Nia ni kuutafuta na kuukata mzizi wa fitna ndiyo maana hata watu wa Yanga waliochangia kwa staha tumeenda nao fresh bila kurushiana vile vijembe vyetu vya kila siku.
Hivi haijakushangaza kwa baadhi ya watu kwenye jukwaa hili ambao hapo kabla walionekana ni watetezi wakubwa wa maslahi ya Simba ila katika uzi huu wameonekana hawajaguswa kabisa na maamuzi mabovu na ya hovyo ya viongozi na wamegeuka watetezi wakubwa wa maamuzi hayo? Kuna kitu nimejifunza leo.
Kramo aliporudi December alisema yuko fresh na Mapinduzi pia alikwenda, mwisho wa siku yakasemwa haya haya "mwalimu ndiyo ataamua kama amtumie", au "madaktari wetu wanaendelea kumchunguza".
Kuna video moja Kramo aliporudi tu ile December akiwa tayari, mchambuzi Mbwaduke alimpa sana maua yake akasema jinsi gani atakuja kuisaidia Simba. Sasa unamuachaje mchezaji huyo katika list ya wachezaji wako huku ukijua una miezi 6 mbele ya mechi zingine ngumu zitakazomuhitaji? Walikuwa wanapoteza nini kwa kutolitoa jina lake CAF?
Na kibaya zaidi na ndiyo kilinishtua, ni kuona dalili kuwa mchezaji hajui kuwa jina lake liliondolewa kwa hiyo inaonyesha kuna maamuzi ya hila na yasiyo ya nia njema dhidi yake na klabu yalifanyika.