Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Kama kweli hana roho mbaya basi anipe mali na kuniacha nizile kwa uhuru. Si anipe kwa shingo upande sababu ameshindwa kwenda nazo kaburini.

Kuwaambia watu wasiuze mali yako ukifa ni kilele cha roho mbaya.
Kama mwenye nyumba alikataa kwanini mnauza? Kama mnataka kuuza Jengeni yenu
 
Hapo hakuna uvivu...
Mbona mwenyewe alipokuwa na matatizo hakuiuza.?

Punguzeni uvivu.

Shida inakuja pale ambapo Mali sasa inamilikiwa na wengi kwahyo suluhu ya hapo ni kuuza kwa sababu kuigawa nyumba kwa wengi haiwezekani...hapo hakuna suala la uvivu
 
Uzeni kama mna uhakika wakati anakataza alikua ana tania hakua serious.
 
Alikataa enzi za uhai wake hata kama akitangulia
Watoto watafute chao aisee km mpaka sasa hawajielewi hiyo hela haitasaidia chochote zaidi ya laana tu.
Km baba kakataa isiuzwe aliwaona mikosi tu.
Usikute walianza kuuliza urithi akiwa hai
 
Kwenye kutenda haki hapo Nina mashaka kama wosia ukisema Mali za marehemu zipewe aidha taasisi fulani na sio watoto...je hapa wosia utapingwaje?
Mtu ana haki ya kumpa mali yake yeyote amtakaye. Kama akisema akifa mali yake ipewe taasisi fulani na akaweka hilo kisheria basi itapewa. Kama ni maneno tu bila nguvu ya kisheria au kuna utata wa kisherai wosia utapingwa.
 
Mtu ana haki ya kumpa mali yake yeyote amtakaye. Kama akisema akifa mali yake ipewe taasisi fulani na akaweka hilo kisheria basi itapewa. Kama ni maneno tu bila nguvu ya kisheria au kuna utata wa kisherai wosia utapingwa.
Naunga mkono hoja
 
hivi hamuwezi kuishi bila kugombania mali za urithi.? pbanieni vya kwenu. iacheni mali ya marehemu
 
Inauzwa tu. Unakuta warithi ni vichwa maji wana njaa kali au wana ugomvi wa kugombea mali wanaona bora wauze tu
Ikiwa alisema pasiuzwe mkauza inakula kwenu. Ila akitokea mwerevu akagoma kushiriki na wenzake wakaendelea basi waliopata mowanja lazima watakuwa mafukara wakati alie goma kula hela ya urithi atakuwa tajiri. That is how karima work. Tena inaenza enda mbali alie goma kula mkwanja akaja kinunua tena Kiwanja cha Mzee wake.
Baba yake Obama alifanyiwa fitina asishike nafasi ktk Taifa la Kenya ila Mungu akamlipizia mtoto akawa Rais wataifa kubwa Duniani akarudi ktk Taifa lake nakumuheshimisha baba yake.
 
Urithi either kwa kuandika au kwamaneno pasipo andika nimuhimu sana kufuwata nje ya hapo mnaweza angamia kizazi kizima
 
Hakuna ubaya wowote kuuza Mali ya urithi ikiwa ni Kwa nia nzuri kama kujiendeleza ki uchumi Kwa kuwa ulicho rithi siyo Mali ya marehemu Tena, ni Mali yako na warithi wako walio hai. Lakini Kumbuka na wewe siku Moja utahitaji kurithisha wanao na utakufa vile vile.
 
Umenikumbusha mbali sana mkubwa. Kuna mshua mmoja alikuwa jirani yetu yeye aliacha usia nyumba zote zinaweza kuuzwa ila kuna moja alisema isiuzwe wala isipangishwe.
Nyumba ile vijana wakaipiga bei, basi unaambiwa kila anaekaaga pale anadedi toka imeuzwa. Mwingine akipanga pale hamalizi mwezi anasepa akikomaa anadedi.
Nyumba iyo ipo Sumbawanga mitaa ya Majengo.
 
Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Kwahyo mnataka kuuza ili muwe maskini wa kupanga au?
 
Hapana mtu akishafariki hana lake kwenye Mali maana yake pia hawezi kuwaongoza walio hai labda uwe na imani za kishetani ila hapo hakuna usaliti
Umesamsaliti marehemu. Ni sawa tu na mtu akakuachia pesa upeleke nyumbani kwake halafu akafa kisha ukaila. Hakuna sheria ya kukuhukumu ila unabaki kuwa msaliti.
 
Zipo nyumba kariakoo zinashindikana kuuzika, reason ni koo imezaliana na kuwa na idadi ya watu ya kutisha, unakuta familia ina watu 150, hao waliowaachia watoto nao walirithi.
Thamani ya hiyo nyumba hapo kariakoo?
 
Alikataa enzi za uhai wake hata kama akitangulia
Isiuzwe,kwani iyo nyumba isingekuwepo wangeishije sema saivi mind zao ziko stagnant,zime stuck hapo kwa hapo nyumba iiuzwe. Wapangishe wale Kodi kwa zamu ama iwe inagawiwa kwa wote equal ratio
 
Back
Top Bottom