Kuna uwezekano Aubin Kramo hajui kuwa jina lake limeondolewa kwenye wachezaji wa Simba

Kwa maoni yangu naona kama Kramo kwa upande wa mashindano ya klabu bingwa anaweza kucheza, kwasababu zifuatazo:

Ukiangalia katika ligi kuu ni wachezaji wote 12 wameshatumika ambao ni
Ayoub
Cha Melone
Babacar
Saidoo
Chama
Onana
Jobe
Freddy
Inonga
Kanoute
Ngoma
Luis

Kama hao wachezaji 12 wametumika, ina maana mchezaji wa 13 ni Kramo ambaye hakusajiliwa kwaajili ya ligi kuu bali atakuwa yupo upande wa mashindano ya kimataifa. Hivyo ni sahihi kwake kucheza klabu bingwa na kwavile mfumo wa klabu bingwa hauna limitation za idadi za wachezaji wa kigeni maanake Kramo anaweza kuingizwa kwenye mfumo.
 
Hayupo kote kwa maana hawezi kucheza mechi yeyote eidha ya ligi au CAF kwasababu sio sehemu ya kikosi.
Umechukua muda mrefu sana kulijibu swali hilo ila najua ni kwa nini. Kwa nini sasa Simba wamelitoa jina lake CAF wakati sheria za CAF zinaruhusu kuwepo kwake kwenye kikosi? Sidhani kama utanijibu hili.
 
Kwa maoni yangu naona kama Kramo kwa upande wa mashindano ya klabu bingwa anaweza kucheza, kwasababu zifuatazo:

Ukiangalia katika ligi kuu ni wachezaji wote 12 wameshatumika ambao ni
Ayoub
Cha Melone
Babacar
Saidoo
Chama
Onana
Jobe
Freddy
Inonga
Kanoute
Ngoma
Luis

Kama hao wachezaji 12 wametumika, ina maana mchezaji wa 13 ni Kramo ambaye hakusajiliwa kwaajili ya ligi kuu bali atakuwa yupo upande wa mashindano ya kimataifa. Hivyo ni sahihi kwake kucheza klabu bingwa na kwavile mfumo wa klabu bingwa hauna limitation za idadi za wachezaji wa kigeni maanake Kramo anaweza kuingizwa kwenye mfumo.
Ndiyo hapo utastaajabu jina lake limeondolewa, kwa mujibu wa facts za Scars, wakati ni mchezaji ambaye angeweza kuisaidia sana timu kipindi hiki. Kibaya zaidi Simba ilikuwa haina cha kupoteza kwa kulibakisha jina lake CAF maana tayari inaendelea kumlipa stahiki zake.
 
Sidhani kama jina limeondolewa, na kama itakuwa hivyo basi uongozi haukutumia uweledi wao.
 
Umechukua muda mrefu sana kulijibu swali hilo ila najua ni kwa nini. Kwa nini sasa Simba wamelitoa jina lake CAF wakati sheria za CAF zinaruhusu kuwepo kwake kwenye kikosi? Sidhani kama utanijibu hili.
Hivi haya maswali yako ni upo serious au unafanya joking?

Inawezekana vipi mchezaji kutambuliwa na CAF bila kupitia shirikisho la nchi ambayo anachezea?

Hivi hilo lingekuwepo unadhani Yanga wangethubutu kumficha Kambole Kigamboni wakati kulikuwa na option ya kumuacha kwa kigezo cha CAF sheria zinaruhusu?

Hivi ulichoandikia ni kweli kuwa hutambui mchezaji anaanzia kutambuliwa na shirikisho husika la nchini mwa hiyo Club?

Hivi ni kweli hutambui kuwa Club haina uwezo wa kupeleka jina la mchezaji CAF bila huyo mchezaji kusajiliwa na shirikisho la nchi hiyo ambayo Club ipo?

Inawezekana vipi mchezaji ambaye hajasajiliwa TFF apate kibali cha kushiriki michuano ya CAF?
 
