Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Inakuwaje kuuza nyumba ya urithi ukawa ubogus Kila mtoto alishakuwa mtu mzima na kwa bahati mbaya mambo yao hayajawaendea vizuri wanatafuta mitaji na kuuza nyumba ni the only way ya kuwa na mtaji ambao utakuwa hauna presha ya marejesho ambapo kwa malengo baadae wanaweza kuchanga na kujenga nyumba Tena kwa ajili ya familia nzima
Wewe Baba wewe; Unasema kila mtoto alishakuwa mtu mzima ila mambo hayajawaendea vizuri eti wanatafuta mtaji kwa kukiuka Agizo la marehemu? Tena unasema huo ni Mtaji ambao hauna presha ya marejesho!!!
Na unahitimisha kwa kuweka matumaini kwamba baadaye???? wanaweza kujenga nyumba kwa kuchangishana.......
Naomba uwe makini kwani:
1. Nyumba ikiuzwa manake kiwanja(Ardhi) imeuzwa. Hiyo "baadaye" matajenga wapi? Elewa iwe iwavyo, hamtakaa kamwe (milele)muweze kupata hapo mlipopauza.i.e. eg. Kitalu Na. xy kilichopo eneo D nyumba Na. Mtapata huko kwingine ila sio hapo alipokataza marehemu.
2. Je, kama Trend ya mambo kutokuenda vizuri ikawa ni endelevu na kutamalaki kwenu mtakimbilia kurudi wapi baada ya kupigika huko mtakakokwenda kuitapanya fedha ya mgawo mliyopata?? Kuna mdau hapo juu kasema mtaishia stendi.
3. Mkiuza nyumba na kila mmoja kupata mgawo stahiki; kila mmoja wenu atashika njia yake. Mtachangishanaje wakati mmeshatawanyika kila mtu na lake? Je, itakuwaje endapo mmoja kati yenu atakuwa katangulia mbele ya haki?
4. Uzoefu unaonesha kwamba Tamko la Marehemu mara nyingi huwa ndo Fainal. Kuzembea na kutotii kauli ya mwenye mali hata kama ni marehemu kunaleta usumbufu sana na wakati mwingine madhara. Marehemu alikufa kimwili lakini kiroho yupo.(Hiyo ni kwa wenye Imani lakini)
5. Kwa sasa hivi unasema kuuza nyumba ndo the only way ya kupata Mtaji.
Hiyo kauli mara nyingi huwa ni kihalalishio tu ili kufikia lengo la kupata fedha.
Baada ya kuzipata fedha inakuja "ponda mali kufa kwaja"
 
Unauza nyumba ili upate mtaji , uuze ardhi mjini kisa hela?? Mbona msiende benki mchukue mkopo miunue ghorofa na malipo muelewane na benki kuwa kodi mtagawana 70%-30%.
Mortgage ya 20 years mkila kila mtu asilimia kidogo ila by 50 years mtakuwa mwapata donge vizuri ( hapa nassume mpo in your 30's kwa kuwa umesema mwatafuta maisha.)
Usiuze ardhi ambayo mwendazake keshasema isiuzwe, mtajipata pabaya mbeleni. Akisema vile alikuwa na sababu kuu
 
Kuna watu Hadi karne hi wanafikilia mali ya urithi seriously 😳🙆🏻‍♂️

Waheshimu tamko la mwenye mali wakifanya kinyume hata iyo Pesa haiwezi kua na baraka na watokosa hata pa kuishi

Mali ya urithi ina kua na baraka kama mwenye mali akagawanya mali yake mwenyewe wakati akiwa hai kwa moyo wake wote aonavyo ni sawa lakini mali ya urithi ambayo MTU ameshakufa hakuacha mirathi yoyote ya maneno au maandishi then watu wanaanza kujigawanyisha kwa utashi wao hi kitu huwa haina faida na mwisho wake huwa mbaya Sana

Nna bamkubwa zangu wawili walitangulia mbele za haki na walikua na mali watu waakagawana lakini sasahivii hamna kitu chochote kilichobakia

Sio kila Mali ya urithi ina faa kujikwamua kiuchumi
 
Alikataa enzi za uhai wake hata kama akitangulia
IUZE , KWA KUZINGATIA YA KWAMBA UNAMNUNULIA MAREHEMU NYUMBA KWANZA, KIASI KINACHOBAKIA GAWANENI HAKUNA SHIDA YOYOTE, USISAHAU HILI, HAPO KWENYE NYUMBA YA MZEE ILIPO, CHUKUWA JIWE NA UDONGO KARAI MOJA, NENDA KAUWEKE KWENYE MAKAZI MPYA!, FANYA HIVI MTABAKI SALAMA.
N. B, KUMBUKA ASSET, INAKWENDA KWA ASSET,.
EXPRIENCED EXPERT!, FEDHA YA ASSET ZA NAMNA HIYO HUWA HAZIFANYI BIASHARA, KAMWE ZINGATIA HILI. BabaMorgan
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Wee ni kijana wa Hovyoo! Mzazi mwenye Hekima huacha urithi Kwa Wana wa wanawe.Mali za wajukuu na vijukuu hizo,tafuta zako
 
Back
Top Bottom