Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Kuna ubaya kuuza nyumba ya urithi ili hali marehemu enzi za uhai wake alikataa

Wenye experience na mali za urithi tunaomba uzoefu wenu kwa vile watoto wa marehemu hali zao za kimaisha sio nzuri wanahitaji kujikwamua kiuchumi je wakiuza nyumba na Kila mtu akichukua stahiki yake ili kujiendeleza Kuna ubaya
Sijawahi ona mtu aliweza nyumba,shamba au kiwanja amepiga hatua. Mara nyingi wanarudi nyuma baada ya kufanya hivyo hata kama hilo mali ni ya kwao na sio ,a kurithi.
 
WAFU hawajui lolote wala hawana sehemu katika yale yafanyikayo chini ya Jua.

“Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao. ”
— Ayubu 14:21 (Biblia Takatifu)
 
Kujikwamua kiuchumi kwa kupitia mali isiyo yenu?
 
Unadhani wajukuu zako watakuwa wangapi?
Wataelewana?
Kwa kawaida mali hasa nyumba za urithi ni changamoto sana. huwa zinaleta mpasuko kwa ndg kufikia hadi kuuwana
Ni bora wauze
Ni imani potofu tuu na pia wahusika kutoacha wosia vizuri. Babu yangu aliwaacha watoto wake 5 wanaume 3 akiwemo baba yangu mzazi, na wa kike 2. Wakati anakaribia kufariki aliwaita watoto wake wote na kuwapa wosia, ikiwemo kutouza mashamba yake, mifugo yake nk...mpaka hii leo mashamba yapo baba zetu walitasimamia na sisi watoto tumeyaendeleza na yapo mpaka leo ambapo kukodisha ekari moja kwa msimu ni laki 4 kulima mpunga. Wengine kwa kulima au kukodisha hayo mashamba ya familia tumeweza kununua mashamba yetu. Cha msingi ni usimamizi imara na kuzingatia wosia wa wazee wetu waliotangulia mbele ya haki.
 
Marehemu anaposema msiuze mara nyingi nia ni kuwe na kitu cha kuwaunganisha. Muwe na kwenu ambapo wajukuu watafika na kukaa pamoja kuwakumbusha kuwa nyinyi ni kitu kimoja.
Kuna ambao nyumbani kila mmoja lazima awe na mti wake ambao anauhudumia na kaupa jina lake, hii inasaidia wakiwa watu wazima wakija kutazama yale mazingira wanaona kuuza pale ni sawa na kuuza historia yao. Kila mwaka wanakutana wote mara moja na kusali na kula pamoja wakiwa na watoto wao ambao nao hurithishwa eneo kama mali ya familia.

Kama ni kuuza Vitukuu au vilembwe ndo waje kuuza pakiwa na thamani ya juu mno.
Sentimental values tu!!? Kwanza marehemu mambo ya walio hai yanamhusu nini?
 
Sentimental values tu!!? Kwanza marehemu mambo ya walio hai yanamhusu nini?
Yanamuhusu sana tu sababu aliacha urithi na maagizo. Hiyo nyumba marehemu angeiuza kusingekuwa na mjadala. Unless uniambie kila mtu kabla hajafa auze kila kitu ili mambo ya urithi yasiwepo, ukiondoka matamanio yako yaondoke na wewe.
 
Yeye aliondoka na kuachia watu nyumba. Watakachoifanya akiwa amekufa hayamhusu, ilimradi tu hawavunji sheria. Hata mahakama haijali wosia wa marehemu anayetaka kuendesha mambo akiwa ameshakufa.

Unaweza andika wosia kwamba ukifa mali yako mrithi awe nani au wawe nani, ukishafanya hivyo huna haki ya kuwapangia cha kuifanyia ukiwa umeishakufa. Kwanza hiyo ni roho mbaya, umekufa lakini bado unataka kucontrol mambo ya walio hai.
 
Yeye aliondoka na kuachia watu nyumba. Watakachoifanya akiwa amekufa hayamhusu, ilimradi tu hawavunji sheria.
Si suala la sheria, ni suala la kusudi. Kabla hujafa na ni nani unamwachia alinde kusudi lako?
Hata mahakama haijali wosia wa marehemu anayetaka kuendesha mambo akiwa ameshakufa.
Marehemu halindwi na mahakama, analindwa na mrithi ndo maana anaacha urithi kwa anayeamini kuwa atalinda alichokusudia mpaka pale atakaposalitiwa.
Unaweza andika wosia kwamba ukifa mali yako mrithi awe nani au wawe nani, ukishafanya hivyo huna haki ya kuwapangia cha kuifanyia ukiwa umeishakufa.
Angekuwa na roho mbaya asingeandika urithi angeuza yeye, wewe unayeachiwa na hutaki wanaofata wanufaike unataka uile ndo mwenye roho mbaya.
 