Sidhani kama jina limeondolewa, na kama itakuwa hivyo basi uongozi haukutumia uweledi wao.
Kwamba Kramo anayo access ya kushiriki michuano ya CAF?

Sheria za CAF zinasema kuwa mchezaji ambaye ame qualify kushiriki michuano ya CAF ni lazima awe na vitu hivi.

1. Awe na leseni iliyotolewa na Club yake na kusajiliwa na shirikisho la nchi hiyo kwenye dirisha linalofanyika July 20 na lile la awamu ya pili la januari 31

2. Awe na leseni ya CAF
3. Awe na sifa ya kushiriki michuano ya ligi kuu kwenye nchi ambayo hiyo Club inashiriki CAF.
4. Awe anaishi kwenye hiyo nchi ambayo timu anayochezea.

Sasa ebu niambie kwa situation hiyo Kramo ana sifa za kuwa mchezaji anayetambulika na CAF na kufanya aweze shiriki michuano hiyo?
 
Hivi haya maswali yako ni upo serious au unafanya joking?

Inawezekana vipi mchezaji kutambuliwa na CAF bila kupitia shirikisho la nchi ambayo anachezea?

Hivi hilo lingekuwepo unadhani Yanga wangethubutu kumficha Kambole Kigamboni wakati kulikuwa na option ya kumuacha kwa kigezo cha CAF sheria zinaruhusu?

Hivi ulichoandikia ni kweli kuwa hutambui mchezaji anaanzia kutambuliwa na shirikisho husika la nchini mwa hiyo Club?

Hivi ni kweli hutambui kuwa Club haina uwezo wa kupeleka jina la mchezaji CAF bila huyo mchezaji kusajiliwa na shirikisho la nchi hiyo ambayo Club ipo?

Inawezekana vipi mchezaji ambaye hajasajiliwa TFF apate kibali cha kushiriki michuano ya CAF?
Unashangaa wakati ninachoongelea nawakilisha mawazo ya wanasimba wengi ambao hadi hivi sasa wanaamini siyo tu kwamba Kramo anastahili kuwa kwenye kikosi cha Simba bali pia wanaamini YUMO kwenye orodha ya wachezaji wanaotegemewa kuisaidia timu katika mashindano ya CAF yanayoendelea. Kwa hiyo unaponishangaa mimi kuna wengi wanakushangaa wewe kwa ulichoandika hapa.

Kuna watu wamekupa mifano hapo juu ya hali kama hii iliwahi kutokea ya mchezaji wa Simba alisajiliwa CAF bila kuwepo kwenye usajili wa ligi. Hadi Yanga wapo wengi wanaamini Kramo amesajiliwa CAF.

Usiseme unashangaa, wote tunashangaa na kuna wengine wanakushangaa wewe kwa mtazamo uliouchukua leo. Inawafanya wajiulize huyu Scars ambaye huwa anaitetea sana Simba, leo imekuwaje anatetea uozo?
 
Huyo Kramo kacheza mechi ngapi mpka mhisi anaweza kua msaada kwenye timu
 
Itakuwa ni mawazo ya wengi ambao hawapendi kujishughulisha kutafuta ukweli kupitia vyanzo sahihi.

Kuna vitu inaonesha vinawaweka kwenye mkanganyiko.

Kuna leseni personal ya mchezaji ya usajili wake kwenye system ya CAF ambayo lazima awe nayo.

Usajili wa leseni ni tofauti na usajili wa ushiriki wa michuano.

Kwa hiyo Kramo sio kama amefutiwa leseni ya CAF ila ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji katika mfumo wa usajili.

Mchezaji anaweza akawa na leseni ya CAF lakini leseni peke yake haiwezi kumbeba kama kigezo cha kumfanya ashiriki michuano ya CAF ikiwa kwenye federation la hiyo nchi ilipo hiyo timu hayupo registered.
 
Kwamba Kramo anayo access ya kushiriki michuano ya CAF?

Sheria za CAF zinasema kuwa mchezaji ambaye ame qualify kushiriki michuano ya CAF ni lazima awe na vitu hivi.

