Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Mali za mtu aliyekufa huwa ni za warithi, hivyo hao ndiyo wenye maamuzi ya nini kifanyike katika mali hizo, lakini kwa ushauri wangu ni bora kila mtu achukue cha kwake baada ya kifo tu, kwani mkichelewesha na wakati ukipita ukorofi lazima utatokea ikiwa kizazi kingine kitakapotaka mali za wazazi wao ambao ndiyo warithi.
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Nyumba ya familia siyo busara kuuzwa, hapo ndio kwao atakayhama maisha yakimpiga atarudi hapo ndio nyumbani.

Tatizo kizazi hiki kikishaferi kinadhani kuuza nyumba na kupata mgao wa million 10 ndio zitamtowa kumbe ndio anateketea.

Kama nyumba ipo kariakoo au ilala naunga mkono kuuzwa kwa sababu ya value pesa itakayogawiwa kila mtu ana uwezo wa kununuwa nyumba yake sehemu nyingine na mtaji anapata.
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Kwa nini msitafute mali zenu kama marehemu alivyokomaa?? Alikataa nyumba yake isiuzwe ili ibaki kama alama ya mji wake kwa watoto, wajukuuu na vilembwe.
 
Hiyo nyumba ipo mjini na kama utambulisho wa mji wake Kuna nyumba ambayo alimjengea mama yake(bibi) ipo kijijini ambako ndio chimbuko la ukoo mzima
 
Kwa hiyo kama iko mjini ndiyo haiwezi kuwa alama yake? Huko Kijijini kamjengea mama yake kama ulivyosema si kwake. Mimi nina nyumba yangu Mburahati Dar ndiyo nyumba yangu ya kwanza kujenga kwa jasho langu, kiukweli nisingependa pauzwe bali watoto na wajukuu zangu wapaendeleze ili siku moja mjukuu au kitukuu waje kuvunja na kujenga ghorofa na mji uendelee. Kuuza nyumba ili wagawane pesa wala siyo suluhu ya kutoka kimaisha, tena wasipokuwa makini wanaweza ishia kulala stend...
 
Dawa ya watu bogus kama hawa unawaambia wapige hesabu nyumba inauzwa shingapi kila mtu mgawo wake shingapi unawalipa pesa yao kisheria wasepe halafu utaona watakapoishia.
Inakuwaje kuuza nyumba ya urithi ukawa ubogus Kila mtoto alishakuwa mtu mzima na kwa bahati mbaya mambo yao hayajawaendea vizuri wanatafuta mitaji na kuuza nyumba ni the only way ya kuwa na mtaji ambao utakuwa hauna presha ya marejesho ambapo kwa malengo baadae wanaweza kuchanga na kujenga nyumba Tena kwa ajili ya familia nzima
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Hakuna ubaya mkuu...
Ukiuza usisahau kunistua ili nije nikushauri nini cha kufanya..😊
 
Kwa hiyo kama iko mjini ndiyo haiwezi kuwa alama yake? Huko Kijijini kamjengea mama yake kama ulivyosema si kwake. Mimi nina nyumba yangu Mburahati Dar ndiyo nyumba yangu ya kwanza kujenga kwa jasho langu, kiukweli nisingependa pauzwe bali watoto na wajukuu zangu wapaendeleze ili siku moja mjukuu au kitukuu waje kuvunja na kujenga ghorofa na mji uendelee. Kuuza nyumba ili wagawane pesa wala siyo suluhu ya kutoka kimaisha, tena wasipokuwa makini wanaweza ishia kulala stend...
Hiyo Ina apply kwa family zinazojiweza kwa watu wa kipato Cha chini ni Bora Kila mtu afe na hamsini zake sababu hiyo nyumba inaweza kuwa mwanzo wa matatizo ya kupigana juju ukizingatia ni watoto wanne
 
Huyo marehemu alikuwa na kiona mbali kilichofanya autabiri mustakabali huo.

Usia huo una mantiki na unastahili kuheshimiwa na kuzingatiwa.

Kwanza haujatueleza hao warithi ni wangapi, nyumba alizozuia marehemu kuuzwa ni ngapi, je kimantiki kama ni nyumba moja 'used' ikiuzwa yaweza kuleta impact za kuwatoa wanufaika kimaisha?
Huo mhemko wa kuuza vitu vya urithi hasa nyumba ya makazi hupelekea wengi kuwa homeless baada ya kuuza na kulamba hizo pesa.

Kwa nini watu wazima akili zenu mziorient kuuza nyumba iliyokatazwa, hamna pengine pa kushika, mmekwama wapi?

Mkiuza na kugawana mnauhakika mtapata seed money za kufanya miradi ya maana itakayosimama maishani mwenu?

Acheni kuwaza kifukara, heshimuni usia wa marehemu na mkiukiuka muelewe kuwa laana zipo na zinafanya kazi.
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Kajifunze kenya nimekupa mfano kwa nini wenye ardhi na nyumba zao wanaitwa landlord
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya

1 WAFALME 21​

Shamba La Mizabibu La Nabothi
1 Baada ya hayo, Nabothi, Myezreeli, alikuwa na shamba la mizabibu jirani na jumba la kifalme la Ahabu mfalme wa Samaria. 2Ahabu akamwambia Nabothi, “Nipe shamba lako la mizabibu nilitumie kwa bustani ya mboga, kwa kuwa liko karibu na jumba langu la kifalme. Badala yake, nitakupa shamba jingine la mizabibu zuri zaidi au, kama utapenda fedha, nitakulipa kiasi chochote unachoona ni thamani yake.”
3 Lakini Nabothi akamjibu, “Bwana na apishe mbali kukupa wewe urithi wa baba zangu.”
4 Basi Ahabu akaenda nyumbani, mwenye huzuni na hasira kwa sababu ya yale ambayo Nabothi, Myezreeli, alikuwa amesema, “Sitakupa urithi wa baba zangu.” Akajinyoosha juu ya kitanda akisononeka, na akakataa kula.
 
Back
Top Bottom