Kuna swali unalikwepa na nakuuliza kwa mara ya tatu, kwa ufahamu wako Kramo amesajiliwa Simba katika mashindano ya CAF au hajasajiliwa?
Tatizo unapenda majibu mepesi.
Kwanza umeshaonesha wasiwasi na taarifa za Club, kitu ambacho ni ngumu sana mimi na wewe kuafikiana upi mbadala sahihi wa sources za kupata taarifa za wachezaji ikiwa kama tutaamua kupuuza vyanzo rasmi vya Club.
Nikikujibu kupitia references za Club unasema wanaongopa, maana yake kuna vyanzo vyako ambavyo unaviamini tofauti na Club.
Vyanzo ambavyo unaviamini nauhakika kwa asilimia kubwa ni hearsay ndio iliyotawala kama msingi miuu wa taarifa.
Ndio maana nimekuambia ili nikupatie majibu yatayofanya uridhike unashauri zitumike references gani kama sources??
Kwamba nimfate mchezaji mwenyewe nimuulize? Hell no!
Kwasababu sitaki maswala ya speculation na assumptions za kuunga unga itaonekana kama ni mjadala wa kijiwe cha kahawa ambapo hoja sio kipaumbele.
Na hoja ya msingi ambayo mpaka sasa umeshindwa kuitambua ni hii.
Wewe unadai kuwa Kramo hajui kama yupo kwenye kikosi.
Na wakati huo huo unakubali kuwa Simba imetoa tamko hadharani kuwa Kramo sio sehemu ya kikosi.
Sasa jiulize tu
Kama unafikiria Simba imemuondoa Kramo bila yeye kujua, ni ipi point ya Simba kwenda hadharani kutangaza kuwa Kramo hayupo kwenye kikosi cha Simba huku ikijua wazi kufanya hivyo kutaweza kufanya habari hizo zimfikie Kramo??