Mmakedonia
Member
- Sep 1, 2021
- 21
- 12
Moja kati ya mijadala ambayo imezua ugomvi mkubwa duniani na kusababisha vifo kwa watu wengi ni katika suala zima la kuwepo au kuto kuwepo kwa Mungu mmoja.kila imani imejaribu kueleza kivyake kuhusu mtazamo wake juu ya suala la imani ya Mungu lakini katika mengi basi lazima lipo jawabu sahihi moja🤝
Kila mtu ukimuuliza kuhusu dini yake hatokuambia ukweli bali ataisifia na hawezi kukupa madhaifu ya dini yake sasa swali ninalojiuliza hivi kama kweli kuna Mungu mmoja kwanini hakuna dhehebu moja au dini moja iliyopata nguvu zaidi kiasi kwamba watu wote waiamini kwasababu dini zote zinasema Mungu ana nguvu kuliko shetani.
Nakumbuka kipindi nasoma madrasa katika Qur-an takatifu surat Ikh-rasu bila shaka aya ya kwanza inasema "kul hu allahu ahad" yaani kwa kiswahili "sema mwenyezi Mungu ni mmoja" pia kipindi nasoma maandiko ya biblia sana kuna mstari unasema "Mimi ndiye bwana Mungu wako, usisujudie miungu mingine" nikabaki na maswali ya kiimani kwamba kwanini inaonekana kuna Mungu mkubwa mmoja lakini watu wake hawapo katika njia moja ya kumtumikia.?
Sitaki kubadili mitazamo ya watu kuhusu njia zao za kumtumikia Mungu lakini najiuliza kwanini watu wametofautiana njia za kumtumikia lakini wote wanapata mahitajia yao katika imani zao sasa kinachowapa majawabu yao ni Mungu au ni imani zao?
Je ni kweli Mungu yupo mmoja swali ambalo limekosa majibu yenye ushahidi wa uhalisia kwetu, Je ni kweli kuna mauti ya milele ile inayosemwa katika biblia kwenye kitabu cha ufunuo na katika Qur-an "izzaa zul zilatil arudhi zil zaalaha" yaani "itakapotikisika dunia katika mtikisiko wake" sasa itakuaje kwa wale walio kufa kabla dini hazijafika Afrika?🤔

Upvote
1