Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

kwasababu huo ni mlalo wa kifo! Kwahiyo kaizari mtoa roho uwa yuko around.
 
Hapo mwisho umeharibu! Ukiota ndoto nzuri ujue unakaribia kufa!? Umetudanganya...lol
 
Woote Mnaokabwa-kabwa hovyo usiku Mna PEPO, Mnahitaji Maombezi.:flame::A S wink:
 
Sijui nini kinanidrive nisilale chali, sijawahi kukutwa na huyo jinamizi, naskiaga tu kwa watu.
 
Ukilala kwa mgongo, Kuna uwezekano mkubwa wa ulimi wako kurudi nyuma na kublock njia ya hewa. Hii inakifanya upumue kwa shida. Ubongo wako iko kama processor ya computer na inaendeshwa kwa oxygen kama nishati. Hewa ikipungua kwenye ubongo unaanza kupata maruweruwe. Pozi zuri la kulala Ni kwa Tumbo na shingo ikae upande Ili njia ya hewa iwe wazi. Ukilala chali ukaota ndoto nzuri ujue unakaribia kufa (sitanii hehehe google 'euphoria')

Kwa kuongezea tu..hayo maruweruwe ni katika automatic functioning ya mwili ili ukistuka na ndoto ya kutisha unadilishe pozi la kulala..usife hehe
 
Ukilala kwa mgongo, Kuna uwezekano mkubwa wa ulimi wako kurudi nyuma na kublock njia ya hewa. Hii inakifanya upumue kwa shida. Ubongo wako iko kama processor ya computer na inaendeshwa kwa oxygen kama nishati. Hewa ikipungua kwenye ubongo unaanza kupata maruweruwe. Pozi zuri la kulala Ni kwa Tumbo na shingo ikae upande Ili njia ya hewa iwe wazi. Ukilala chali ukaota ndoto nzuri ujue unakaribia kufa (sitanii hehehe google 'euphoria')

Dah... Basi mie nimezoea kulalia tumbo mpaka nahisi kero sometimes. Nisipolalia tumbo usingizi hauji, afu hata kama nikilala vipi mwisho wa siku nitajikuta nishageuka na kulalia tumbo. Kuna wakati nilidhani kulalia sana tumbo kuna athari kiafya kumbe sio kweli.. Asante kwa kunifungua
 
Siwezi kulala kulalia tumbo. Lazima nilale kuelekea juu hapo usingizi utakua mtamu....
 
Kaka yaelekea una bonge la ndambi hahahaaaaa!! Maana hao ndo hawawezi kulalia tumbo na wakilala chali wanakoroma hao aibuuu....!

Mkuu natamani nikuekee picha yangu. Huo mlalo kuelekea chini kutafuta kuziba pumzi nani anakubali.....
 
Mkuu natamani nikuekee picha yangu. Huo mlalo kuelekea chini kutafuta kuziba pumzi nani anakubali.....

Kweli tumepishana!! Mie ndiyo mlalo wangu huo dakika tano nishapitiwa na usingizi mkali vibaya!!
 
Kweli tumepishana!! Mie ndiyo mlalo wangu huo dakika tano nishapitiwa na usingizi mkali vibaya!!

hata me nalalaga ivyo ila nikiangalia ukutani ndo balaa ndoto za ajabu ajabu mara nyoka mara jini oh!
 
hata me nalalaga ivyo ila nikiangalia ukutani ndo balaa ndoto za ajabu ajabu mara nyoka mara jini oh!

Heee....!! Hii mupya, ukilala umegeukia upande wa ukutani unaota ndoto za ajabu ajabu tena?? Mh! Hebu badilisha chumba pengine rangi ya ukuta inakuzingua. Na ukilala chali je??
 
Mara nyingi wanaopata ndoto za kutisha au kuhisi kukabwa wakiwa usingizini, ni matokeo ya mgandamizo wa nerves au wakati mwingine kunasababishwa na kushiba sana au kuvimbiwa.

Ulaji wa chakula kingi kabla ya kwenda kulala si mzuri, kwa sababu kunasababisha tumbo kukugasana na diaphragm, na hi upelekea mgandamizo kwenye mapafu na kusababisha kutoweza kupumua vizuri.

Hali hii inapotokea, ubongo unajaribu kutafuta au kutaka kujuwa nini tatizo ili kuweza kukupa taarifa au ufahamu wa kile kinachoendelea. Matokeo ni pale ubongo unaposhindwa kutafairi tatizo ndio ukuletea taarifa ambayo wewe unaiona kuwa kuna mtu au dubwana fulani linakukaba na ndoto zingine za kutisha.

Vilevile inaweza kuwa ni Paralysis, ambayo usababiswa kwa kuharibiwa kwa nervous system au mgandamizo mkubwa kwenye nervous wakati wa kulala, ushauri jaribu kutumia mto ambao si mgumu na kula chakula masaa mawili au matatu kabla ya kulala na chakula kiwe laini na usishibe sana kwa sababu itakusababishia mgandamizo kati ya tumbo na diaphragm na kupelekea kupata hayo mamtatizo.

Kabla ya kulala ni vema ukakoga maji ya uvuguvugu, hii usaidia nerves zako ku relax na kukupelekea kupata usingizi mzuri na unywaji wa maziwa ya moto kabla ya kulala, japo nusu saa kabla pia inasaidia kupata usingizi mzuri.

Ila kama tatizo ni kubwa ni bora kuonana na daktari ili kuweza kujuwa tatizo kwa undani zaidi.
 
Heee....!! Hii mupya, ukilala umegeukia upande wa ukutani unaota ndoto za ajabu ajabu tena?? Mh! Hebu badilisha chumba pengine rangi ya ukuta inakuzingua. Na ukilala chali je??

nikilala chali hakuna tatizo nikigeukia ukutani ni balaa sehemu yoyote nitakayokuwa!
 
Back
Top Bottom