Kuna uwezekano mkubwa miradi ya SGR na Stieglers' Gorge isikamilike

Kuna uwezekano mkubwa miradi ya SGR na Stieglers' Gorge isikamilike

Mkuu Gambino, tumeishajiandaa kwa yote, hili likitokea miradi hiyo kusimama kutokana na Corona, hiyo hali kisheria inaitwa force majeure, hivyo kitakacho fuata, ni kumuongezea muda wa kutosha rais Magufuli aendelee kusalia madarakani hadi akamilishe miradi mikubwa yote ndipo tumruhusu.

P

Kumbe akiingia Rais mwingine madarakan kuna uwezekano akaifutilia mbali miradi iliyoanzishwa na mtangulizi wake hata kama iko katika hatua za kukamilika?
 
Typing errors kibao unatumia simu ya tochi?

Pili acha ubishi kwenye issue za kitaalamu zinazohitaji akili kama hizi!!

Upo mtupu kichwani.
Si lazima useme hivyo. Wachawi mnajulika kwa kuuficha ficha mambo hata maneno mnaficha ficha hamui wawazi.

Endemic au pandemic doesn't matter. Yeyote upendavyo itumie, makes no different wakati wewe umeli localize hilo janga kwenye SGR na Striker pekee lakini hujagusia migodi ya Twiga.

Pia umesahau kuwa juzi tu SCB one "negotiate" Kwa niaba ya serikali na kufanikisha financing ya mradi ws SGR mpaka unwpoiehiq phase ya pili.

Sasa hivi watu wapo kwenye maandalizi ya kupata fedha za kuanza phase ya tatu na kuendelea, uko wapi wewe, umelala?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
When one door is closed the other is opened.

Miradi itaendelea labda litokee lingine.

Historia inaonesha hakuna calamity ya endemic/pandemic iliyomaliza mwaka mmoja bila kutulia.

Umeandika kiushabiki kama vile unafurahi hiyo miradi isipokamilika.

Miradi itakamilika na utaendelea kuuguza majeraha ya moyo huku upo ndani ya SGR.

Umeniaminisha wachawi wengi Tanzania.
Aliyetangaza kuitekeleza ana undugu na mzee yusufu!
Mipasho na kebehi juuu!!!
 
Mkuu Gambino, tumeishajiandaa kwa yote, hili likitokea miradi hiyo kusimama kutokana na Corona, hiyo hali kisheria inaitwa force majeure, hivyo kitakacho fuata, ni kumuongezea muda wa kutosha rais Magufuli aendelee kusalia madarakani hadi akamilishe miradi mikubwa yote ndipo tumruhusu.

P
Hiyo "force majeure" inatupa haki ya kumuondoa magufuli ikulu.
Nyie wapambe nuksi!!!
 
Kumbe akiingia Rais mwingine madarakan kuna uwezekano akaifutilia mbali miradi iliyoanzishwa na mtangulizi wake hata kama iko katika hatua za kukamilika?
Vipi unajua chochote kuhusu Bandari ya Bagamoyo?. Nani alianzisha?, alipoingia mwingine do you know what happened?.
Vipi unajua chochote kuhusu Katiba mpya?. Do you know how much we spent?. Do you know aliyefuata, amefanya nini?.
P
 
Hizi nchi zetu masikini ikitokea changamoto kidogo ni shida kubwa sana.

Tanzania inategemea mapato ya utalii kwa zaidi ya 25%. Utalii mwaka huu ni kama umekufa kabisa kama sio uko chini ya 2%. Hasa kipindi hiki cha March hadi June hua kuna watalii wengi sana nchi hii, ila sababu ya corona kila mtu anajua kinachoendelea.

Maana yake ni kua mapato ya utalii tumeyakosa na hata mwaka wa 2020/2021 ni vigumu kuyapata kwa sababu nchi karibu zote Duniani zimeathirika na chumi nyingi Duniani zitaporomoka. Kama kutakua na watalii ni wachache sana.

Kwa miezi 9 ya mwaa huu wa fedha TRA wamekusanya 10.9 Trillion ila tegemea robo ya mwaka huu, yaani March-June makusanyo kua madogo sana kwa sababu hakuna biashara, wafanyabiashara wengi wanaomba kufunga na mambo yameharibika. Hivyo mwaka huu tu ni changamoto kubwa. Kitakachopatikana chote kitaishia kwenye matumizi.

Kutokana na uchumi kuvurugika serikali italazimika kukopa zaidi na hiyo mikopo haitakua ya maendeleo, itakua ya matumizi kwa sababu hata makusanyo ya matumizi itakua ni changamoto. Serikali italazimika kuachana na miradi yake mikubwa ili kugharimia matumizi ya kawaida na ya lazima.

