Kuna umuhimu gani wa mtu kuota ndoto?

Kuna umuhimu gani wa mtu kuota ndoto?

Ahsante sana Mwl kwa somo la lango la ndoto. Nimeelewa vizuri sana Mungu akubariki.

Mimi ni kati ya wale wanaoota hata nikilala dakika moja tuu, iwe ni mchana au usiku.
Nina swali kuna kipindi nilitanga mbali kabisa lakini niliendelea kuota kila siku, hiyo inatokana na nini?
Na mimi hii kitu hua inatokea... ila mara moja moja hata week nzima ila ndoto tofauti iwe nimelala mchana au usiku wakati mwingine.... hata ukiamka kukojoa mchana ukirudi inaendelea palepale ilipoishia...
 
Na mimi hii kitu hua inatokea... ila mara moja moja hata week nzima ila ndoto tofauti iwe nimelala mchana au usiku wakati mwingine.... hata ukiamka kukojoa mchana ukirudi inaendelea palepale ilipoishia...
Mungu ana kazi na wewe, hizo ndoto za kujirudia na zenye kuendelea ulikoisjia huwa zina ujumbe unaotakiwa kufanyiwa kazi bila kupuuza.
 
Mungu ana kazi na wewe, hizo ndoto za kujirudia na zenye kuendelea ulikoisjia huwa zina ujumbe unaotakiwa kufanyiwa kazi bila kupuuza.
May be ila mimi... hata sinaga mda wa kuzifatilia kuna kipindi nilianzaga hadi kuandika kila siku, ila bahati mbaya kukumbuka asubuh ndo mtihani yani nimesha sahau nikaahirisha...
 
May be ila mimi... hata sinaga mda wa kuzifatilia kuna kipindi nilianzaga hadi kuandika kila siku, ila bahati mbaya kukumbuka asubuh ndo mtihani yani nimesha sahau nikaahirisha...
Jitahidi kupata utulivu mara tu uamkapo usijihimu kwenye distractions esp simu
 
Kwa nini mimi sioti ndoto?

Ni Maswali kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa hawapati ndoto ?

Kuna umuhimu gani wa mtu kuota ndoto?
Ndoto ni njia moja wapo ambayo Mungu au miungu wanaitumia kwa ajili ya kuzungumza na Mwanadamu Ayub 33:14_15

Kwa hiyo kama ndoto ni njia ambayo Mungu au miungu wanaitumia kwa ajili ya mawasiliano na mwanadamu maana yake kukosa ndoto ni kukosa mlango mmoja wa kuwasiliana na ulimwengu wa roho

Ndoto ni njia ya mawasiliano kati ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili

Hivyo basi mtu anapokosa kuota ndoto maana yake anakosa njia moja wapo ya kuwasiliana na ulimwengu wa roho

Sababu za kukosa ndoto
Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kuwa sababu ya mtu kukosa kuota ndoto na sababu hizo ni pamoja na :_

Sababu kubwa ya mtu kukosa ndoto ni sababu ambayo inatokana na umiliki wa shetani juu ya mlango wa ndoto wa mwanadamu

Ndoto ni mlango wa mawasiliano baini ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili , hivyo basi anayemiliki mlango ndiye anaye hamua nini kiingia na nini kisiingie

Shetani akipata uhalali juu ya mlango wa ndoto wa mwanadamu hata hakikisha ndoto zote za Mungu azimfikii mwanadamu ndio maana utakuta unakosa ndoto au kila ndoto nzuri utakayo hota haukumbuki

Kwanini shetani anazuia watu kuota ndoto, kwa sababu ndoto ni mlango na kama ni mlango wa kiroho kwa hiyo unaweza kutumiwa na Mungu au shetani ndio maana ikiwa shetani anaumiliki mlango wa ndoto hata uruhusu Mungu kuutumia kwa ajili ya kukusaidia

Faida ya kuota ndoto, ndoto ni njia moja wapo ya Mungu kiwasiliana na sisi, soma habari ya kuzaliwa kwa Yesu na ndoto za Yusufu na wale Mamajusi Mathayo 2:1-23