Yeye aliondoka na kuachia watu nyumba. Watakachoifanya akiwa amekufa hayamhusu, ilimradi tu hawavunji sheria. Hata mahakama haijali wosia wa marehemu anayetaka kuendesha mambo akiwa ameshakufa.

Unaweza andika wosia kwamba ukifa mali yako mrithi awe nani au wawe nani, ukishafanya hivyo huna haki ya kuwapangia cha kuifanyia ukiwa umeishakufa. Kwanza hiyo ni roho mbaya, umekufa lakini bado unataka kucontrol mambo ya walio hai.
Fuatilia mkasa wa gorofa la kariakoo utajua sheria inasemaje

Yule mzee kasema floor ya juu ya gorofa iwe wakfu na iwekwe pale madrasa kwenye wosia wake halafu watoto wanaleta ujuaji uliza kilichowatokea
 
Si suala la sheria, ni suala la kusudi. Kabla hujafa na ni nani unamwachia alinde kusudi lako?

Marehemu halindwi na mahakama, analindwa na mrithi ndo maana anaacha urithi kwa anayeamini kuwa atalinda alichokusudia mpaka pale atakaposalitiwa.

Angekuwa na roho mbaya asingeandika urithi angeuza yeye, wewe unayeachiwa na hutaki wanaofata wanufaike unataka uile ndo mwenye roho mbaya.
Yote unayofanya lazima yasound kisheria. Kucontrol walio hai ukiwa umekufa haisound kisheria na batili. Na ni roho mbaya. Mtu aache kusonga mbele kiuchumi sababu ya "Kulinda" kusudi lako wewe uliyekufa!!?
 
Unasonga mbele kiuchumi kwa mali za marehemu? Za kwako zipo wapi? Mtu alipojenga nyumba yake kwamba akifa wajukuu watakaa na wewe unayeiuza nani ana roho mbaya?
 
Fuatilia mkasa wa gorofa la kariakoo utajua sheria inasemaje

Yule mzee kasema floor ya juu ya gorofa iwe wakfu na iwekwe pale madrasa kwenye wosia wake halafu watoto wanaleta ujuaji uliza kilichowatokea
Hakuna kilichowatokea. Wanagombania mali tu. Wangefaidika zaidi wakiuza na kugawana mali.
 
Sasa Marehemu na wewe nani ana roho mbaya? Wewe kwanini hutaki kutunza ukawapa wengine kama ulovyopewa?
Hiyo hiyo nyumba itatunzwa miaka mingapi!? Itatosha kuwaachia wajukuu. Tunauza tunajenga zingine za kuwaachia watoto wetu. Kuna watu wana roho mbaya na ulafi wa mali kiasi kwamba wanataka kuzicontrol hata wakiwa wamekufa.
 
Njaa tu ndo zinakuongoza hapo hakuna lingine. Marehemu kakabidhi kipande cha nyama kwa fisi. Kama kweli unauza ili utengeneze urithi mwingine sawa ila watu wenye njaa mara chache sana kutengeneza mali, wanatauza wajifanye wanafanya biashara na nyumba inapotelea huko.
 
Njaa tu ndo zinakuongoza hapo hakuna lingine. Marehemu kakabidhi kipande cha nyama kwa fisi.
Vyovyote, marehemu yeye hayamhusu. Kama anaroho mbaya asijifiche kwenye wosia uchwara. Auze mali zake zote na azile akiwa hai hapa hapa.
 
Vyovyote, marehemu yeye hayamhusu. Kama anaroho mbaya asijifiche kwenye wosia uchwara. Auze mali zake zote na azile akiwa hai hapa hapa.
Marehemu angekuwa na roho mbaya asingekuachia urithi. Tatizo ni njaa zako tu na huenda marehemu anajua huwa unaongozwa na njaa hivyo akaacha urithi na wosia angalau labda utauheshimu ili angalau ukulinde na njaa zako.

Ukishaongozwa na njaa kufanya maamuzi ni mara chache sana ukafanya kitu cha maana, utauza na pesa zitapotea sababu maamuzi yanatoka tumboni. Ndo ile unasikia marehemu kafa na mali zinamfata.

Haya mambo yapo kwenye jamii, mitoto ya marehemu inauza kila kitu inatapanya pesa mwishowe inaanza kumuabisha baba yao kwa kuomba omba hifadhi baada ya pesa kuisha.
 
Back
Top Bottom