Kws mtazamo wangu, serikali italazimika kukopa ma moja ya masharti ili ipewe mkopo ni kuachana na miradi kama SGR na Stieglers. Ikitokea hivyo ujue mradi ndio utakufa au utachukua mida mrefu kukamilika. Naona yunaelekea huko.

Binafsi naunga mkono miradi kama Stieglers na SGR ila naona kuna uwezekano mkubwa sana corona kutia mchanga kitumbua chetu na kuturudisha nyuma kama sio kutumaliza kabisa.

Itakapotokea tukaweka nchi kwenye lock down ndio itakua mwisho ya hiyo miradi na mbaya zaidi uchumi hautakuja kuka vizuri hivi karibuni. Madhara ya corona kiuchumi yanaweza kuja kukaa vizuri baada ya miaka kadhaa mbele.

Hata wahisani wetu wa maendeleo sina hakika kama watatoa hela maana wao ndio wameathirika zaidi. Njia pekee itakua ni mikopo na mikopo hiyo itakua ni eitha WB au IMF, tegemea masharti ya kuachana na miradi kama hii.

Tusubiri tuone itakuaje.
Hii miradi ya SGR na Stiglers Gorge hata bila corona ni miradi unaitwa WHITE ELEPHANTS. Unaweza ukaimaliza lakini isikupe Desired Return on Investment.

Kwa mfano SGR hata ikimalizika kwenda huko Rusumo sijui ambako tuna target mzigo wa Rwanda, bado haina faida kwa vile throughout ya Rwanda ni less than 800k metric tons.

Mzigo wa ndani ni very insignificant kwa vile Magufuli hana vision. Anajenga reli huku anaua sekta binafsi. Umefirisi akina Yusuf Manji, umewatisha kina Mo Dewji kwa kuwateka, umesababisha vifo vya akina Mufuruki na Shamte kwa chuki zako, Je unategemea local traders gani wasafirishe mzigo kwenye SGR?

Hiyo Stiglers Gorge ni upotevu wa Matrilioni ya hela tu kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo adui mkubwa wa hydro electricity. Kamwe hawezi kupata hizo megawatt 2100 kama anavyotamba kwenye maradhi na matv.

Ataishia kuharibu baioanuai ya selous tu na kuteremsha hadhi ya pori tengefu
 
Hiyo "force majeure" inatupa haki ya kumuondoa magufuli ikulu.
Nyie wapambe nuksi!!!
Mkuu Jogi, I doubt!. Kunapotokea mazingira ya force majeure, kila mmoja anaubeba mzigo wake mwenyewe!.
P
 
SGR na Umeme wa bonde la nyerere ni uwekezaji mkubwa kimkakati kwa maendeleo ya taifa! Hiyo miradi lazima ikamilike kwa gharama yoyote! Hii miradi piga ua lazima ikamilike hata kwa watumishi kupunguzwa au kulipwa nusu mishahara! Bado bandari hipo inapitisha mizigo kwa nchi zaidi ya 8 hela itapatikana!
"Piga ua lazima ikamilike..."

Ni kweli itakamilika tu.
 
Mkuu Jogi, I doubt!. Kunapotokea mazingira ya force majeure, kila mmoja anaubeba mzigo wake mwenyewe!.
P
Kiwepo kipengele, kama hakipo imekula kwetu.
Atakayebanwa na "force majeure" ataungana na Donald Trump kumshtaki mchina.

Watanzania wengi mno hawaifurahii miradi hii ambayo magufuli "anatusogoma" (nimekosa tafsiri rasmi la neno hilo la kigogo)
 
Vipi unajua chochote kuhusu Bandari ya Bagamoyo?. Nani alianzisha?, alipoingia mwingine do you know what happened?.
Vipi unajua chochote kuhusu Katiba mpya?. Do you know how much we spent?. Do you know aliyefuata, amefanya nini?.
P
Sio sheria kwamba kila anayeingia hapo ikulu ni lazima atelekeze miradi ya mtangulizi wake, huenda akaja mwingine akaendeleza, hivyo tusiishi kwa kukariri.
 
Sio sheria kwamba kila anayeingia hapo ikulu ni lazima atelekeze miradi ya mtangulizi wake, huenda akaja mwingine akaendeleza, hivyo tusiishi kwa kukariri.
Historia inaonyesha kila mtu hua anakuja na vipaumbele vyake.
 
Vipi unajua chochote kuhusu Bandari ya Bagamoyo?. Nani alianzisha?, alipoingia mwingine do you know what happened?.
Vipi unajua chochote kuhusu Katiba mpya?. Do you know how much we spent?. Do you know aliyefuata, amefanya nini?.
P

Naona ile mada yangu ya katiba mpya imeibuka huku kinamna.
 
hiyo miradi ilikufa kabla ya kuanza. huwezi kufanikiwa kutekeleza miradi mikubwa kama ile huku unajitia maskini jeuri unawaita wazungu mabeberu. siku zote chunga ulimi.
 
Back
Top Bottom