Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Hii kila mtu afe na chake imeangamiza familia nyingi sana, na sio mpango bora, fanyeni kampuni za asset na mali zisizohamishika!, na kila memba kuwa na nyumba bora inakuwa ndiyo msingi mkuu!
Sasa mkuu mpo watano. Mkiuza nyumba mnapata milioni 200. Mkiiacha watakaa ndugu au mtapangisha kwa 500K max kwa mwezi, maana nyumba yenyewe ya zamani. Si bora mgawane milioni 40 kila mmoja kuliko hiyo laki laki ya mwezi. Hiyo laki itakuwa mwanzo wa kuangamizana.
 
Unadhani wajukuu zako watakuwa wangapi?
Wataelewana?
Kwa kawaida mali hasa nyumba za urithi ni changamoto sana. huwa zinaleta mpasuko kwa ndg kufikia hadi kuuwana
Ni bora wauze
Wenzetu wahindi katika mazazi yao, huzingatia koo fulani zenye ujirani na familia, lakini dada zetu hawa wa leo wanazaliana hovyo na makabila mengine ya ajabu ajabu na kuzaa vitoto vyenye tabia za ajabu ajabu ni shida sana.
 
Sasa mkuu mpo watano. Mkiuza nyumba mnapata milioni 200. Mkiiacha watakaa ndugu au mtapangisha kwa 500K max kwa mwezi, maana nyumba yenyewe ya zamani. Si bora mgawane milioni 40 kila mmoja kuliko hiyo laki laki ya mwezi. Hiyo laki itakuwa mwanzo wa kuangamizana.
Tunachokwepa baadhi ya wanafamilia wataharibu fedha na baadae kuanza kulalama ovyo!
 
Hiyo Ina apply kwa family zinazojiweza kwa watu wa kipato Cha chini ni Bora Kila mtu afe na hamsini zake sababu hiyo nyumba inaweza kuwa mwanzo wa matatizo ya kupigana juju ukizingatia ni watoto wanne
Dah umasikini n mbaya sana aisee
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Kama alikataa isiuzwe ni heri kuipangisha
 
Hiyo pesa watakayopata itayeyuka na hawatajua imeishaje..wosia wa marehem uheshimiwe kuepuka kadhia
 
Sasa mkuu mpo watano. Mkiuza nyumba mnapata milioni 200. Mkiiacha watakaa ndugu au mtapangisha kwa 500K max kwa mwezi, maana nyumba yenyewe ya zamani. Si bora mgawane milioni 40 kila mmoja kuliko hiyo laki laki ya mwezi. Hiyo laki itakuwa mwanzo wa kuangamizana.
Marehemu anaposema msiuze mara nyingi nia ni kuwe na kitu cha kuwaunganisha. Muwe na kwenu ambapo wajukuu watafika na kukaa pamoja kuwakumbusha kuwa nyinyi ni kitu kimoja.
Kuna ambao nyumbani kila mmoja lazima awe na mti wake ambao anauhudumia na kaupa jina lake, hii inasaidia wakiwa watu wazima wakija kutazama yale mazingira wanaona kuuza pale ni sawa na kuuza historia yao. Kila mwaka wanakutana wote mara moja na kusali na kula pamoja wakiwa na watoto wao ambao nao hurithishwa eneo kama mali ya familia.

Kama ni kuuza Vitukuu au vilembwe ndo waje kuuza pakiwa na thamani ya juu mno.
 
Nyie ndiyo mnakaa bila kujishughulisha huku mkiwaombea wazazi wafariki waachie urithi. Mimi mitoto ya namna hii huwa inanikera sana. Tena usikute mwenye nyumba alikufa kwa kukosa huduma lakini bado hakutaka jasho lake ambalo ni nyumba yake iuzwe ili atibiwe. Halafu anatokea mtoto tena mwenye akili timam na nguvu anapiga dua usiku na mchana ili mzazi wake afe ili auze nyumba apate mtaji. Huyo atakuwa siyo mtoto halali wa marehem bali mtoto haramu.

Hashimu wosia, otherwise hata mkiuza km yeye alikataa hizo pesa mtamalizia kwenye pombe na Malaya tu.
 
Back
Top Bottom