Kuna ubaya wowote mtu kumpenda mke wa mtu? Mbona Daudi alimpenda mke wa Uria na akabarikiwa?

Nakiri kabisa hii mada mwanzoni sikuielewa, ila baada ya habari za yohana na housegirl wake kuvuja ndio nkaielewa lengo lake
 
Mkuu Pasco, Kisa cha General Uriah lazima ukiangalia katika mlengo wa Kifalsafa zaidi. Ni falsafa inayogusa Imani, Mapenzi, Uaminifu, Dhambi na Adhabu yake na mwisho ni Haki ya Mtu. Uriah kama kamanda wa vita wa mstari wa mbele alijitolea kufa kwa ajili ya Mfalme Daudi na hata Daudi alipogundua kwamba Beerisheba ni mjamzito alimwita nyumbani akifikiri atalala na mke ili "kuhalalisha" mimba ile lakini alikataa na akafia vitani. Mungu alikmwadhibu Mfalme Daudi kwamba yule mtoto aliyezaa na Mke wa Uriah alikufa lakini hakumnyang'anya ufalme.
Kwa mbali unaona kuwa Adhabu aliyopewa Mfalme Daudi ni "nyepesi". Kwa mbali pia unaona kama Uriah alitolewa sadaka na licha ya uzalendo wake haijaandikwa kama alizawadiwa cho chote. Hitimisho nafikiri hilo unalolisema inawezekana likatafsiriwa hivyo kwamba si vibaya kumpenda mke wa mtu kwani hapa tunaona kabisa aliyependa mke wa mtu "hakuadhibiwa" ipasavyo. Wanatheolojia mnaweza kunisahihisha!
 

Pasco huyu.....
Kuna mfalme anamtolea mfano hapa si bure ....ukijumlisha na hizi tetesi ipo namna.
Adhabu ya Daudi haikuwa nyepesi na alipitia malipizi kiasi kikubwa sana. Ila kwakuwa matarajio ya wanadamu labda wangependa kuona akivuliwa ufalme ...
Daudi hakutenda lililo jema hata aigwe.
 
kama fununu zinazodai kuwa yule mama wa akina bashite kuwa ana mimba ya mkuu wa kaya itakuwa ni ya kweli bhas huu uzi kaka mkubwa kauleta ili kuandaa watu kupokea taarifa kwa mikono miwili,,,,,,,,,,,,,,
 
Kuna kupenda na kutamani
Sehemu kubwa kwa sisi Wanaume ni kutamani.
Je unayempenda na hasa akiwa mke wa mtu naye anakupenda?
Ili umpate huyo mke wa mtu uliyempenda au kumtamani unatumia njia njia gani? Pesa, ushawishi au madaraka yako?
Power corrupts and absolute power corrupts absolutely
 
Ni kosa kubwa sana kulala na mke wa mfanya kazi wako. Ni mbaya zaidi mke huyo akiwa pia ni mjakazi wako
 
Tunasahau ya kuwa Daudi alikuwa mteule wa Mungu... na aliadhibiwa kwa dhambi ile...ila hulka ya binadamu ni kutenda dhambi....so nikirejea swali lako...kaka haliwezi kutosha popote......mke wa mtu unampenda na kumezea moyoni....ukitaka kubananishwa makalio endelea tuu kaka......
 
Amri ya Tisa
Usimtamani mwanamke asiye kua mke wako
Amri ya Kumi
Usitamani mali ya mtu mwingine
 
@pakali hivi mke wa mkapa ndo yule wa mramba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…