makala nyingi youtube utaelewa mfano jina la zombies ni msukule na huu mchanganyiko wa dawa ukielezwa ulitokana na uchawi wa kuwa fanya watu wawe misukule wa kufanya kazi yoyote.
Hakuna uchawi kwenye kuliita zombie jina zombie, mfano kuliita embe kwamba ni embe kuna uchawi au sayansi gani?
Ila kuna sayansi kwenye kutoa scientific name. Maana inafuatia taxonomic hierarchy na imefanyiwa classification. Embe likiitwa Mangifera indica ina maana yake kisayansi na ina utaratibu wake wa kuandikwa. Mturuki, Mreno, Mnyakyusa au Mvietnam anaelewa.
Haijulikani ili kitu kiwe classified kama zombie kiwe na sifa ipi. Sayansi inaondoka contradictions kwenye classification. Sasa nyinyi wachawi zombie, msukule, zimwi, jinamizi, jini, pepo, mzimu mna clear classification ya hivyo vitu. Au leo ukiamka unaliita jini, kesho unaliita pepo.
Hii dawa inatumiwa sana vikosi vya ulinzi wa serikali ndio maana unakuta mwanajeshi huruma hana au wasiojulikana.
Kwenye sayansi hii kitu ipo, kwenye uchawi hamjui mechanism kwa sababu hamtumii sayansi ndio maana hamuwezi kufanya mass production. Kwenye vita ya pili ya dunia, Nazi Germany waliwapa wanajeshi wao methamphetamine ya Pervitin. Kampuni yao kubwa ya madawa duniani kwa sasa hii Bayer ilitoa sana dawa za kulevya kwa wanajeshi wa Ujerumani ili kuondoa usingizi, kupunguza hamu ya kula, kutoa uchovu na kuchangamsha mwili. Hii ni kwa sababu Ujerumani ilikuwa inatumia Blitzkrieg (kushambulia kwa kasi) hivyo muda wa kula na kulala hovyo hawakuwa wanataka kuupoteza wakishambulia.
Walikuwepo wanasayansi wa kijeshi kama Joseph Mengele na walifanya tafiti hata za kichawi kuutoa uchawi kwenye kukariri kuufanya ueleweke kisayansi ili uwe mass utilized. Walishindwa sababu uchawi sio sayansi.
Vita ya Maji Maji ilifeli sababu hii, uchawi ukazidiwa na sayansi ambayo Mjerumani alikuwa anaweza tengeneza bunduki na mizinga mingi sababu inafuata sheria za kisayansi. Wachawi wenzako wakamtegemea Kinjekitile Ngwale ambaye mechanism ya risasi kuwa maji hajui, wanaomfuata hawajui, mass production ya huo uchawi haiwezekani sababu sheria na kanuni za kisayansi hakuna. Mwishowe kilichotokea uliona.