Kuna umuhimu gani wa mtu kuota ndoto?

Kuna chumba nilikuwa nikilala nikiota ndoto ni 100% correct.
Kuna uhusiano mkubea wa ndoto na mahali ulipolala, kama umelala eneo ambalo kulikuwa kunafanyika ibada z miungu au Mungu utaota ndoto za miungu au Mungu kwa hiyo eneo linabeba roho ambayo inatumika kupotisha ndoto mfano soma habari za Yakobo na habari za Samweli

10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani.

11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.

12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.

13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.

16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
Mwanzo 28:11_17)6

Mahali ambapo Yakobo alilala ni mahali ambapo Babu yake Ibrahimu alijenga madhabau kwa kutoa sadaka kwa hiyo eneo unalo lala ni chanzo kikubwa cha ndoto hivyo tuwe makini na lodge tunazolala
 
Lakini ndoto ni mafumbo usipoweza kufumbua hilo fumbo utawezaje kuhusisha hiyo ndoto na kilichotokea kwa usahihi?
Mungu hawezi kukuwekea ndoto asikupe namna ya kupata maarifa , mwombe Mungu anaweza kukufunulia tafsri kwa neno lake au roho mtakatifu au kwa kutumia watu kama vile Farao alivyopewa Yusufu
 
Asante! mkuu ngoja nianze kufatilia....
 
Asante Mwl Mwakujonga
na swali... Ni njia GANI unaweza kutumia kufafanua ndoto ya mafumbo.....
Mfano, kuna ndoto niliota ilinitisha sana... Kama ya Daniel chapter 7....
Ila mimi niliota tai mkubwa kama kimo cha nyumba za kawaida... Akaja kutua mbele yangu akanitazama kwa gadhabu sana... Halafu alikuwa ni tai mwili wote.. Ila kichwa cha binadamu halafu katikati anapembe ndogo na macho makubwa... Akanambia kwa sauti ya hasira au kuu huku amenitazama et "UTAWALA WA MUNGU UMEKWISHA, SASA NI UTAWALA WA SHETANI" ilikuwa saa 9:40 usiku nilipo shituka¡ na heartbeat ilikuwa imepanda sana...
Hapo nilikuwa na kama week mbili baada ya kubatizwa...
 
Mungu hawezi kukuwekea ndoto asikupe namna ya kupata maarifa , mwombe Mungu anaweza kukufunulia tafsri kwa neno lake au roho mtakatifu au kwa kutumia watu kama vile Farao alivyopewa Yusufu
Hapo umeeleza kana kwamba nimeshajua kuwa ndoto imetoka kwa Mungu na si vinginevyo, maana ndoto hizi zengine chanzo kinaweza ni mawazo yetu ya kawaida sababu za kibaiolojia.
 
mtu kutoota au kutokumbuka ndoto hakumaanishi moja kwa moja kwamba amepoteza mawasiliano na Mungu au kwamba kuna nguvu za kiroho zimezuia ndoto zake. Ndani ya imani ya Kikristo, uhusiano wa mtu na Mungu haupimwi kwa ndoto pekee, bali pia kwa imani, maombi, kujifunza Maandiko, na uongozi wa Roho Mtakatifu.
 
You have a point maana hiyo nyumba ilikuwa kubwa nilikuwa peke yangu.

So nilikuwa nabadili vyumba vya kulala .

Kila nikilala hicho chumba nikiota ni 100 correct hakuna tofauti kwa lolote ; muhusika anakuwa yule yule na jambo linakuwa lile lile.
 
Kama ulivyosema ndoto yako inafanana na ile ya Daniel lakini kama alivyosema daniel aina ya mnyama ni aina ya utawala kama vile yule mtu wa

Daniel 7: 16 Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo.

17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.
Danieli 7:17
Kwa hiyo huyo tai ni aina ya mtawala ambaye anakujulisha kwamba kuna utawala ambao huko juu yako

Linganisha na habari ya Yesu pale alipomaliza kubatizwa pale mto wa yordani tunaona roho mtakatifu anashika kwa sura ya njiwa na sauti kutoka mbinguni ikiwa ni ishara ya utawala wa Mungu dunia kupitia Yesu Kristo

Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; Mathayo 3:16

Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 4:17

Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; Mambo ya Walawi 11:13

Kwa hiyo kama tai ni miongoni mwa ndege ambao Mungu aliwakataa kuliwa kwamba ni machukizo, natubafahamu pia kibiblia mnyama amebeba picha ya roho ya utawala kwa hiyo kuna roho ya uhasi ambayo inawezekana huko nyuma wazazi wetu kizazi cha 3 au 4 kuingia katika maagano ya miungu ndio maana ulipopatizwa ndoto ilikuja ili kukumbusha kwamba kuna utawala ulionao kwanini unataka kuingia utawala mwingine wakati uko katika utawala mwingine?

Mambo ya kuzingatia

Unaweza kuongea na wazee wako kabla ya kuokoka kupata historia ya ukoo wenu?

Pili ingia kwenye maombi ya toba Zab 51, Maombelezo 5:7.

