Kuna ukweli biashara ya kubeba mizigo kwa kirikuu imeyumbishwa na maguta ya Kichina

Kuna ukweli biashara ya kubeba mizigo kwa kirikuu imeyumbishwa na maguta ya Kichina

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
1778101297010.png

1778101177847.png

Hapo zamani biashara hasa za hardware walikuwa wanatumia sana kirikuu kubeba cement, mabati, nono, n.k. lakini sikuhizi tunazidi kuona kasi ya maguta yakichukua nafasi hii

wafanyabiashara wanaoenda kununua vitu kama maduka makubwa nao hawachezi mbali wameanza kuyaelewa maguta

Pia kirikuu zilitumika sana kwenye wahamiaji wa vyumba na vyumba vya kupanga lakini sikuhizi utaona wahamaji wengi wakitumia maguta.

Yote haya ni kwa uzoefu wangu tu niliouona na kudhani kwamba maguta yanaweza yakawa ameharibu soko la kirikuu, je kuna ukweli.
 
Achana na ivyo, kuna vile vya umeme ndio kabisaaa.

Pia izo guta nimekuta watu wanahama kwa kutumia izo.

Man.
Vile vya umeme vinatumika zaidi kwenye delivery, lakini huku kwetu bado ni vichache na havijaenea sana.

Kwa upande wa wahamiaji, nao wameanza kuyakubali maguta, bajeti zimetaiti sana.
 
Kila biashara ina muda wake;
Longtime maskani, tulikuwa tunatumia hiace kutoka kijiji kimoja kwenda kingine, zikaja boda na bajaji. Barabara zikapigwa lami, Hiace zikabidi zitafute route ingine. Nani atasubiri ujaze abiria ndio muondoke.

Hiace zikapinduliwa na probox/mchomoko. Nenda Kigoma, hakuna mtu anapanda hiace.

Teksi zikapunduliwa na boda/uber/bajaji.

Mtu hawezi kukaa foleni kusubiri hiace ijae wakati kuna bajaji/boda na mchomoko.

Ushauri; wauze virikuu wanunue maguta! Mambo hubadirika.
 
Ni kweli kabisa, waki kazania hayo ma kirikuu, Yatawadodea kama jamaa wa Tax 😁
 
Kwanza mkae mkijua guta linauzwa galama ndogo kuliko kilikuu,guta inanguvu kuliko kilikuu na mtaji wakununua kilikuu used japan pamoja na tra,usafiri adi ifike mkonon mwako unapata maguta mawili mpya unayabikili mwenyewe na chenchi inabaki na mbaya zaid maguta yapiga tipa ambapo kilikuu haiwez mwisho nauli za kusafilisha mzigo kwa guta zinafanana au guta kua chini ivyo guta litavutia zaid wateja kuliko gar kilikuu
 
Hayo maguta yanabeba mzigo mkubwa kuliko kirikuu na gharama ya kununua ni ndogo kuliko kirikuu hata uendeshaji ni rahisi hivyo yana advantage kwenye kila angle.
 
Back
Top Bottom