Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Nakiri kabisa hii mada mwanzoni sikuielewa, ila baada ya habari za yohana na housegirl wake kuvuja ndio nkaielewa lengo lake
 
Wana MMU,
Salaam.

Japo mimi sii member active sana humu MMU, ila ni mfuatiliaji mzuri wa mada za MMU.

Kwenye what's app group fulani kuna mjadala kuhusu jamaa fulani kampenda mke wa mtu.

Watu wanajifanya kushangaa sana iweje mtu ampende mke wa mtu?. Wengine hadi wakafikia kumlaani huyu mpendaji kuwa kitendo cha kumpenda mke wa mtu, atalaaniwa!.

Hii ni thread ya swali hypothetical tuu na naliuliza very objectively, kuna ubaya gani mtu kumpenda mke wa mtu?.

What is Love?.
Kupenda is love, ni kitu kinachotokea naturally for a reason au inaweza kutokea tuu for no reason at all!. Sasa ikitokea tuu naturally, mtu kumpenda mke wa mtu mwingine, jee kuna ubaya gani?. NB. Naomba lets underline, kupenda, love na kutoka na mke wa mtu!, hapa nazungumzia ku penda, just imagine wewe ni mwanamke mke wa watu, halafu umependwa na mwanaume mwingine, jee wewe una kosa kupendwa?, kwani ni wewe ndio umemwambia huyo mwanamume, akupende?.

Hitimisho.
Wanawake, ni mama zetu, dada zetu na wake zetu, wengi wao wanaishi kwenye ndoa za mateso, hawapendwi, hawatimiziwi, hawatoshelezwi, sasa katika safari ya kuelekea kwenye usawa wa kijinsia, kama sisi wanaume tulivyo na uhuru wa kupenda mtu zaidi ya mmoja na isinekane ni jambo la ajabu, its high time, tuwape uhuru huo wa kupenda na kupendwa, mama zetu, dada zetu, na wake zetu.
Namalizia kwa swali hili la msingi, Japo "The Forbidden Fruits the Sweetest", na "Vifunikavyo Vyaliwa, Vyaachwa Vilo Wazi", Jee ikitokea mtu kumpenda mke wa mtu mwingine, jee kuna ubaya gani?.

Ila pia pamoja na yote, mwisho wa yote ni hukumu ya haki iitwayo karma, ambayo kila binadamu atahukumiwa kwa kadri ya wema wake!, unaweza kumpenda mke wa mtu kwa lengo la kumsaidia yeye na familia yake, ukapata baraka kwa usaidizi huo, na unaweza kumpenda mke wa mtu, kwa dhambi ya matamanio ya mwili tuu, na hivyo kumuangamiza mume wake na kuisambaratisha familia yake, japo kidunia unaweza kufanikiwa sana, lakini mwisho wa siku lazima karma itakuhusu!.

Muongozo wa kuujadili uzi huu:
Nasisitiza uzi huu ni hypothetical situation, hivyo nawaombeni sana, msiingize jina la mtu yoyote, na pia isiiamini sana taarifa za umbeya wa mitandaoni kuhusu wake za watu!.
Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa ...

Nawatakia Jumatano Njema.
Paskali
Rejea
Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 Asubuhi ...
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya ... - JamiiForums
Mkuu Pasco, Kisa cha General Uriah lazima ukiangalia katika mlengo wa Kifalsafa zaidi. Ni falsafa inayogusa Imani, Mapenzi, Uaminifu, Dhambi na Adhabu yake na mwisho ni Haki ya Mtu. Uriah kama kamanda wa vita wa mstari wa mbele alijitolea kufa kwa ajili ya Mfalme Daudi na hata Daudi alipogundua kwamba Beerisheba ni mjamzito alimwita nyumbani akifikiri atalala na mke ili "kuhalalisha" mimba ile lakini alikataa na akafia vitani. Mungu alikmwadhibu Mfalme Daudi kwamba yule mtoto aliyezaa na Mke wa Uriah alikufa lakini hakumnyang'anya ufalme.
Kwa mbali unaona kuwa Adhabu aliyopewa Mfalme Daudi ni "nyepesi". Kwa mbali pia unaona kama Uriah alitolewa sadaka na licha ya uzalendo wake haijaandikwa kama alizawadiwa cho chote. Hitimisho nafikiri hilo unalolisema inawezekana likatafsiriwa hivyo kwamba si vibaya kumpenda mke wa mtu kwani hapa tunaona kabisa aliyependa mke wa mtu "hakuadhibiwa" ipasavyo. Wanatheolojia mnaweza kunisahihisha!
 
Pasco huyu.....
Kuna mfalme anamtolea mfano hapa si bure ....ukijumlisha na hizi tetesi ipo namna.
Adhabu ya Daudi haikuwa nyepesi na alipitia malipizi kiasi kikubwa sana. Ila kwakuwa matarajio ya wanadamu labda wangependa kuona akivuliwa ufalme ...
Daudi hakutenda lililo jema hata aigwe.
 
kama fununu zinazodai kuwa yule mama wa akina bashite kuwa ana mimba ya mkuu wa kaya itakuwa ni ya kweli bhas huu uzi kaka mkubwa kauleta ili kuandaa watu kupokea taarifa kwa mikono miwili,,,,,,,,,,,,,,
 
Kuna kupenda na kutamani
Sehemu kubwa kwa sisi Wanaume ni kutamani.
Je unayempenda na hasa akiwa mke wa mtu naye anakupenda?
Ili umpate huyo mke wa mtu uliyempenda au kumtamani unatumia njia njia gani? Pesa, ushawishi au madaraka yako?
Power corrupts and absolute power corrupts absolutely
 
Ni kosa kubwa sana kulala na mke wa mfanya kazi wako. Ni mbaya zaidi mke huyo akiwa pia ni mjakazi wako
 
Tunasahau ya kuwa Daudi alikuwa mteule wa Mungu... na aliadhibiwa kwa dhambi ile...ila hulka ya binadamu ni kutenda dhambi....so nikirejea swali lako...kaka haliwezi kutosha popote......mke wa mtu unampenda na kumezea moyoni....ukitaka kubananishwa makalio endelea tuu kaka......
 
Amri ya Tisa
Usimtamani mwanamke asiye kua mke wako
Amri ya Kumi
Usitamani mali ya mtu mwingine
 
Back
Top Bottom