Nifanyeje ili niweze kuota ndoto, jambo la kwanza omba toba kwa Mungu juu ya jambo lolote ambalo limefungua mlango na shetani kupata uhalali juu ya lango la ndoto

Pili tumia Damu ya Yesu kuondo uhalali wa dhambi kutawala katika lango lako la ndoto Matayo 26:28

Tatu tumia Damu ya Yesu kuondoa uhalali wa sadaka zinazotoa uhalali wa shetani kumiliki lango lako la ndoto 1 Wakoritho 5:7

Nne funja kila madhabahu za shetani ambazo zimepata uhalali juu ya lango la ndoto

Tano kemea kila pepo linalotawala lango lako la ndoto

Sita ombea Ufalme wa Mungu kuja katika lango lako la ndoto ktk Kristo Yesu
Ni vizuri kupata habari kutoka ulimwengu wa roho.
 
Mi naomba kuliza kwa watalam wa ndoto

Ivi mtu umelala usiku ukaota ndoto flan ikakustusha au ikakuwazisha so ukashtuka usingizini uka kaa kitandani km dakika 2/5 zen ukalala cha ajabu ukajikuta unaota ndoto ile ile.

Yan inakua kama movie ume piga stop zen ukaruhusu play

Kwa ufupi unabakia kuota ndoto ile ile iliyokusababisha usituke usingizini

Hii huwa ina maana gan
 
Mi naomba kuliza kwa watalam wa ndoto

Ivi mtu umelala usiku ukaota ndoto flan ikakustusha au ikakuwazisha so ukashtuka usingizini uka kaa kitandani km dakika 2/5 zen ukalala cha ajabu ukajikuta unaota ndoto ile ile.

Yan inakua kama movie ume piga stop zen ukaruhusu play

Kwa ufupi unabakia kuota ndoto ile ile iliyokusababisha usituke usingizini

Hii huwa ina maana gan
Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto.

Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini.

Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto.

Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka.

Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema.

Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao.

Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu.

Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Mwanzo 41:1_8.

Ukipata muda soma Mwanza sura 41 nzima , kuna kitu utajifunza
Ndoto ambayo utaota na ukalala ikaendelea tena maana yake ndoto ni moja na ni muhimu kujua kuwa ndoto hiyo ina umuhimu kwako

Mfano Farao ameota ndoto mara baada ya kuota ndoto ya kwanza akaamka ina maana kuna mawazo yaliingia ndani yake juu ya ndoto hiyo akaamua kulala akidhani ni ndoto tu, tunaona ndoto hiyo hiyo ikajirudia kw namna tofauti

Kwanini unatakiwa kuifatili ndoto ya namna hiyo,

Kitu cha kwanza ndoto hiyo mara baada ya kuota moyoni mwako unaskia nini? Wengine mara baada ya kuota ndoto anaskia moyoni kama masononeko, uzuni, hali ya moyo kufa nk hii inakujulisha roho mtakatifu anataka uifanyie hiyo kazi

Kwanini Faraoa akiifanyia kazi ndoto hiyo?

Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Mwanzo 41:8

Kilichomfanya Farao kufatilia ndoto hiyo ni kule kufadhaika kwa moyo, kulimpa ishara kwamba ndoto hii ni muhimu kuifatilia

Mfano Farao hasingeifatilia ndoto hii dunia ya kipindi kile ingepata shida ya njaa kwa hiyo kiashiria moja wapo cha kufatilia ndoto ni hali ya moyo mara baada ya kuota ndoto umeamka asubuhi ndani yako unaskia nini.

Kuna watu wameota ndoto wanakimbizwa na majitu na wanapohamka wanajiskia moyo unapiga kwa kasi kama ni kweli walikuwa wanakimbizwa maana yake ndoto za namna hiyo sina uhalisi kwamba kitu kimetendeka katika ulimwengu wa roho kinatakiwa kufanyiwa kazi kabla madhara kutokea
 
Back
Top Bottom