1. Awe na leseni iliyotolewa na Club yake ya kusajiliwa na shirikisho la nchi hiyo kwenye dirisha linalofanyika July 20 na lile la awamu ya pili la januari 31

2. Awe na leseni ya CAF
3. Awe na sifa ya kushiriki michuano ya ligi kuu kwenye nchi ambayo hiyo Club inashiriki CAF.
4. Awe anaishi kwenye hiyo nchi ambayo timu anayochezea.

Sasa ebu niambie kwa situation hiyo Kramo ana sifa za kuwa mchezaji anayetambulika na CAF na kufanya aweze shiriki michuano hiyo?

1) Naomba nioneshe kipengele kilichoanisha kuwa mchezaji anatakiwa awe na sifa ya kushiriki ligi kuu.
2) haikuwahi kutokea mchezaji wa Simba kutoshiriki ligi kuu lakini mashindano ya CAF akawa anashiriki?

Hizi chini taratibu za CAF champions league ila sijaona hiko kipengele cha ligi kuu
IMG_20240324_161810.jpg
 
Sidhani kama hupo sahihi ndugu, Aubin Kramo kama muajiriwa wa Simba na Simba akiwa kama muajiri, pande zote mbili zina haki ya kujua na kutumiza makubaliano waliyoingia kimkataba.

Hivyo basi Aubin anajua fikra jina lake kuondelewa kwa msimu huu katika mashindano yote kwa vile Simba hawawez kuvunja makubaliano pasipo kuwasiliana na Aubin.

Isitoshe hali ya ugonjwa/majeraha ya muda mrefu inawapa haki pande zote mbili kufukiana makubaliano ya kusitisha mkataba kwa maelewano ya pande zote mbili.
 
Pamoja na mapenzi kwa timu yangu, ila mara kwa mara sijasita kuja na malalamiko dhidi ya uongozi wa Simba na moja ya maeneo yanayokera wengi yanahusiana na treatment ya wachezaji wake kuanzia wale walio bora hadi wale ambao wanaonekana mchango wao umepungua mno na wanaigharimu timu. Imefika wakati unashangaa wachezaji walio bora wanapewa huduma mbovu ndani ya timu hadi kuachwa katika mazingira ya kutatanisha, halafu wale ambao viwango vyao vinatia mashaka ndiyo tunaaminishwa ndiyo tegemeo la timu.

Juzi nilikuwa naangalia video moja wakati Simba inakwenda Zanzibar, ukimsiklliza interview ya Aubin Kramo haupati picha kama ni mtu aliye na taarifa kuwa si tena sehemu ya kikosi cha Simba msimu huu. Ukimsikiliza Ahmed Ally anasema jina la Kramo liliondolewa ila anaendelea kulipwa stahiki zake zote. Kama kuna mtu anabisha, mtu ajitokeze amuulize swali hili moja kwa moja Kramo mwenyewe kama anajua kuwa jina lake limeondolewa. Kama anasema anajua natoa 100,000 kwa mwandishi yoyote atakayepewa jibu hilo. Kwa mtazamo wangu Kramo alishapona ila kuna watu wamemkazia ili kulinda wachezaji wao. Majeraha ya Kramo hayakuwa ya kumkalisha nje muda mrefu kiasi hiki.

Huyu ni mchezaji mwingine ambaye msimu ukiisha ataachwa katika mazingira ya kutatanisha halafu ukamkuta upande wa pili anakiwasha. Hii ni story inayojirudia ya Moses Phiri, tulikuwa tunaambiwa hajapona hajapona, mara amepona ila ni maamuzi ya mwalimu kumtumia, mwisho wa siku mchezaji mwenyewe anaona huu ni upuuzi anaonyesha dalili za kutojali maana hata juhudi zake bado hazimpi namba tena, mara anakuja kuachwa. Kuna tatizo kubwa sehemu pale Simba ila hatutaki kulisema.

