Kuna uwezekano mkubwa Rais Samia kuonana na wakuu wa Serikali ya Marekani akiwamo Rais Joe Biden

Kuna uwezekano mkubwa Rais Samia kuonana na wakuu wa Serikali ya Marekani akiwamo Rais Joe Biden

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kuna uwezekano mkubwa wa Rais Samia kuonana ana kwa ana na wakuu wa Serikali ya Marekani akiwamo Rais Joe Biden kwenye ziara yake hii.

Ifahamike mambo ya ugaidi wa kubambikiziana tumeshaachana nayo na tumeonyesha nia njema ya kuzungumza na wapinzani katika hatua mbalimbali. Ikumbukwe pia kuna vita vya Russia na Ukraine ambako tumekuwa hatueleweki eleweki.

Tutakuwa tuna maelekezo yetu huko. Muda wetu wa kupiga kura kwa kuwajibika (responsibly) utakuwa umefika.

Bila shaka tukavuna pia na pesa za kutosha japo kupoza poza makali ya maisha na mfumuko wa bei. "Punde na Warusi wa Buza tutakuwa tunaongea lugha moja." Ya msingi zaidi kwetu ni kufunguliwa zaidi kwa milango ya demokrasia.

"Hii ikiwamo haki zetu, kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na hatima ya waathirika wote wa figisu za kisiasa nchini." Tumtakie mama safari njema ya mafanikio tele.

========================

Rais Samia kukutana na Makamu Rais wa Marekani

Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris anatarajiwa kukutana na Rais Samia Suluhu ambaye yupo katika ziara Nchini humo siku yoyote hivi karibuni.

Ofisi ya Rais wa Marekani, Joe Biden imetoa taarifa hiyo ambapo wanatarajiwa kukutana Ikulu ya White House ambapo watajadiliana kuhusu uchirikiano wa kiuchumi na biashara na masuala mengine ya kidunia.

Source: EconoTimes
 
Hayawi hayawi huwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa rais Samia kuonana ana kwa ana na wakuu wa Serikali ya Marekani akiwamo rais Joe Biden kwenye ziara yake hii.

Ifahamike mambo ya ugaidi wa kubambikiziana tumeshaachana nayo na tumeonyesha nia njema ya kuzungumza na wapinzani katika hatua mbalimbali.

Ikumbukwe pia kuna vita vya Russia na Ukraine ambako tumekuwa hatueleweki eleweki.

Tutakuwa tuna maelekezo yetu huko.

Muda wetu wa kupiga kura kwa kuwajibika (responsibly) utakuwa umefika.

Bila shaka tukavuna pia na pesa za kutosha japo kupoza poza makali ya maisha na mfumuko wa bei.

"Punde na warusi wa Buza tutakuwa tunaongea lugha moja."

Ya msingi zaidi kwetu ni kufunguliwa zaidi kwa milango ya demokrasia.

"Hii ikiwamo haki zetu, kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na hatima ya waathirika wote wa figisu za kisiasa nchini."

Tumtakie mama safari njema ya mafanikio tele.
Kwa sifa hizi hapa kwa nini asizulu? Ikulu ya while House pale kuna VP mwanamama.👇

Screenshot_20220413-192506.png

20220412_105242.jpg
 
Hayawi hayawi huwa.

Kuna uwezekano mkubwa wa rais Samia kuonana ana kwa ana na wakuu wa Serikali ya Marekani akiwamo rais Joe Biden kwenye ziara yake hii.

Ifahamike mambo ya ugaidi wa kubambikiziana tumeshaachana nayo na tumeonyesha nia njema ya kuzungumza na wapinzani katika hatua mbalimbali.

Ikumbukwe pia kuna vita vya Russia na Ukraine ambako tumekuwa hatueleweki eleweki.

Tutakuwa tuna maelekezo yetu huko.

Muda wetu wa kupiga kura kwa kuwajibika (responsibly) utakuwa umefika.

Bila shaka tukavuna pia na pesa za kutosha japo kupoza poza makali ya maisha na mfumuko wa bei.

"Punde na warusi wa Buza tutakuwa tunaongea lugha moja."

Ya msingi zaidi kwetu ni kufunguliwa zaidi kwa milango ya demokrasia.

"Hii ikiwamo haki zetu, kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na hatima ya waathirika wote wa figisu za kisiasa nchini."

Tumtakie mama safari njema ya mafanikio tele.
Samia Ni mjanja aliona akiongoza kwa mkono wa chuma Kama JPM, hatofanikiwa kwa mabeberu, afu kesi ya Mbowe ilikuwa imemuharibia vibaya Sana, nadhani sahivi ana amani kwenda nchi za magharibi, lakini ukweli Ni kwamba CCM hawapendi upinzani sema njaa zao kwa mabeberu ndo zinafanya waufyate
 
Mkuu hata kenya wapinzani walikomalia misaada ya mabeberu ndo ikapatikana democracy
 
Huu uzi ni wa Pro USA kuwa neutral ni jambo la busara kuliko vyote. Tuendelee kubaki na msimamo wetu shida mmezoea vya kupewa pewa vyenye masharti lini tutajitegemea ??

Tutaendelea kuwa waoga na kuomba misaada mpaka lini?
Ungekuwa wewe Rais ungefanyaje kwa mfano. Tueleze ungefanyaje. Hapa sio issue ya kuomba omba wala nini wala kijitegea ni diplomasia ambayo nadhani wengi hatujui tuwaachie viongozi wetu wakatende wanaipenda nchi yetu.
 
Dikteta aliharibu mentality za vijana wengi, wamekuwa mazuzu kabisa......
 
ebu niambie Nchi gani ya Africa ambayo haipewi misaada na hao wazungu? na hakuna Rais ambae kwenye uongozi wake hajawai kupewa au kuomba hela kwa Nchi wahisani, Magufuli alikuwa anawadanganya nyinyi tu ambao huelewi wenu aliuharibu kabisa,

Magufuli anaingiaje kwenye hii thread? Huna hoja
 
Huu uzi ni wa Pro USA kuwa neutral ni jambo la busara kuliko vyote. Tuendelee kubaki na msimamo wetu shida mmezoea vya kupewa pewa vyenye masharti lini tutajitegemea ??

Tutaendelea kuwa waoga na kuomba misaada mpaka lini?
Akitoka huko aende Russia then Ukrain ili kuonyesha kuwa tuko neutral kikwelikweli
 
ebu niambie Nchi gani ya Africa ambayo haipewi misaada na hao wazungu? na hakuna Rais ambae kwenye uongozi wake hajawai kupewa au kuomba hela kwa Nchi wahisani, Magufuli alikuwa anawadanganya nyinyi tu ambao huelewi wenu aliuharibu .
Muache Magufuli apumzike
 
Back
Top Bottom