Asante
Mwl Mwakujonga
na swali... Ni njia GANI unaweza kutumia kufafanua ndoto ya mafumbo.....
Mfano, kuna ndoto niliota ilinitisha sana... Kama ya Daniel chapter 7....
Ila mimi niliota tai mkubwa kama kimo cha nyumba za kawaida... Akaja kutua mbele yangu akanitazama kwa gadhabu sana... Halafu alikuwa ni tai mwili wote.. Ila kichwa cha binadamu halafu katikati anapembe ndogo na macho makubwa... Akanambia kwa sauti ya hasira au kuu huku amenitazama et "UTAWALA WA MUNGU UMEKWISHA, SASA NI UTAWALA WA SHETANI" ilikuwa saa 9:40 usiku nilipo shituka¡ na heartbeat ilikuwa imepanda sana...
Hapo nilikuwa na kama week mbili baada ya kubatizwa...
Kama ulivyosema ndoto yako inafanana na ile ya Daniel lakini kama alivyosema daniel aina ya mnyama ni aina ya utawala kama vile yule mtu wa
Daniel 7: 16 Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo.
17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.
Danieli 7:17
Kwa hiyo huyo tai ni aina ya mtawala ambaye anakujulisha kwamba kuna utawala ambao huko juu yako
Linganisha na habari ya Yesu pale alipomaliza kubatizwa pale mto wa yordani tunaona roho mtakatifu anashika kwa sura ya njiwa na sauti kutoka mbinguni ikiwa ni ishara ya utawala wa Mungu dunia kupitia Yesu Kristo
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; Mathayo 3:16
Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 4:17
Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; Mambo ya Walawi 11:13
Kwa hiyo kama tai ni miongoni mwa ndege ambao Mungu aliwakataa kuliwa kwamba ni machukizo, natubafahamu pia kibiblia mnyama amebeba picha ya roho ya utawala kwa hiyo kuna roho ya uhasi ambayo inawezekana huko nyuma wazazi wetu kizazi cha 3 au 4 kuingia katika maagano ya miungu ndio maana ulipopatizwa ndoto ilikuja ili kukumbusha kwamba kuna utawala ulionao kwanini unataka kuingia utawala mwingine wakati uko katika utawala mwingine?
Mambo ya kuzingatia
Unaweza kuongea na wazee wako kabla ya kuokoka kupata historia ya ukoo wenu?
Pili ingia kwenye maombi ya toba Zab 51, Maombelezo 5:7.
Kama unanena kwa lugha omba kwa kunena kwa lugha Mungu atakusadia
Tatu fanya kama alivyofanya Gidion kwa kutoa sadaka dhidi ya miungu ya baba yake Waamuzi 6:15_20
Nne omba uongozi wa roho mtakatifu
Nb usisahau kutumia Damu ya Yesu kuomba toba Mathayo 26:24 ,Waebrania 12:24
Omba Mungu akusaidie katika vita ambayo unapigana maana hiyo ni vita dhidi ya wakovu wako usiposhinda wokovu wako utakuwa na upizani sana katika maisha yako