Kuna ugumu gani wa kuacha unywaji wa Pombe?

kila nikijaribu kuacha moja ya ulevi huu kati ya hvi nashindwa..Punyeto, pombe, madawa ya kulevya, uasherati na betting.

Vitu hvi vitano ni hatari kwa kweli.

Yaani mpaka naingia kwenye ndoa mpaka naingia utu uzima najaribu kuacha lakin nashindwa.
 
HADI MADAWA UNABWIA ...? we jiandae kupelekewa moto tu hakuna namna ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ chochote kitu watu watapita nacho soon
 
Wewe njoo twende kawe tu kwa nabii, una tatizo kubwa๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Nimesema moja kati ya vitu hvyo na si vyote, nimeshindwa kuweka wazi ila kipo miongoni mwa hvyo.
 
Ukiamua kuacha pombe una ACHA vizuri TU. Mwaka WA nne huu tangu niachane nazo
 
kila nikijaribu kuacha moja ya ulevi huu kati ya hvi nashindwa..Punyeto, pombe, madawa ya kulevya, uasherati na betting.

Vitu hvi vitano ni hatari kwa kweli.

Yaani mpaka naingia kwenye ndoa mpaka naingia utu uzima najaribu kuacha lakin nashindwa.
uchawi upo, we si ndio umetoa ushauri mbovu wa kuacha pombe???
 
na wewe ni mtumiaji wa vimiminika vyenye kileo ndani yake

"Msiwape pombe wafalme watasahau majukumu yao, bali wapeni pombe masiki wanywe wasahau shida zao"

Mkuu nisinywe afu niteseke? muda wote nikae nakumbuka shida zangu? Kweli hata we unaona sawa??๐Ÿ˜น
 
"Msiwape pombe wafalme watasahau majukumu yao, bali wapeni pombe masiki wanywe wasahau shida zao"

Mkuu nisinywe afu niteseke? muda wote nikae nakumbuka shida zangu? Kweli hata we unaona sawa??๐Ÿ˜น
ukishalewa na shida ndio zinakwisha ni mujiza gani huu wallah

nikiwaita walevi ni wapumbavu nakosea
 
Ni suala la mtu binafsi. Na hata ugumu unatofautiana kati ya mtu na mtu.

Binafsi huwa nakaa mpaka miaka miwili bila kunywa pombe.

Mwaka huu mara ya mwisho nimekunywa glasi moja ya Champagne January 1 2024 kusheherekea mwaka mpya, hapo ndipo ilikiwa mara ya mwisho kunywa pombe.

Niliamua kuacha tu bila tatizo lolote, kwa sababu nilitaka tu.
 
๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑMlevi aliyekuwa addicted na pombe Hana tofauti kabisa na Teja la madawa ya kulevya

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Ndugu yako akiingia kwenye sakata hili familia nzima inaumia, hakuna tofauti na ndugu yako kuwa kichaa na kuzurura uchi mjini

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Wapo waliokuwa ma genius darasani Sasa hivi ni Wenda wazimu kwa ajili ya pombe,

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Wapo waliokuwa Matajiri Pesa na mipango ya Pesa inasambaratika

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Idadi ya vijana wanaofanyiwa dialysis kwa kuua figo kwa sababu ya pombe Kali imeongezeka maradufu

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Ujio wa hizi pombe Kali ambazo zamani ziliitwa viroba na Sasa zinauziwa kwenye vichupa inamaliza vijana. Serikali isipoingilia kati wapiga kura wake watapukutika

๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ Bora zamani watu walikuwa wanakunjwa mataputapu na gongo lakini kwa haya ma pombe ya vichupa ya Sasa ni bomu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