Kuna umuhimu wa afya za viongozi wa ngazi za juu ziwekwe wazi kila baada ya kipindi fulani?

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Nimelazimika kupandisha huu uzi hewani baada ya kurudisha kumbukumbu namna mzee wetu hayati JPM alivyotutoka bila hata ya kutupatia angalau dakika 5 za kumuombea

Tukiweka ushabiki wa kivyama pembeni hayati JPM alikuwa akipendeka sana ndani na nje ya nchi kiasi cha kama wananchi wangehisi hujuma kwenye kifo chake huenda yangezuka machafuko

Kulingana na hayati kuwa na maradhi ya muda mrefu ambayo yalionekana kuwa na uwezo was kumuondoa Duniani wakati wowote ingekuwa vyema kama wananchi wakajulishwa mapema ili kuondoa uwezekano wa machafuko endapo ikitokea kifo cha ghafla hadharani ama sirini

kwahiyo natoa pendekezo kwa mamlaka husika kuweka utaratibu wa kutangaza hali za kiafya za viongozi wakubwa kama Raid,waziri mkuu,Speaker,CDF,IGP nk ili kuwaweka watu tayari endapo likitokea la kutokea

Hebu fikiria mpaka sasa huko Magu kuna tetesi Mabeyo alikuwa mgonjwa sana na alikuwa akitibiwa kwa zaidi ya miezi mi2 nyumbani kwa mama yake baada ya kugoma kupelekwa nje ya nchi kwa sababu/machale zake binafsi
 
Kwani ulihitaji nini kujua jiwe ni mgonjwa ?

Kwenye kampeni zile feni na kampeni siku 2 mapumziko siku 8 hukujua kuna shida.??

Sio kila kitu kitawekwa wazi ila muda haujawahi kudanganya.
 
Sipo tayari mtake msitake
 
Kwani ulihitaji nini kujua jiwe ni mgonjwa ?

Kwenye kampeni zile feni na kampeni siku 2 mapumziko siku 8 hukujua kuna shida.??

Sio kila kitu kitawekwa wazi ila muda haujawahi kudanganya.
Kwani alikuwa anawekewa mifeni kipindi cha kampeni
 
Tatizo ni wale waliosema Raisi Magufuli ni mzima na anachapa kazi ,Suali walishindwaje kutujuvya kuwa Raisi ni Mgonjwa na anahitaji maombi au duwa ?
Hawa ndio tatizo au ndio wenye siri .maana walitoka kwa vishindo na kuwasuta wananchi kuwa Raisi sio mgonjwa kama ilivyotandaa kwenye mitandao ,siku moja baada ya kauli zao tunasikia Raisi kipenzi cha wanyonge hakimu wetu ametuaga na sasa anahukumiwa yeye.

Waliotangaza watoke hadharani watuambie ni sababu gani zilizowafanya waseme uongo kulitangazia Taifa au na wao walidanganywa ? Sijui kwa nini ilikuwa siri ?
 
"Mzee wetu" ni mzee wako na nani? Usiweke wingi bila kushirikisha wengine kabla.
 
Afya zao hazipaswi kuangaliwa mara kwa mara kwa sababu viongozi wa ngazi za juu wanatakiwa kufa haraka sana kwa sababu ni mafisadi wanaohamasisha ufisadi kwenye serikali zao tena kupitia TV ya Taifa
 
Back
Top Bottom