Kwa kumalizia, kwenye dirisha dogo lililopita kuna mchezaji mwenye sifa ya kuikaba timu ambaye mkataba wake ulikuwa umeisha kulingana na taarifa walizokuwa wametupa hapo kabla ila dirisha dogo likafungwa hatukuambiwa kama ameongezewa mkataba na usishangae mwakani tena tukawa naye huku kina Kramo wakiachwa.
Kramo kaondolewa ili kupisha nafasi kwa mchezaji mwingine kuitumikia Simba, kwa lengo la kumpa nafasi ya kupona vizuri majeraha yake.

Awali, kulikuwa na makosa ya kutaka kumtumia haraka kwenye kikosi, na kuanza mazoezi kabla ya kupona vizuri na kujitonesha.

Yaliyofanyila ni maamuzi ya pande zote, kwani bado ana mkataba na Simba, na msimu ujao atarudi kikosini, ikiwa atakuwa amepona kabisa.

Ova
 
1) Naomba nioneshe kipengele kilichoanisha kuwa mchezaji anatakiwa awe na sifa ya kushiriki ligi kuu.
2) haikuwahi kutokea mchezaji wa Simba kutoshiriki ligi kuu lakini mashindano ya CAF akawa anashiriki?

Hizi chini taratibu za CAF champions league ila sijaona hiko kipengele cha ligi kuu View attachment 2943514
Hapa sasa ndio tutakuwa tunafanya mjadala kisomi.

Naona ume quote maelezo yanayozungumzia mifumo ya usajili. sasa shuka chini ibara ya pili kuhusu vigezo vya mchezaji kushiriki michuano.

Kwanza soma hiyo ya kwanza kabisa achana na hiyo niliyo highlight
dzccwlfeawo1gewhntcj-13.jpg
 
Hapa sasa ndio tutakuwa tunafanya mjadala kisomi.

Naona ume quote maelezo yanayozungumzia mifumo ya usajili. sasa shuka chini ibara ya pili kuhusu vigezo vya mchezaji kushiriki michuano.

Kwanza soma hiyo ya kwanza kabisa achana na hiyo niliyo highlight
View attachment 2943533
Kwa kipengele (A na B) hilo linawezekana kama uongozi wa Simba ilikuwa na malengo kumtumia katika mashindano ya klabu bingwa ambavyo itamaliza hadi ishu ya kipengele D kwavile hivyo vyote inafanyika wakati wa kuingiza jina kwenye system (kabla hata ya mashindano kuanza)

Kwa kipengele C ili kujua kama haiwezekani au inawezekana tutoke kwenye nadharia twende kwenye reference ya Perfect Chikwende dhidi ya Kahata.

Katika hao wachezaji wawili, kuna mmoja hakuwa anashiriki michezo ya ligi kuu lakini michuano ya CAF alikuwa anacheza. Je iliwezekanaje?
 
Kramo kaondolewa ili kupisha nafasi kwa mchezaji mwingine kuitumikia Simba, kwa lengo la kumpa nafasi ya kupona vizuri majeraha yake.

Awali, kulikuwa na makosa ya kutaka kumtumia haraka kwenye kikosi, na kuanza mazoezi kabla ya kupona vizuri na kujitonesha.

Yaliyofanyila ni maamuzi ya pande zote, kwani bado ana mkataba na Simba, na msimu ujao atarudi kikosini, ikiwa atakuwa amepona kabisa.

Ova
Huyu mwandishi huwa ana habari za ndaani kwenye masuala ya usajili na ni mshabiki wa Simba. Kuna mtu alimuuliza jana akasema Kramo amesajiliwa na Simba CAF. Kama nilivyosema toka post ya kwanza hii issue inaenda kufanana na ya Phiri, huyu mwandishi anasema uamuzi umebaki kwa kocha kumtumia ama la, kama tulivyokuwa tunaambiwa kwa Phiri.

Screen Shot 2024-03-24 at 5.28.05 PM.png
 
Huyu mwandishi huwa ana habari za ndaani kwenye masuala ya usajili na ni mshabiki wa Simba. Kuna mtu alimuuliza jana akasema Kramo amesajiliwa na Simba CAF. Kama nilivyosema toka post ya kwanza hii issue inaenda kufanana na ya Phiri, huyu mwandishi anasema uamuzi umebaki kwa kocha kumtumia ama la, kama tulivyokuwa tunaambiwa kwa Phiri.

View attachment 2943559
Asa ikiwa hivyo kama huyo mwandishi alivyosema, huoni kuwa uzi wako unakuwa batili? Maana wewe unasema kuna uwezekanao jina la Kramo limeondolewa.
 
Sidhani kama hupo sahihi ndugu, Aubin Kramo kama muajiriwa wa Simba na Simba akiwa kama muajiri, pande zote mbili zina haki ya kujua na kutumiza makubaliano waliyoingia kimkataba.

Hivyo basi Aubin anajua fikra jina lake kuondelewa kwa msimu huu katika mashindano yote kwa vile Simba hawawez kuvunja makubaliano pasipo kuwasiliana na Aubin.

Isitoshe hali ya ugonjwa/majeraha ya muda mrefu inawapa haki pande zote mbili kufukiana makubaliano ya kusitisha mkataba kwa maelewano ya pande zote mbili.
Kuna watu mmenipa kazi ya kupekenyua mitandao, itabidi mnilipe maana si kwa kazi hii niliyofanya. Hii interview ya jana tu ya Ahmed Ally anasema Kramo hayupo kwenye usajili wa Simba kwenye NBC wala CAF.

View: https://www.youtube.com/watch?v=gO5BU-9jq2Q&t=10s

Kuna viashiria kuonyesha uwezekano wa kwamba Kramo hajui kuwa jina lake halipo katika wachezaji wa Simba ambao wanaoweza kutumika CAF katika hatua zilizobaki, mojawapo ya ni hii interview wakati timu inakwenda Zanzibar.

View: https://www.youtube.com/watch?v=43dFwMmZdZE&t=151s

Na hapo nimeacha interview nyingi nilizokutana nazo za watu waliohojiwa wengine wako karibu na timu na viongozi na inaonyesha wote walikuwa wanaamini Kramo amesajiliwa na muda wowote anaweza kutumika.
 
Asa ikiwa hivyo kama huyo mwandishi alivyosema, huoni kuwa uzi wako unakuwa batili? Maana wewe unasema kuna uwezekanao jina la Kramo limeondolewa.
Post yake inapingana na kauli ya Ahmed Ally na huyo mkuu anayetoa vifungu vya sheria hapo juu. Nimeileta post yake kuonyesha inawezekana hili jambo limekuwa linafichwa kiasi kwamba hadi wafuatiliaji wa karibu wa Simba mpaka uzi huu ulipokuwa unapandishwa walikuwa wanajua Kramo anaweza kutumika hata mechi na Al Ahly.

Huo ndiyo msingi wa huu uzi ndiyo maana unaona huu mkanganyiko ulioibuka. Angalia video mbili nilizopost hapo juu.
 
Post yake inapingana na kauli ya Ahmed Ally na huyo mkuu anayetoa vifungu vya sheria hapo juu. Nimeileta post yake kuonyesha inawezekana hili jambo limekuwa linafichwa kiasi kwamba hadi wafuatiliaji wa karibu wa Simba mpaka uzi huu ulihpokuwa unapandishwa walikuwa wanajua Kramo anaweza kutumika hata mechi na Al Ahly.

Huo ndiyo msingi wa huu uzi ndiyo maana unaona huu mkanganyiko ulioibuka. Angalia video mbili nilizopost hapo juu.
Ni sahihi post yake inapingana na Ahmed Ally ila ukweli utakuja kudhihirika, kama hatokuwepo hata sub basi ni wazi Ahmed Ally yupo sahihi ila ikitomea amecheza au yupo sub basi Ahmed Ally hajui mambo yote ya ndani ya klabu ya Simba.

Kuhusu huyo aliyoweka vifungu vya sheria, nakumbuka Kahata alikuwa hachezi ligi kuu bali alikuwa yupo kwaajili ya mashindano ya CAF pekee.
 
Back
Top Bottom