Kama unanena kwa lugha omba kwa kunena kwa lugha Mungu atakusadia

Tatu fanya kama alivyofanya Gidion kwa kutoa sadaka dhidi ya miungu ya baba yake Waamuzi 6:15_20

Nne omba uongozi wa roho mtakatifu

Nb usisahau kutumia Damu ya Yesu kuomba toba Mathayo 26:24 ,Waebrania 12:24

Omba Mungu akusaidie katika vita ambayo unapigana maana hiyo ni vita dhidi ya wakovu wako usiposhinda wokovu wako utakuwa na upizani sana katika maisha yako
 
Kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa makubwa na manyoya mengi; na tazama, mzabibu huo ukapinda mizizi yake imwelekee yeye, ukachipuza matawi yake yamwelekee yeye, toka matuta yake ulipopandwa; ili yeye apate kuunywesha.
Ezekieli 17:7,

Ukiweza kusoma biblia ya kiingereza ya Amplifier Bible Ezekiel 17:3, 17:7 Neni tai wamefananisha na mfalme Nebukadneza na Mfalme wa Misri kwa hiyo Tai anabeba picha ya ufalme na ukiona Nebukadneza na Farao Mfalme wa Misri walikuwa wafalme ambao walikuwa wanaabudu miungu hivyo basi kwa ndoto yako tai ni aina ya ufalme ambao ulikuwa unatumikiwa na familia au uko
 
 

Attachments

  • Screenshot_20260729_173914_Devotional Bible.jpg
    285.6 KB · Views: 5
Asante¡ mtumish..... hivi inawezekana kumuota mtu ambaye hujawahi kumuona?
Ipo hivi... Nishaota wazazi wa baba, wamekuja home kututembelea sasa wakati tumekaa wakawa kama wanamgombeza mzee yani kama vile kuna mambo kuhusu mila ameyapuuzia na mimi na wa zoom tu ila mzee amekaa kimya... By the way sijawahi kuwaona na upande wa mzee hatujawahi hata kukanyaga nayeye hata kutupeleka hata kuwasalimia hua anapiga chenga tu¡ what a resson behind... Mwl Mwakujonga
 
Mh! hapo kuna mambo ya asili hapo.
 
Inawezekana kabsa
Tusome kwanza biblia
Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Yohana 1:48

Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.Yohana 8:58

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 1:27

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.Yohana 4:24

Nimeweka mistari hapo juu kwa ajili ya kuonyesha ushahidi wa kwamba unaweza kuota ndoto ya mtu ambaye hata umjui au haujawai kumwona, kwanini? Kwa sababu mtu ni roho, na roho ya mwanadamu haifi ni ya milele kwa hiyo roho ilivyo umbwa na Mungu ni kuyajua ya mwanzo na mwisho ndo maana roho ni ya milele


Mimi pia nilishawai kuota ndoto kama yako najua maana ya kuota ndoto ya watu ambao huwajui

Twende kwenye maana ya ndoto hii

Ndoto hii maana yake kuna mambo ambayo babu yako naamini hayuko hai na wakati anakufa hayo mambo yalitakiwa kufanywa na baba yako lakini hakuyafanya ndio maana anamkombeza

Kwanini anamgombeza hayo mambo ni ya kiroho kuna kitu cha kurithi kinatakwa kutoka kizazi kimoja kwemda kizazi kingine

Sijajua kama wazazi wako wako hai, kama wako hai maana yake wanatakiwa kufanya hayo mambo kabla hawajaondoka duniani ili kuwepo na mrithi wa kitu cha kiroho
 
I do know why! mabalaa kwetu hayaishagi hasa brother na sister!
 
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mhubiri 9:5

Sio wafu wamsifuo Bwana, Wala wo wote washukao kwenye kimya. Zaburi 115:17

Kwa hiyo wafu hawajui neno lolote kwa hiyo kama walishakufa na ndoto ni ya rohoni maana yake hata maelekezo yao hayana maana kwa sababu wafu hawana taraja katika yoyote ambayo wanakuelekeza kufanya

Ndio maana ni hatari sana kuota ndoto za watu waliokufa wakikupa maelekezo au wakikupa kitu

Kwanini walikuwa wanaongea na baba yako, inawezekana kuna mambo ya kiroho ambayo baba yako anatakiwa kuyafanya kwa ajili ya ukoo kama mambo ya kurithi

Pia tufahamu wazazi wetu wanapokwena kwa miungu wanatutoa na sisi kuwa sehemu ya agano na wanapo hapa kweye madhabahu ya miungu , inapata uhalali wa kututafuta tuitimikie kwa agano alilofanya babu

Kwa hiyo ndoto hiyo ni kumwomba Mungu akupe ushindi katika vita hivyo vya kiroho, kumbuka ombea jina lako kwa Damu ya Yesu , futa jina lako kwenye orodha ya ukoo ambayo ina maagano na miungu ili miungu isiwe na uhalali na maisha yako

Inaonekana baba yako ndio ameweka ngumu kwa miungu kukufikia kwa hiyo unatakiwa kuomba kuvuka kabla baba yako hajaondoka duniani kwa sababu itakuwa ngumu kwako kupambana mwenyewe

Mungu akutete na kukupigania damu ya Yesu ikushindie katika vita hii, muhimu usitumie maombu ya kuvunja madhabau ya ukoo ni hatari kwao , ombea toba kwa damu ya Yesu na ombea ujitenge na hiyo madahabahu kwa ajili ya kupata uhalali wa kupambana nayo maana kwa sasa jina lako liko ktk hiyo madhabau ndio maana wanakutafuta
 
Thanks... mkuu¡ kikubwa ni kumwamini YESU na kuwa mwaminifu..... ndilo ombi langu¡¡¡
 
Ahsante sana Mwl kwa somo la lango la ndoto. Nimeelewa vizuri sana Mungu akubariki.

Mimi ni kati ya wale wanaoota hata nikilala dakika moja tuu, iwe ni mchana au usiku.
Nina swali kuna kipindi nilitanga mbali kabisa lakini niliendelea kuota kila siku, hiyo inatokana na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…