Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Marehemu angekuwa na roho mbaya asingekuachia urithi. Tatizo ni njaa zako tu na huenda marehemu anajua huwa unaongozwa na njaa hivyo akaacha wosia.

Ukishaongozwa na njaa kufanya maamuzi ni mara chache sana ukafanya kitu cha maana, utauza na pesa zitapotea sababu maamuzi yanatoka tumboni. Ndo ile unasikia marehemu kafa na mali zinamfata.
Kama kweli hana roho mbaya basi anipe mali na kuniacha nizile kwa uhuru. Si anipe kwa shingo upande sababu ameshindwa kwenda nazo kaburini.

Kuwaambia watu wasiuze mali yako ukifa ni kilele cha roho mbaya.
 
Unadhani familia zenye watu wanaojielewa huwa wanakutana na hili tatizo? Mzee anaacha urithi kwa amani anajua watoto ni smart, watakachoamua ni kwa manufaa yao na watakaofata.

Ukishaona urithi unakuja na makatazo ya usiuze ujue mzee anawasiwasi na upeo wa mtoto au watoto, anajua kuna shida kwenye ubongo hivyo anajaribu kuwasaidia hata akiwa kaburini maana anajua akiwaacha ni suala la muda mtakuwa omba omba maana wenye akili hategemei mali za mzazi tu.
 
Hajaribu kusaidia. Ameacha kuwasaidia toka mnazaliwa hadi mnakuwa ndiyo awasaidie akiwa kaburini. Ni ucontrol freak na ukatili wa kupitiliza.
 
Dadeki, MUNGU aniepushe na mitoto isiyo na akili. Yaani nikukuze ukue, urithi nikupe halafu uniite freak? Dadeki.

KINA MAMA TUONEENI HURUMA WANAUME, MNAVYOKAA NAO HAWA HUWA MNAWAAMBIAGA NINI HAWA WATOTO?
 
Mwenye mali ameshafariki kwanini zisiuzwe ili kila mmoja apate haki yake

Mnataka kutengeneza urithi ndani ya urithi
 
Kuna wosia unasema.

"Iwapo mtoto yoyote kati ya watoto wangu wa nne ana uhitaji wa kuishi katika nyumba basi akae au wakae bila kusumbuliwa na yoyote, ila kinyume na hapo nyumba ipewe msikiti kwa ajili ya shughuli za ibada"

Hapa urithi ni endapo tu hamna nia ya kuuza, mkitaka kuuza tu mashekhe hawa hapa.
 
Sasa hapo mzee kaacha wosia ambao kisheria unatambulika na hakuna wa kupinga endapo umefuata taratibu zote za kisheria
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ila kwa Mali ambayo haikuachwa maagizo yeyote ya kisheria inauzwa tu bila wasiwasi
Upo salama kisheria, ila kama mhusika alikupa maagizo kabla ya umauti unakuwa msaliti wa marehemu.
 
Dadeki, MUNGU aniepushe na mitoto isiyo na akili. Yaani nikukuze ukue, urithi nikupe halafu uniite freak? Dadeki.

KINA MAMA TUONEENI HURUMA WANAUME, MNAVYOKAA NAO HAWA HUWA MNAWAAMBIAGA NINI HAWA WATOTO?
Sasa kama unataka kucontrol walio hai ukiwa kaburini kwa nini usiitwe control freak?
 
Upo salama kisheria, ila kama mhusika alikupa maagizo kabla ya umauti unakuwa msaliti wa marehemu.
Hapana mtu akishafariki hana lake kwenye Mali maana yake pia hawezi kuwaongoza walio hai labda uwe na imani za kishetani ila hapo hakuna usaliti
 
Mbona mwenyewe alipokuwa na matatizo hakuiuza.?

Punguzeni uvivu.
 
Wosia huo lazima uendane na sheria na utende haki. Ndiyo maana unapingwa mahakamani.
Kwenye kutenda haki hapo Nina mashaka kama wosia ukisema Mali za marehemu zipewe aidha taasisi fulani na sio watoto...je hapa wosia utapingwaje?
 
Marehemu anaposema msiuze mara nyingi nia ni kuwe na kitu cha kuwaunganisha. Muwe na kwenu ambapo wajukuu watafika na kukaa pamoja kuwakumbusha kuwa nyinyi ni kitu kimoja.
Kuna ambao nyumbani kila mmoja lazima awe na mti wake ambao anauhudumia na kaupa jina lake, hii inasaidia wakiwa watu wazima wakija kutazama yale mazingira wanaona kuuza pale ni sawa na kuuza historia yao. Kila mwaka wanakutana wote mara moja na kusali na kula pamoja wakiwa na watoto wao ambao nao hurithishwa eneo kama mali ya familia.

Kama ni kuuza Vitukuu au vilembwe ndo waje kuuza pakiwa na thamani ya juu mno.
Zipo nyumba kariakoo zinashindikana kuuzika, reason ni koo imezaliana na kuwa na idadi ya watu ya kutisha, unakuta familia ina watu 150, hao waliowaachia watoto nao walirithi.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom