SoC01 Kuna ukweli kuhusu Mungu?

SoC01 Kuna ukweli kuhusu Mungu?

Stories of Change - 2021 Competition

Mmakedonia

Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
21
Reaction score
12
Moja kati ya mijadala ambayo imezua ugomvi mkubwa duniani na kusababisha vifo kwa watu wengi ni katika suala zima la kuwepo au kuto kuwepo kwa Mungu mmoja.kila imani imejaribu kueleza kivyake kuhusu mtazamo wake juu ya suala la imani ya Mungu lakini katika mengi basi lazima lipo jawabu sahihi moja🤝

Kila mtu ukimuuliza kuhusu dini yake hatokuambia ukweli bali ataisifia na hawezi kukupa madhaifu ya dini yake sasa swali ninalojiuliza hivi kama kweli kuna Mungu mmoja kwanini hakuna dhehebu moja au dini moja iliyopata nguvu zaidi kiasi kwamba watu wote waiamini kwasababu dini zote zinasema Mungu ana nguvu kuliko shetani.

Nakumbuka kipindi nasoma madrasa katika Qur-an takatifu surat Ikh-rasu bila shaka aya ya kwanza inasema "kul hu allahu ahad" yaani kwa kiswahili "sema mwenyezi Mungu ni mmoja" pia kipindi nasoma maandiko ya biblia sana kuna mstari unasema "Mimi ndiye bwana Mungu wako, usisujudie miungu mingine" nikabaki na maswali ya kiimani kwamba kwanini inaonekana kuna Mungu mkubwa mmoja lakini watu wake hawapo katika njia moja ya kumtumikia.?

Sitaki kubadili mitazamo ya watu kuhusu njia zao za kumtumikia Mungu lakini najiuliza kwanini watu wametofautiana njia za kumtumikia lakini wote wanapata mahitajia yao katika imani zao sasa kinachowapa majawabu yao ni Mungu au ni imani zao?

Je ni kweli Mungu yupo mmoja swali ambalo limekosa majibu yenye ushahidi wa uhalisia kwetu, Je ni kweli kuna mauti ya milele ile inayosemwa katika biblia kwenye kitabu cha ufunuo na katika Qur-an "izzaa zul zilatil arudhi zil zaalaha" yaani "itakapotikisika dunia katika mtikisiko wake" sasa itakuaje kwa wale walio kufa kabla dini hazijafika Afrika?🤔
 
Upvote 1

Zab.53:1

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Ni hivi: MUNGU yupo, isipokuwa mifumo (dini na madhehebu) ya kumtafuta ndiyo ina maswali.
 
Mmakedonia,

More so, I wish I exposed you to the basics of the Doctrine of Israelology vs Egyptology for you to understand the subject.
 
Zab.53:1

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Ni hivi: MUNGU yupo, isipokuwa mifumo (dini na madhehebu) ya kumtafuta ndiyo ina maswali.
Ili usipotee... kwanza nikufungue toka kwenye kifungo cha wengi kwamba MUNGU hana dini wala dhehebu. MUNGU siyo Mkristo, siyo Muislam, siyo Mhindu, siyo M-budha, siyo Myahudi, siyo M-kurd, siyo M-bahai, siyo M-aramean, siyo M-armenia, siyo M-druze, siyo M-krishan, et al.

Ukitoka hatua hiyo sasa utatakiwa kuingia hatua nyingine ya kutafuta kujuwa sura ya MUNGU ni ipi?

MUNGU siyo mwanaume, siyo mwanamke, siyo mtoto, siyo mkubwa, siyo mweusi, siyo mzungu, siyo kilema, hana kabila. MUNGU NI ROHO. Kule Marekani kwenye Chapel ya Chuo Kikuu chenye heshima kubwa namba moja duniani cha Havard, MUNGU anatajwa kuwa ana nafsi nne (Baba, Mama, Mwana, Roho Mtakatifu). Unaona sasa upotofu wa mafundisho ya dhana na itikadi za madhehebu na dini! Usipotaja nafsi zote nne wanaharakati wa haki za wanawake (Feminists) wanakuburuza Mahakamani.

Wanajenga hoja kuwa hakuna MUNGU mwana bila MUNGU Baba na MUNGU Mama kuzaa pamoja.

Maswali magumu ninayowauliza hawa Wamarekani ni haya:
1. MUNGU Baba alioa lini?
2. MUNGU Baba alifunga ndoa na MUNGU mama anayeitwa nani? Binti wa nani? Kabila gani? Lini? Dini/Dhehebu lipi? Posa ilipelekwa wapi? Posa bei gani?
3. Sheikh yupi au Mchungaji yupi alifungisha ndoa ya MUNGU Baba na MUNGU Mama?

NB. Ndiyo Wamarekani hawa hawa wanaoichagiza dunia iridhie na kutambua haki za mashoga. Baghosha!

Count me out!
 
Fuatilia historia ya dunia hii na mambo ya ajabu yaliomo then uridi tena lasiivo hatuta elewana
 
Bado umeniacha na maswali mengi pia mkuu
 
Zab.53:1

Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Ni hivi: MUNGU yupo, isipokuwa mifumo (dini na madhehebu) ya kumtafuta ndiyo ina maswali.
Sasa kipi cha kufanya ili kujua mfumo ulio sahihi!?
 
Ni kuishi kwenye mfumo usio wa mapokeo. Ishi imani-halisi usiishi imani-nadharia, kwa sababu MUNGU siyo nadharia, MUNGU ni halisi. Tukimhusisha MUNGU kwenye nadharia basi tunamfanya kuwa siyo halisi, maana mojawapo ya tabia za msingi sana za nadharia ni kuwa siyo lazima itimie (siyo lazima nadharia iwe halisi).
 
Back
Top Bottom