Kuna umuhimu wa kujenga nyumba ukiwa na miaka 60?

Kuna umuhimu wa kujenga nyumba ukiwa na miaka 60?

Maisha yote uliishi nyumba ya kupanga, leo ukiwa 60 ndiyo umestaafu na kulipwa mafao. Ndiyo unatafuta kiwanja ujenge nyumba. Ni kheri kuhesabu pesa ya mafao kwa kodi ya nyumba kwa miaka iliyobaki au uingie kwenye changamoto za ujenzi?

Kodi ni laki mbili na nusu kwa mwezi na mafao yako ni milioni 100, bado kuna pension ya laki moja na nusu kila mwezi.
Milioni 100, kimahesabu ni nyingi, lakini ukiwazipata na kuamua kuspend ni ndogo mno, huwezi kukaa naxo hata miaka 3. Kuna mzee mmoja, alipostaafu akapata zake mafao hayo, aliamua kutumia kwelikweli. Aliishi amukia bar na kulala hotelini with sweet babies. Nakuambia hazikukaa hata miaka miwili. Leo hii ukimuona anasikitisha ni Kama kichaa, anaongea pekee yake na kunywa kangara. Bahati yake alikuwa amejenga nyumba enzi za utumishi wake. Na kwa taarifa yako haumwi na hajafa. Hivyo, Bora ujenge uishi kwako na bila stress. Ujue pia hela nyingi ambaxo hujawahi kumiliki, Ni ngumu kuzitunza na kukaa naxo.
 
NINAO matajiri wanaojenga baada hata ya 70 maana nyumba ni asset itakayoweza kuhifadhi watu na kuwapatia kipato wote watakaoimiliki kwa miaka kama 40-50 tangia kujengwa.Ni vizuri kufikiri mbali kuliko miaka yetu
 
Unatakiwa ujenge ukiwa na kwanzia miaka 23 ukifika 30 unaacha unaanza kula bata
 
Kama una familia jenga kwa manufaa ya familia, kama huna unamjengea nani? Ama vipi ponda maisha Ila uache kidogo ya kukuzika.
 
Back
Top Bottom